Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dah..yaani mtoto anafikisha miaka 13...yule jamaa anarudisha majeshi.......halafu mwamba unawekwa kando .....wanawake hawa.......dah 🤭 🤣Mkuu wewe ni time Traveller uliishi zama za Yesu sasa umerudi katika ulimwengu huu[emoji23][emoji23][emoji23] Sema anyway itakuwa unampenda sana huyo mdada lakini Angalia usiwe unategemea kulipwa wema 100% huyo dada anaweza kuendeleza mechi za ugenini na Jamaa aliekataa mimbaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Maana wanawake achana nao mkuu.
Stori za vijiwe vya kahawaNI MAAMUZI MAGUMU LAKINI YAMETOKA MOYONI
Wapendwa wana jukwa hili la mahusiano, mapenzi na urafiki ninawasalimu nyote.
Kama habari ya awali inavyosemaka kuwa nimechukua uamuzi mgumu wa kuwa baba mtarajiwa wa mtoto mtarajiwa wa rafiki yangu kwa hiyari na kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nitakazo zieleza hapa chini, lakini kabla ya hizo sababu naomba nitoe ufafanuzi wa urafiki wetu.
Kuna dada mmoja tulikutana ofisi flani ya serikali, ni dada flani mpole kiasi na mcheshi kiaina. Kwa muda mfupi sana nilivutiwa naye na ikafikia hatua ya kubadilishana naye namba za simu.
Zoezi la huduma lilienda vyema kwa yeye kufanya koneksheni na mtumishi flani na tukafanikiwa kupata hiyo huduma (pass ya kusafiria kwa haraka)
Baada ya hapo hatukuwasiliana haraka japo nilipanga lazima nimtafute. Ulifika wakati tukaanza kuwasiliana hapa na pale. Na ukafika wakati nikawa nachomekea viutani kuwa ninamhitaji awe rafiki yangu.
Baada ya muda mrefu tulifanikiwa kuwa marafiki hatimaye tukaanza kushirikiana....hapa wakubwa mmeelewa. Jambo nililompenda zaidi ni mwelewa na mwenye misimamo yake mizuri. Tuliwekana wazi kuhusu mahusiano yetu, kwake yeye mpenzi wake alikuwa ni raia wa kigeni na anaishi huko kwao huja mara chache hivyo alikuwa anajiandaa kwenda kumtembelea na walikuwa wamepanga kuoana.
Nini kilitokea kati yao?
Uliwadia wakati wa kusafiri alinijulisha nami nilimpa nafasi ya kuwa mbali naye kimawasiliano ili ajiweke sawa na akili yake iwaze juu ya mpenzi wake. Alifanikiwa kwenda na kurudi. Baada ya kurudi mawasiliano yetu yalikuwa hafifu kwani nilikuwa tight sana na kazi.
Baada ya miezi kama mitatu na nusu, tuliwasiliana na kupiga stori nyingi na mwishowe akanijulisha ni mjamzito. Nikampa hongera zake. Lakini mawasiliano yakazidi kuwa hafifu zaidi. Ukafika wakati nikamuuliza maendeleo na mipango ya ndoa na kama wamepanga lini wataanza kuishi pamoja?
JIBU LAKE NDILO HASA LILINIGUSA NA KUAMUA HAYA
Rafiki yangu huyu alinishtua aliponieleza kuwa walitengana na yule mchumba kwani walipokutana ughaibuni alimfanyia visa vingi vibaya mno..sitavitaja
Na alipotua nchini alimtumia ujumbe kuwa asimtafute tena. Akiwa katika hali ya kutafakari yaliyompata na jinsi gani atasonga mbele...ndipo alianza mahusiano na jamaa flani aliyeanza kumnyemelea kitambo na muda mfupi akapata ujauzito.
Baada ya kupata ujauzito alimjulisha mhusika lakini hakuwa tayari kuukubali bali alimwambia autoe kwani yeye anafamilia lakini aligoma kuutoa na akajiapiza ataulea na kwa vile jamaa ameukataa hata jina litakuwa la upande wa familia yake yaani ubini wa baba.
Habari hii iliniumiza sana na niliwaza haya yafuatayo;
1. Kuwa huyu dada ataishi kwa sonono kubwa wakati wa ujauzito na atamwathiri mtoto akiwa tumboni wazazi wanajua hili
2. Huyu atakayezaliwa hatakuwa na upendo katika jamii na anaweza kuja kuwa na tabia ya ajabu
MAAMUZI YANGU
1. Nikamwomba kama naweza kuwa baba wa wa hiyari na apewe ubini wa jina langu kama baba alikubali hili kwa mshangao mkubwa sana (Haya[emoji116]sijamshirikisha)
2. Nitamhudumia kipindi chote cha ujauzito
3. Nitamfanya mwenye furaha ili kulinda afya mama na ya mtoto atakaye zaliwa
4. Baada ya mtoto kukua yeye yuko huru kuwa na maisha yake bila mimi kumwingilia uhuru wake
5. Nitampa mtoto kiwanja na kumjengea kadri Mungu atakaponiweka hai na kunibariki, ili apate malazi na malezi bora.
Uamuzi huu nimeufanya mwenyewe japo sipangi kuishi na mtoto isipokuwa kumsapoti kimalezi tu.
Baada ya kukubaliana naye hasa kuhusu mtoto kuitwa kwa jina langu kama baba, alifurahi sana kiasi cha kulia machozi na nikamwahidi kuwa siku chache zijazo atakuja mkoa nilipo apate mapumziko ya muda mfupi sio nyumbani kwangu lakini. Amemweleza mama yake mzazi na hajaamini kuwa kuna mtu anaweza kufanya maamuzi magumu kiasi hiki.
Pamoja na hayo sijamweleza kwa undani namna nilivyojipanga kumsapoti mtoto hasa kumpa eneo na kumjengea, hili nimebaki nalo nikiomba Mungu aniwezeshe kulitimiza.
Wapendwa wana jf, inaweza kuonekana kuwa uamuzi wangu ni wa kijinga sana lakini kwangu mimi nitaona fahari kubwa kama hili litafaniniwa kwani;
Sisi wanaume tunapaswa kuwa chemichemi ya furaha ya wake zetu, mama, watoto na dada zetu lakini kinyume chake tumekuwa ni chanzo cha machozi.
Tujitahidi sana kuwafanya watu kuwa na furaha badala ya machozi. Muwe na wakati mwema wote.
Wazazi wako unawasaidia kweli? Una matatizo sio bure.
Sina uhitaji naye bali kumvusha tuMkuu unawajua wanawake kweli wewe?[emoji3][emoji3][emoji3]. Sawa hongera kwa moyo wa kujitoa na kila mtu humu atakupa Hongera na Mimi nakupa hongera. Lakiniii unawajua wanawake vizuri kweli mkuu?
I see!Sio majungu mkuu ila binafsi ninavojua wanaojielewa hasa WANAUME wanatoa msaada bila kujitangaza kuwa wamesaidia.
Kwa mawazo yangu finyu kitendo cha kutoa taarifa hapa ni kuwa unampenda huyo dada umeleta uzi kisomi kupata ushauri.
USHAURI:kama unampenda oa yaani oa bila kujali ni single mama.
Hujui nini maana ya wivu wewe. Uhaisia ndo huo alichoandika hapa ni jinsi anavyowaza ila haiwezekani😂😂😂😂Sioni kama kutakuwa na tatizo maana mtoa mada hajasema kuwa atakuwa mke wa pili, amesema atampa uhuru kwenye upande wa kimahusiano
Hiyo cheers naipokea kishingo upande [emoji2][emoji3][emoji3] maana wananifilisi kwa kweli, napenda watoto wengi lkn cha moto nakiona[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
The good thing is you are responsible.
[emoji1635][emoji1635] Cheers.
Kumbuka inaelekea ni wewe ndiye uliyonekana kuwa front katika kubeba huo mzigo maana yeye alishakupotezea ukawa unamtafuta..Nimeelezea kwa kina sana mkuu.
My concern ni kumvusha kipindi hiki kigumu na kuandaa mazingira bora ya kijacho tu.
amu saidia hili
Unachosema ni kweli kabisa, waliokwisha badilishana damu ngumu sana upendo wao kufa moja kwa mojaMa single. Maza wengi diniani wanasumbuliwa na nyumbani za kupanga. Mi staki umpe upendo kiviiiile, maana una wengi wa kuwapenda ikiwemo familiya yako na mama yako,na wengine wajao, Hata ukikutana ma Mimi leo huyo mbona utamsahau![emoji16] kabla hilo halijatokea wewe MPE nyumbani tu Mungu atakubariki.
Maisha ya usingle mother ni kama kamali, naona umejitoa hadi raha, lakini nature ya usingle mother unaweza ifunye hiyo furaha ulopanga kutoweka, mtoto akizaliwa huwa ni mtamu, baba yake lazima aanze uchokozi, weekend ukiwa kwa mkeo, huyo Dada akakupigia hupokei,unaogopa kuharibu kwa mkeo, Dada mchepuko anapata upweke na hasira, Mara SMS ya mzazi mwenzie inaingia " najua unanichukia ila mm nakupenda, Mke wangu ndo kikwazo, plz njoo umchukulie mtoto matumizi, plz Niko chini ya figo zako"[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji2]
Mstari wa mwisho nitaufanyia kazi siku zoteKumbuka inaelekea ni wewe ndiye uliyonekana kuwa front katika kubeba huo mzigo maana yeye alishakupotezea ukawa unamtafuta..
Dunia haipo kama jinsi uionavyo hizo jitihada za wewe kumtafuta believe me ni nguvu za kukuaribia future yako kupitia huyo mama...
Trust me scenario za hivi huwa zina bitter end.
Kusaidia MTU ni jambo jema tena sana but take extra precaution namna unavyoenda kuhandle hii issue. All the best