Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe mlikuwa mnaibana Sina haja ya kujiuliza kwa nini aliachwa...hongera baba k naona unahisi huenda mimba ni yako maana mlikuwa mnachanganywa 3 kwa mpigoMkuu mimi sina tatizo na mahusiano yake mapya, huruma iko kwa mtoto anayekataliwa na hana hatia.
Katika mapenzi sihitaji huruma, ni simba ninayejua kuwinda mawindo manono.
Sina mashaka na uwezo wangu katika misimamo katika mapenzi.
Yuko huru kuolewa na yeyote mtoto akikua.
Ukisoma vizuri hapo juu sisi tulikuwa tunaibana na kila mtu alikuwa na mahusiano yake.
Kiongozi naona usonge mbeleNI MAAMUZI MAGUMU LAKINI YAMETOKA MOYONI
Wapendwa wana jukwa hili la mahusiano, mapenzi na urafiki ninawasalimu nyote.
Kama habari ya awali inavyosemaka kuwa nimechukua uamuzi mgumu wa kuwa baba mtarajiwa wa mtoto mtarajiwa wa rafiki yangu kwa hiyari na kwa kupenda mwenyewe kwa sababu nitakazo zieleza hapa chini, lakini kabla ya hizo sababu naomba nitoe ufafanuzi wa urafiki wetu.
Kuna dada mmoja tulikutana ofisi flani ya serikali, ni dada flani mpole kiasi na mcheshi kiaina. Kwa muda mfupi sana nilivutiwa naye na ikafikia hatua ya kubadilishana naye namba za simu.
Zoezi la huduma lilienda vyema kwa yeye kufanya koneksheni na mtumishi flani na tukafanikiwa kupata hiyo huduma (pass ya kusafiria kwa haraka)
Baada ya hapo hatukuwasiliana haraka japo nilipanga lazima nimtafute. Ulifika wakati tukaanza kuwasiliana hapa na pale. Na ukafika wakati nikawa nachomekea viutani kuwa ninamhitaji awe rafiki yangu.
Baada ya muda mrefu tulifanikiwa kuwa marafiki hatimaye tukaanza kushirikiana....hapa wakubwa mmeelewa. Jambo nililompenda zaidi ni mwelewa na mwenye misimamo yake mizuri. Tuliwekana wazi kuhusu mahusiano yetu, kwake yeye mpenzi wake alikuwa ni raia wa kigeni na anaishi huko kwao huja mara chache hivyo alikuwa anajiandaa kwenda kumtembelea na walikuwa wamepanga kuoana.
Nini kilitokea kati yao?
Uliwadia wakati wa kusafiri alinijulisha nami nilimpa nafasi ya kuwa mbali naye kimawasiliano ili ajiweke sawa na akili yake iwaze juu ya mpenzi wake. Alifanikiwa kwenda na kurudi. Baada ya kurudi mawasiliano yetu yalikuwa hafifu kwani nilikuwa tight sana na kazi.
Baada ya miezi kama mitatu na nusu, tuliwasiliana na kupiga stori nyingi na mwishowe akanijulisha ni mjamzito. Nikampa hongera zake. Lakini mawasiliano yakazidi kuwa hafifu zaidi. Ukafika wakati nikamuuliza maendeleo na mipango ya ndoa na kama wamepanga lini wataanza kuishi pamoja?
JIBU LAKE NDILO HASA LILINIGUSA NA KUAMUA HAYA
Rafiki yangu huyu alinishtua aliponieleza kuwa walitengana na yule mchumba kwani walipokutana ughaibuni alimfanyia visa vingi vibaya mno..sitavitaja
Na alipotua nchini alimtumia ujumbe kuwa asimtafute tena. Akiwa katika hali ya kutafakari yaliyompata na jinsi gani atasonga mbele...ndipo alianza mahusiano na jamaa flani aliyeanza kumnyemelea kitambo na muda mfupi akapata ujauzito.
Baada ya kupata ujauzito alimjulisha mhusika lakini hakuwa tayari kuukubali bali alimwambia autoe kwani yeye anafamilia lakini aligoma kuutoa na akajiapiza ataulea na kwa vile jamaa ameukataa hata jina litakuwa la upande wa familia yake yaani ubini wa baba.
Habari hii iliniumiza sana na niliwaza haya yafuatayo;
1. Kuwa huyu dada ataishi kwa sonono kubwa wakati wa ujauzito na atamwathiri mtoto akiwa tumboni wazazi wanajua hili
2. Huyu atakayezaliwa hatakuwa na upendo katika jamii na anaweza kuja kuwa na tabia ya ajabu
MAAMUZI YANGU
1. Nikamwomba kama naweza kuwa baba wa wa hiyari na apewe ubini wa jina langu kama baba alikubali hili kwa mshangao mkubwa sana (Haya[emoji116]sijamshirikisha)
2. Nitamhudumia kipindi chote cha ujauzito
3. Nitamfanya mwenye furaha ili kulinda afya mama na ya mtoto atakaye zaliwa
4. Baada ya mtoto kukua yeye yuko huru kuwa na maisha yake bila mimi kumwingilia uhuru wake
5. Nitampa mtoto kiwanja na kumjengea kadri Mungu atakaponiweka hai na kunibariki, ili apate malazi na malezi bora.
Uamuzi huu nimeufanya mwenyewe japo sipangi kuishi na mtoto isipokuwa kumsapoti kimalezi tu.
Baada ya kukubaliana naye hasa kuhusu mtoto kuitwa kwa jina langu kama baba, alifurahi sana kiasi cha kulia machozi na nikamwahidi kuwa siku chache zijazo atakuja mkoa nilipo apate mapumziko ya muda mfupi sio nyumbani kwangu lakini. Amemweleza mama yake mzazi na hajaamini kuwa kuna mtu anaweza kufanya maamuzi magumu kiasi hiki.
Pamoja na hayo sijamweleza kwa undani namna nilivyojipanga kumsapoti mtoto hasa kumpa eneo na kumjengea, hili nimebaki nalo nikiomba Mungu aniwezeshe kulitimiza.
Wapendwa wana jf, inaweza kuonekana kuwa uamuzi wangu ni wa kijinga sana lakini kwangu mimi nitaona fahari kubwa kama hili litafaniniwa kwani;
Sisi wanaume tunapaswa kuwa chemichemi ya furaha ya wake zetu, mama, watoto na dada zetu lakini kinyume chake tumekuwa ni chanzo cha machozi.
Tujitahidi sana kuwafanya watu kuwa na furaha badala ya machozi. Muwe na wakati mwema wote.
(KATIKA HILI SITEGEMEI ANY RETURN)
Too late mkuuKiongozi naona usonge mbele
Ila ushauri wa ziada; kwa nini usimuoe huyo dada akatulia na kuemuepushia kuzalishwa tena hapo baadae
Naamini atakuheshimu down to Earth na hata ukioa mwingine; believe me itakuwa vigumu sana kupata mtu wa kukuheshimu kama huyo...
NI MAAMUZI MAGUMU LAKINI YAMETOKA MOYONI

hiyo ni karama yako mkuuSaidia na wewe pia
Watoto wanahitaji msaada wa Baba. Kuna matukio yanahitaji msaada wa Baba na kisaikolojia Baba ni muhimu sana.Akiwa na maana gani??
Wewe ni malaika.[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]watabiri bhana hamuwazagi positive hata siku moja.
Nimejaribu kusapoti jamii mara kadhaa.
Nimewahi sapoti mama mmoja wakati wa uzazi mwanzo mwisho hadi alipoweza kujitegemea kibiashara...alikimbiwa na mume na msaada ulikuwa unapitia mtu mwingine na hakujua anayemsapoti hadi baadae sana.
...Nimesapoti mabinti 2 kusoma hadi chuo kikuu bila kutaka hata ukaribu bali kulipa ada zao tu tena nimeanza nikiwa kijana mdogo.
Katika hili sina wasiwasi ninachoomba ni afya njema.
Sifungwi na sijaahidi kufanya makubwa kupita uwezo wangu bali sawa na uwezo atakao nipa Mungu.
Kwani mm nimekataa Haya yote usifanye? Fanya hata zaidi ya hayo. Ahaaaa ati ni heshima na urafiki wa kawaida? Nachojua things change.Haya baba nimekubali ni urafiki wa kawaida, ila ninachoamini, akili ya kichwa kidogo haijawai mwacha mwanaume salama. All the best.[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Eti???
Nisimpende hivyo???
Kwa kifupi ninayemhurumia ni yule aliyekataliwa.
Sioni nafasi ya upendo wetu kuendelea zaidi ya heshima na urafiki wa kawaida.
Sikusudii kumfanya kuwa karibu yangu zaidi ya kumpa sapoti ndogo ndogo wakati huu mgumu kwake.
Ninajua thamani ya mtu kukukali ngaa kidogo wakati wa mapito yako magumu.
Ni hivyo tu Lucky