Omerta
JF-Expert Member
- Jan 3, 2016
- 5,957
- 7,505
Anaendelea na maisha yake akiwa wapi?Hahusiki kabisa na kesi hiyo na anaendelea na maisha yake.
Wacha uongo wewe utalaanika
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Anaendelea na maisha yake akiwa wapi?Hahusiki kabisa na kesi hiyo na anaendelea na maisha yake.
Pole sana ,kapotelea mikononi mwa hili jeshi la kigaidi?Mimi shemeji yangu mpaka leo hajulikani alipo Sister kalia mpaka kashukuru Mungu
Aahh ok sawa Mkuu... sio ushindi kwa akina Mbowe; ni DPP hana nia ya kuendelea na kesi tena; hii hufanyika kabla mahakama haijatoa hukumu. Kesi itafunguliwa upya kwa ushahidi ulioboreshwa.
Katika nchi zetu za kiafrika watawala wetu maamuzi yao ndo huwa sheria zenyewe. So hata huyo DPP yupo kama kiinimacho tu hana meno.Anateuliwa na Rais na anafanya kazi kwa matakwa ya katiba ya JMT!
Alaanike Zero. Yaani hili kundi lake, ni aheri hata ya majambazi.Ushahidi wa huyu mke umenitoa machozi,
Samia ameishi kwenye uovu kwa miaka mitano. Ameuishi uovu kwa miaka 5. Ameufurahia uovu kwa miaka mitano. Hata akitaka kutoka, hawezi kutoka ghafla kwa 100%. Ni lazima ile roho ya uovu itaendelea kuwa ndani yake.Kwa hiyo Samia kwanini asitoe amri ya kufutwa hii case?
Hivi ni nani alisema kule BBC kuwa watuhumiwa wengine wa hii case walisha kiri makosa na kuhukumiwa?
Angekuwa haitaki hii case angeifuta toka mwanzo wakati Mbowe ana kamatwa.
Lazima tukubali hii case imechangiwa sana na vugu vugu la katiba mpya.....
Hii case ina ushawishi wa Rais aliyeko madarakani wala usitetee....
Tunasubiri hukumu ya kesi ndogoJe itabidi kwanza tusubiri hukumu ya hii kesi ndogo ama tunaendelea na shauri la msingi?
Pamoja na pongez kwa Jaj, ata huyu mama amekuwa jasiri. Yaan ushahid wa uongo na wa ukweli ni haraka kuwatambua...haya ni maneno ya faraja sana toka kwa Jaji, Ubarikiwe Jaji kwa kumtia nguvu shahidi, maana wamama huwa wana majonzi sana - anaweza kuanza kulia na kushindwa kutamka neno lolote lile
Ipo siku watalipia huo uhuni waoHapa nimejifunza kwamba polisi ndio hatari kuliko jambazi.
Samia ameishi kwenye uovu kwa miaka mitano. Ameuishi uovu kwa miaka 5. Ameufurahia uovu kwa miaka mitano. Hata akitaka kutoka, hawezi kitoka ghafla kwa 100%. Ni lazima ile roho ya uovu itaendelea kuwa ndani yake.
Hata pale anapokuwa na dhamira ya kutenda mema, kuna wakati atatumia uzoefu alio nao, ambao ni uovu.
Kwa hiyo kwenye hili kuna mkono wake na ile roho ya uovu aliyoiishi kwa miaka 5.
Kazi IPO..Mimi binafsi yangu nauona ukweli kuwa hawa mabwana wametungiwa KESI.. Hakika kuna watu hawana hofu ya Mungu kabisa.Karibuni hapa kwa updates kutoka mahakama ya uhujumu uchumi kwenye kesi namba 16 ya mwaka 2021 inayomuhusu mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu...
Watuhumiwa tayari wamefikishwa mahakamani, leo shahidi wa tatu upande wa utetezi ataanza kutoa ushahidi wake.
View attachment 1956923
Mawakili upande wa Utetezi tayari wapo katika ukumbi wa Mahakama. Mawakili upande wa Mashtaka bado wapo Nje.
-------------------------------------------------------------------------
Jaji ameshaingia Sasa Mahakamani, kesi inatajwa.
Wakili wa Serikali: naomba radhi tumeingia wakati umeshaingia
Jaji: sawa
Wakili wa Serikali: Kidando Wakili wa Serikali anatambulisha wenzake
1. Robert Kidando2. Nassoro Katuga3. Ignas Mwanuka4. Esther Martin5. Tulimanywa Majigo
Kibatala: anatambulisha Wenzake
Adv. Peter KibatalaAdv. Jonathan MndemeAdv. Fredrick KiwheloAdv. John MalyaAdv. Sisty AloyceAdv. Alex MasabaAdv. Idd MsawangaAdv. Gaston GarubindiAdv. Evaresta KisangaAdv. Faraj MangulaAdv. Maria MushiAdv. Bonifasia Mapunda
Wakili Dickson Matata: anaombewa Ruhusa Mdogo wake anafanyiwa Operesheni Hospitali ya Lugalo
Jaji: Wakili wa Serikali
Wakili wa serikali: Tumekuja kwa ajili ya kesi ndogo ambapo Shahidi wa tatu yupo tayari kuendelea Kutoa Ushahidi wake
Jaji: John Mallya
Mallya: Tunaye, na Shahidi yupo tayari kutoa Ushahidi
Jaji: anaandika Kidogo na Ukimya wa Mahakama
Jaji: Shahidi wa 3 upande wa Utetezi ambaye ameandaliwa Tafadhali anaweza Kuja
Shahidi Mdada anatokea Nyuma kabisa ya Chumba Cha Mahakama anaenda Kizimbani
Jaji: Shahidi upo Mahakamani ondoa Hofu, nitakuuliza Majina yako na Nitakuapisha, Wakili wa Utetezi atakuongoza na Mawakili wengine watakuuliza Swali na Mawakili wa Serikali watakuuliza Maswali, pia huna Haja ya Kuogopa, tupo hapa kutafuta Haki.
Jaji: Shahidi unaitwa nani
Shahidi: Lilian Kibona, Dini Mkristo Shahidi Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa Ukweli na Ukweli Mtupu, Mungu ni Saidie.
Jaji: Liliani utachagua Kukaa au Kusimama, Hata Ukikaaa nitakuona.
Jaji: wakili Mallya endelea
Mallya: Shahidi Unaishi wapi
Shahidi: Chalinze Mkoa wa Pwani
Mallya: sehemu gani huko Chalinze
Shahidi: Ramboni
Jaji: ni Mtaa.?
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Unaishi na nani..?
Shahidi: Na mme wangu na Watoto ambaye kwa Sasa Mme wangu ameshikiliwa.
Jaji: ni Miongoni Mwa washitakiwa?
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Mme wako anaitwa nani?
Shahidi: Adamu Khalfani Kasekwa
Mallya: hapa nitakuwa namuita Mshitakiwa wa Pili nitakuwa namaanisha pia ni yeye
Shahidi: ndiyo
Mallya: Mmeoana lini, 05/08/2016, Ndoa Ya Kiserikali
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Mlikuwa mnaishi wapi
Shahidi: Pale pale Chalinze
Mallya: unaweza Kukumbuka Mme wako alikuwa anafanya kazi gani wakati huo
Shahidi: Askari Jeshi la JWTZ, kikosi cha 92 Ngerengere
Mallya: alikuwa anafanya kazi gani Nyingine
Shahidi: alikuwa hana kazi Nyingine zaidi ya hiyo ya Serikali
Mallya: naruka nakuja 2020 Mme wako alikuwa anafanya kazi gani
Shahidi: alikuwa anafanya shughuli zake za Biashara
Mallya: Mwanzoni Mwa Mwezi wa Nane Mwaka 2020 unakumbuka Kilitokea Kitu gani kati yako na Mme wako
Shahidi: Mme wangu alikuwa Moshi, tulikuwa tunawasiliana naye Vizuri
Mallya: Kabla ya Kwenda Moshi mlikuwa na Hali gani kati yako na Mme wako
Shahidi: Palikuwa na Mawasiliano
Mallya: kabla hajaenda Moshi kitu gani kilitokea
Shahidi: Rafiki yake Ling'wenya waliwasiliana kuwa kuna Kazi imepatikana Moshi
Mallya: Unaweza Kukumbuka Siku na Saa ya hayo mawasiliano
Shahidi: Hapana sikumbuki
Jaji: unasema palikiwa na Mawasiliano Kati ya Mme wako na Ling'wenya .?
Shahidi: Ndiyo Kwamba Ling'wenya alimpigia Simu kuwa kuna kazi Imepatikana Moshi
Jaji: Ndiyo
Mallya: Simu zilikuwa zinapigwa kati ya Ling'wenya na Mme wako, wewe ulijuaje
Shahidi: Mimi Kama Mke wake alinishirikisha, Mimi kama Mke nilimruhusu
Mallya: Jambo gani lilifanyika, kabla ya Mme wako kwenda Moshi
Shahidi: Nakumbuka walikutana na Ling'wenya wakaenda Kwanza Morogoro, Wakarudi, Waliporudi wakajiandaa Wakaenda Moshi
Mallya: Hali ya Mme wako kiAfya Wakati anaenda Moshi hali yake ilikuwaje
Shahidi: Ilikuwa Nzuri inamruhusu kwenda Kufanya kazi
Mallya: Hali Nzuri unamaanisha nini ,Mwambie Mheshimiwa Jaji
Shahidi: haumwi na Kwamba anaweza Kwenda Moshi
Mallya: kitu gani kilifuata baada ya Kwenda Moshi
Shahidi: alinitaarifu kuwa amefika Moshi
Mallya: mlikuwa mnatumia Njia gani kufanya mazungumzo
Shahidi: kwa Njia ya Simu
Mallya: Siku ya Tarehe 05/08/2020 kitu gani kilitokea
Shahidi: alinipigia na akaongea na watoto, tulipokuwa tunaongea akasema Hebu subiri nikamsubiri
Mallya: ilikuwa Saa ngapi
Shahidi: Kama Saa Moja
Mallya: alipokwambia Subiri kidogo nitakupigia Kidogo kitu gani Kilifuata
Shahidi: Nilipoona Muda umeenda ilipofika Saa 10 ilibidi nimpigie, Simu iliita ikawa imepokelewa lakini Kila nikisema Hallo Sisikii Mtu akiongea
Mallya: Unaweza Kukumbuka namba ya Simu uliyopiga, ambayo ulipiga Ikapokelewa.?
Shahidi: Sikumbuki Kichwani lakini ipo kwenye Simu yangu
Mallya: Baadae kilifuata nini baada ya Simu kutokupokelewa
Shahidi: baadae Ikawa haipatikani
Mallya: kitu gani Kilifuata
Shahidi: kwa kuwa nilikuwa na namba ya Mwenzake Ling'wenya nikampigia Ling'wenya
Mallya: baada ya Kumpigia Ling'wenya.?
Shahidi: Ikawa inaita Mpaka jioni, Mpaka Usiku, Mpaka Kesho yake inaita haipokelewi
Mallya: Sasa wewe ulipata hisia gani baada ya kuona Inaita hadi Kesho yake haipokelewi
Shahidi: niliona labda ni Mambo ya Kazi, sikuwa na wasiwasi wowote
Mallya: Wewe ulichukua hatua gani..?
Shahidi: Sikuwa na namna yoyote zaidi ya Kusubiri simu kutoka kwao
Mallya: umesema una mtoto, anaumri gani
Shahidi: Miaka 3 na Miezi 9
Mallya: Nataka kukupeleka Tarehe 09 Mwezi 08 kitu gani Kilitokea
Shahidi: nakumbuka ilikuwa tarehe 09 mwezi 08 Mwaka 2020 niliamka Asubuhi ikiwa siku ya Jumapili, Mtoto alikuwa anasumbuliwa na tumbo
Jaji: Mtoto wa Jinsia gani
Shahidi: Wa kike
Mallya: kwanini Unakumbuka kuwa ilikuwa Siku ya Jumapili
Shahidi: Sababu ilikuwa Siku ya Ibada
Mallya: Ikawaje
Shahidi: Sikwenda Ibadani badala yake nikaenda Hospitali
Mallya: ikawaje huko Hospitali
Shahidi: Nilipokelewa
Mallya: Hospitali gani
Shahidi: Hospitali ya Serikali pale pale Chalinze
Mallya: baada ya Kupokelewa Hospitali
Shahidi: nilipatiwa Huduma nikarudi Nyumbani
Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani
Shahidi: niliona Miguu ya watu kama Imekanyaga, Wakati natoka Nyumbani nilifunga Mlango lakini niliporudi nikakuta Milango ipo wazi
Mallya: Ule Mlango ulikuwa katika hali gani
Shahidi: Mlango ulikuwa wazi na Kitasa nikakuta kimevunjwa
Mallya: kitu gani kikatokea
Shahidi: kwa akili ya haraka haraka nilijua Wezi, Cha ajabu kila kitu nilikuta Vipo, Kitu kama Tv lakini vipo
Mallya: enheeee ikawaje
Shahidi: Nikaingia Chumbani nikakuta Nguo zimemwagwa Chini
Jaji: Za Mme wako
Shahidi: zote zimemwaga,na Mabegi yamefunguliwa
Shahidi: Kuna begi la jeshi alinunua Congo nilipokuja nikakuta halipo
Jaji: ukisema begi la jeshi alinunua Congo unamaanisha nini
Shahidi: Alinunua Congo Begi lenye Mabaka Mabaka ya Jeshi
Mallya: Kitu gani kilifuata
Shahidi: Nilienda Kuuliza Majirani zangu
Mallya: Jirani yako anaitwa nani.?
Shahidi: Judith Charles
Mallya: lengo la kwenda kwa Jirani lilikuwa nini
Shahidi: nilienda Kuuliza kama Mme wangu amekuja Nyumbani.? wamemuona.? kwamba kuna kitu huenda alikuja Kukitafuta kwa haraka haraka
Mallya: Jirani alikwambiaje
Shahidi: Kuna Magari yalikuja hapa Ya Kipolisi, Moja walikuwa wamevaa Sare na Wengine walikuwa Wamevaa Kiraia
Mallya: Taarifa Nyingine alikupa Jirani yako ni Ipi
Shahidi: kwamba Mapolisi walimuita kwa lengo la Kuniulizia Mimi. baada ya hapo Mapolisi walishuka kwenye gari wakaingia Ndani
Mallya: yeye Jirani alikuwa anafanya nini wakati huo
Shahidi: alikuwa anashuhudia wakati wanaingia ndani ya Nyumba yako
Mallya: Kitu gani kingine walikufahamisha au Kumpatia
Shahidi: walisema walichukua Begi, Vyeti vyake vya Kijeshi vya Adamu, Walichukua Hati ya Uwanja, Kadi ya pikipiki
Mallya: Kitu gani Kingine alikwambia
Shahidi: aliongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze
Mallya: aliyeongozana na Mkuu wa Upelelezi wa Chalinze alikuwa ameongozana na akina nani
Shahidi: Jirani yangu aliongozana na Mkuu wa Upelelezi na aliacha namba ya Simu kwa Jirani.
Jaji: kwa ajili ya Nini
Shahidi: alisema Kama Kuna Lolote ambalo hajalielewa ampigie
Mallya: Siku ya Jumapili 08 Mwezi 09 Nyumba imesachiwa na Umekuta namba ya simu ya Mkuu wa Upelelezi Chalinze, kitu gani Kilifuata baada ya hapo
Shahidi: nilimpigia Simu,yeye aliniambia kuwa alipigiwa tu simu kuwa inabidi waongozane kwenda Kusachi kwenye Nyumba ya Adamu Kasekwa
Mallya: alikufahamisha kuwa alipigiwa Simu na nani..?
Jaji: Mnasikia au Mvua inasababisha Kupoteza Usikivu tuhairishe kidogo.?
Jaji: labda nisikilize Mawakili
Mallya: Mheshimiwa Jaji naomba tubreak Kidogo kwa Sababu Shahidi akitumia Sana Nguvu anaweza kupoteza Energy na huenda akawa na siku Ndefu
Jaji: upande wa Serikali
Wakili wa Serikali: hatuna Pingamizi
Jaji: kama Mvua imeacha Kidogo, Hebu tuendelee Kidogo, Ikirudi na tukashindwa ,Tutaahirisha
Jaji: uliishia Kuhusu kumpigia simu Mkuu wa Upelelezi Chalinze
Mallya: nilimuuliza Mkuu wa Upelelezi alijibu Kitu gani
Shahidi: alisema amepigiwa simu Kutoka Moshi
Jaji: naona Mvua haitupi Muda wa kuendelea, siwezi Kukadiria kwa muda gani. Kwa muda Mchache nahairisha Shauri, Jaji anatoka Nje.
--------------------------------------------------------
Jaji amerejea Mvua Imekatika Sasa Kesi inatajwa Kesi namba 16 ya Mwaka 2021,Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire, Adam Hassan Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe
Jaji: wakili John Mallya tuendelee
Mallya: Baada ya Kuwa ameshakwambia kuwa alipigiwa simu Kutoka Moshi kitu gani kilifuata
Shahidi: Muda ulikuwa umeshaenda , nikasema itabidi Kesho yake niende kwa sababu sikuamini alichoniambia
Mallya: Kesho yake ikawaje
Jaji: Tunasikilizana, kama Mvua Inanisubiri Mimi, (Imeanza Kunyesha)
Mallya: Ulisema Ulienda Kituoni kesho yake wapi
Shahidi: Kituo cha Chalinze
Jaji: sasa ilikuwa Jumatatu
Mallya: tarehe 05 Umepigia Umemkosa, Tarehe 09 ukakuta kumesachiwa, Kitu gani kilitokea Tarehe 10 Ya Jumatatu pale Kituoni
Shahidi: Nikaomba Kuonana na Mpelelezi, Nilipo muona nikajitambulisha Kuwa Mimi ni Yule Dada ambaye Mmekuja Nyumbani Kusachi
Mallya: akakwambiaje
Shahidi: akasema kama nilivyokueleza sina ambacho nakijua zaidi ya Kuchukuliwa na kuwasindikiza Kwenda Nyumbani Kwako Kusachi,Sina ninachokijua Zaidi
Mallya: Wewe ulikuwa unafanya Jitihada gani zingine
Shahidi: nilianza kutafuta namba za Mke wa Ling'wenya
Mallya: awali ulituambia namba za Ling'wenya ulikuwa nazo na Ukampigia, za Mke wake unazitafuta, Za Ling'wenya ulitoa wapi
Shahidi: ni Mtu wa Karibu wa Mme wangu, Rafiki yake, tuseme siku wanaondoka walikuwa naye
Mallya: ulitumia Njia gani za Kupata namba za Mke wa Ling'wenya
Shahidi: nilimtafuta Mwenzao SHIKUNZI aliyekuwa anaishi nao Kimara
Jaji: Mwenzao, Kwamba alikuwa Askari Jeshi
Shahidi: Ndiyo
Mallya: alikuwa kimara anakaa na nani
Shahidi: alikuwa anakaa karibu na Ling'wenya
Mallya: kikichokufanya Umtafute SHIKUNZI ili umtafute Mke wa Ling'wenya ni nini.?
Shahidi: Nilitaka kumuuliza Mke wa Ling'wenya ili Kumuuliza huko kwake ni nini kilikuwa kinaendelea.?
Jaji: Kwanini hukumtafuta SHIKUNZI.?
Shahidi: walikuwa ni Majirani
Mallya: SHIKUNZI akafanyeje..?
Shahidi: alinipatia namba ya Mke wa Ling'wenya
Mallya: ulifanya hatua gani..?
Shahidi: nilimpigia Mke wa Ling'wenya Ilikuqa siku ya Jumatatu, na yeye akaniambia Siku ya Jumapili ambayo ni Jana yake walienda Nyumbani Kwake wakafanya Upekuzi
Mallya: nini kilifuata baada ya hapo
Shahidi: akaniambia baada ya hapo walienda Kwa Mwingine anaitwa Bwire, tumtafute Mke wa Bwire. nikamwambia wewe huko ni Jirani Mtafute Mke wa Bwire
Mallya: Kitu gani alikueleza Mke wa Ling'wenya
Shahidi: kwamba nilitaka Kujua kama kwake walienda kusachi akaniambia Wameenda kusachi, akaniambia pia tutafute Mke wa Bwire
Mallya: ulipata namba ya Mke wa Bwire na Unaweza kukumbuka Majina yao
Shahidi: Mke wa Bwire anaitwa mama Itham na Mke wa Ling'wenya anaitwa Mama Somoye
Mallya: nini Kinafuata
Shahidi: Mke wa Bwire alikuwa Dar es salaam anakasema Inabidi nitoke Chalinze nije Dar es salaam
Jaji: alisema utoke wapi.?
Shahidi: Chalinze nije Dar es salaam
Mallya: hii sintofahamu yote ilitokana na nini
Shahidi: Kutokana na kutokujua Mwenza wangu yupo wapi, namtafuta simpati alafu Nyumbani wamekuja Kusachi
Mallya: baada ya Kushauriwa Ulichukua hatua gani
Shahidi: Nilitafuta Nauli nikaja Dar es salaam
Mallya: ilikuwa lini.?
Shahidi: Sikumbuki
Mallya: Baada ya Kufika Dar es salaam nini Kilifuata
Shahidi: tulishauriana tuanze Kutafuta Vituo Vyote vya Polisi
Mallya: unaweza Kujua Nyumbani Kwake Bwire
Shahidi: Maeneo ya Temeke
Mallya: Unaweza kukumbuka mlianzia Wapi
Shahidi: Kituo cha Polisi CHANG'OMBE
Mallya: halafu
Shahidi: Tukajitambulisha kuwa sisi Waume zetu Wamekamatwa hatujui wamepelekwa Kituo gani
Mallya: mlimkuta Polisi gani
Shahidi: Polisi wa zamu
Mallya: Mkajitambulishaje..
Shahidi: Kwa Majina yetu na Waume zetu
Mallya: baada ya hapo yule Askari alifanyeje
Shahidi: akaanza kupekua Kitabu kwa kuangalia yale Majina ya waume zetu hatukuyaona
Mallya: Baada ya Kutoyaona Majina ya Mnaowatafuta Kitu gani Kilifuata
Shahidi: tulienda kituo Kingine
Mallya: Kituo gani
Shahidi: Central Police Dar es salaam
Mallya: Ikawaje
Shahidi: vile vile tukajitambukisha ya kwamba, sisi waume zetu wameletwa polisi na hatujui Kituo gani
Mallya: baada ya Kujitambulisha kwa Askari nini Kilifuata
Shahidi: aliangalia kile Kitabu hakuona yale Majina yetu
Mallya: wakati anaangalia Majina ya waume zenu Nyie Mlishiriki Vipi
Shahidi: Wakati anaangalia Kitabu, Wote tuliinama kuangalia Majina ya Waume zetu kwa usahihi
Mallya: Mmeangalia pamoja na Askari Majina ya wenza wenu hamjayaona, nini Kiliendelea baada ya hapi
Shahidi: tulitoka Kituo vha Polisi Central Police tukaenda Oysterbay, Tukajitambulisha kwa Askari wa zamu akaangalia kwenye kitabu, Majina yao, hayakwepo
Mallya: baada ya Kuwakosa Central nini kilifuata
Shahidi: tulienda Tazara
Mallya: unaweza Kueleza Kwanini Mlienda Tazara
Shahidi: tulienda kwa Sababu tulikuwa kwenye Kuendelea kuwatafuta Kituo gani cha Polisi wamepelekwa
Mallya: Unaweza Kuiambaia Mahakama mara zote mlipokuwa mnatafuta mlikuwa mnawatafuta kwa Namna gani
Shahidi: mara zote tunataja Majina na Mimi nilitaja Jina la Mme wangu Adamu Khalfani Kasekwa
Mallya: Kitu gani Kilifuata
Shahidi: Hatukuyaona Majina yao
Mallya: Mmeshaenda Vituo Vinne Kutafuta wenza wenu, hatua gani ilifuata baada ya hapo
Shahidi: Tulirudi Nyumbani kwa sababu Muda ulikuwa umeenda na tuliacha watoto wadogo
Mallya: Nyumbani kwa Maana Wapi
Shahidi: Kwa Mke wa Bwire
Mallya: kwa Mazungumzo yako na Mke wa Bwire alikwambia nini kimetokea Kule Moshi
Shahidi: akaniambia Kule Moshi kuna wifi yake ambaye ni Dada wa Mohammed Abdilah Ling'wenya
Jaji: twendeni Taratibu, Mmeshazunguka Vituo Vyote ilikuwa siku gani..?
Shahidi: Tarehe 13
Jaji: ooohhh tunakosa Mtiririko kwa sababu nilikuwa bado nipo kwenye Vituo Vya Polisi
Mallya: Samahani Mheshimiwa Jaji nilirudi Nyuma Kumuuliza kama waliongea na Mke wa Bwire
Mallya: alikwambia nini sasa
Shahidi: Kwamba Wifi yake amempigia Simu Kuwa Adam wakiwa Moshi na Mohamed, akiwa anakunywa Chai Adamu alikuwa anazungumza na Simu, ikawa kama kelele za Mvutano, Niache niache baada ya hapo wakawa wanamvuta Kumleta Sehemu za Vyakula sasa.
Mallya: Nini kilifuata
Shahidi: Kwamba alikuwa amepigwa akawa anavuja Damu
Jaji: hii ni Habari ambayo umesema Umeambiwa na Mke wa nani..?
Shahidi: Mke wa Ling'wenya Tukiwa kwa Mke wa Bwire
Mallya: huyo wifi yake anaitwa nani.?
Shahidi: anaitwa Athima
Jaji: nafikiri tulirudi kwenye Mstari hapo tunaanza kuzungumzia "Here say" yeye kaambiwa na Mke wa Ling'wenya na Mke wa Ling'wenya kaambiwa na Wifi nafikiri Mkiona Kuna Umuhimu mumwite Wifi yake aje kutoa Ushahidi ila Hatuwezi Kwenda hivyo.
Mallya: sawa Mheshimiwa Jaji
Mallya: Mliporudi Nyumbani ikawaje
Shahidi: tulikubaliana tupite Hospitalini
Mallya: Mlikuwa na Nyenzo gani katika Kuwatafuta
Shahidi: Tulikuwa na Picha zao
Mallya: Mlianzia Wapi
Shahidi: tulianzia Hospitali ya Muhimbili
Jaji: Kwanini Mlianza Kuwatafuta Kwenye Mahospitali
Shahidi: Ni baada ya Kuwakosa Kwenye Vituo vya Polisi
Jaji: Kwa Off Record tu, Moshi waliwambiaje
Shahidi: kwamba huku hawapo wameletwa Dar es salaam tukahisi labda wamepata Ajali
Mallya: Mlipofika Muhimbili ikawaje
Shahidi: Tukajitambulisha na Kueleza kuwa tunawatafuta Waume zetu, tulizunguka Kwenye wodi na Monchwari hatukuwaona
Mallya: nini Kikafuata
Shahidi: Tukaenda Hospitali ya Amana, Tukajitambulisha na Kuingia Kwenye Mawodi na Monchwari hatukuwaona pia
Mallya: baada ya Amana .?
Shahidi: tulienda Mwananyamala tukajitambulisha na Kuwatafuta waume zetu kwenye Mawodi na Mochwari hatukuwaona
Mallya: Siku ya tatu Sasa Mmeanda Muhimbili, Amana na Mwananyamala mkawakosa, Ulichukua hatua gani
Shahidi: ilibidi nirudi Chalinze kwa Sababu nauli ilikuwa imeshaaanza kuisha na Kwa sababu nina wawasiliano ikabidi nirudi Chalinze
Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani, kwa Mara ya kwanza Ulipata Taarifa ya Mume wako yupo wapi
Shahidi: Ilikuwa kwenye Taarifa Ya Habari ya Jioni
Mallya: uliwaona wakiwa wapi
Shahidi: Mahakamani Kisutu Mallya Kituo gani Cha Habari
Shahidi: ITV
Mallya: Uliwaona au Ulisimuliwa
Shahidi: niliona
Mallya: wanatuhumiwa kwa Makosa gani
Shahidi: Anashitakiwa kwa Ugaidi na uhujumu Uchumi
Mallya: mara Ya Mwisho Mme wako wakati anakuaga alikwambia anaenda Moshi Kufanya nini
Shahidi: kwamba Kuna kaz Imepatikana anaenda kuifanya
Mallya: ikawaje
Shahidi: Niliwasiliana na wenzangu
Mallya: Uliona hiyo Taarifa ya Habari ITV saa ngapi
Shahidi: Ilikuwa Saa 2 za Usiku
Mallya: mkafanya Mawasiliano, Mawasiliano gani
Shahidi: tulikubaliana Twende Mahabusu kwa Sababu hatukujua wamepelekwa Mahabusu gani
Mallya: Baada ya hapo nini kilifuata
Shahidi: Mzee Ling'wenya alikuja kutoka Mtwara
Mallya: kitu gani alifanya baada ya Kutoka Mtwara Mzee Ling'wenya
Shahidi: Tulikuwa hatuelewi wapo Mahabusu gani, Tulianza kutafuta Mahabusu waliopo
Mallya: mlianza kutafuta Mahabusu gani
Shahidi: Mimi sikwepo nilikuwa Chalinze, Tulifanya Mawasiliano
Mallya: wakakwambiaje
Shahidi: Kwamba wameenda Keko wamewakosa ila Segerea Wamewakuta wapo
Jaji: ni akina nani
Shahidi: Mke wa Mohammed Abdilah Ling'wenya na Mzee Ling'wenya
Jaji: Mke wa Ling'wenya na nani..?
Shahidi: Na Baba Mkwe wake, Mzee Ling'wenya
Mallya: sasa Ushajua Mwenza wako yupo Segerea hatua gani ilifuata
Shahidi: Nilikuja Jumapili kutoka Chalinze, Jumatatu tuliamka wote Mke wa Bwire, Ling'wenya tukaenda Wote Segerea
Mallya: Mlipofika Segerea ikawaje
Shahidi: Tulipokelewa na Askari wa Jinsia ya kike akatueleza leo siyo siku ya kuwaona Mahabusu Mje Jumamosi au Junapili
Mallya: baada hapo ulifanya Hatua gani
Shahidi: Nilienda Jumamosi
shahidi: nilisikia Ma ASKARI wakisema ndiyo Yule Jamaa ambaye yupo Kabatini
Mallya: ni nani aliteyaongea hayo
Shahidi: ni Ma Askari niliowaleza Majina kuwa namtafuta Mme wangu
Mallya: hatua gani ilifuata
Shahidi: Wakachukua funguo wakasema tunaenda kumleta
Mallya: unaweza Kutuambia hapo ulipokuwepo pana taswira gani ili Mheshimiwa jaji apate Picha
Shahidi: Ukiingia Segerea maeneo ambayo kuna Meza ya Kuwekea Chakula na Kuna Chuma kama Grill lililotenganisha
Mallya: Kitu gani kilifuata
Shahidi: nilimuona Mume wangu akitembea Kwa tabu kama Vile inaonekana ameteswa
Mallya: Unaeeza Kukumbuka Mume wako alikuwa amevaaje
Shahidi: Alikuwa amevaa kama Singlendi
Mallya: hali yake ilikuwaje
Shahidi: Amedhoofika, alikuwa amekonda Sana
Mallya: Mwendo wake ulikuwaje, alivyokuwa anatembea.?
Shahidi: alikuwa anachechemea
Mallya: Ulichukua hatua gani
Shahidi: Kama Utaratibu ulivyo wa pale, Nilibeba vitu kwa ajili yake
Jaji: ukikuwa umeleta Vitu gani
Shahidi: Chakula, shuka na Sababuni
Jaji: Vitu ulimkabidhi nani.?
Shahidi: Askari akishakagua anachukua ukiwa unamuona
Mallya: ulisema ulikuwa unamuona Mume wako anaelekea sehemu, Ni sehemu gani
Shahidi: Eneo la Nyavu ambalo mnaweza Kuzungumza
Mallya: ilikuwaje Mazungumzo kati yenu
Shahidi: Nilimuuliza Hali yake na Kilichotokea
Mallya: alikujibu nini
Shahidi: HaLi yangu ni hivyo hivyo ila siyo Nzuri
Mallya: alikwambia kwanini hali yake siyo Nzuri
Shahidi: aliniambia Kuna Mateso alipitia wakati yupo Moshi, alipigwa sana Ndiyo Maana Unaniona nipo Kwenye hali hii
Mallya: Baada ya Hapo.?
Shahidi: alichukuliwa akapelekwa Mahabusu
Mallya: nitakurudisha Nyuma Kidogo, Kilichokufanya utamtafute Vituo vya Polisi na Mahospitali Mume wako ni Kitu gani
Wakili wa Serikali: OBJECTION wakili ameshauliza
Mallya: Sikuuliza, Kama aliulizwa ni Off Records nataka sasa iingie kwenye Records
Wakili wa Serikali: Ameshaliuliza hilo swali
Jaji: Sijachoka Kuandika, Muuulize tena
Mallya: nitakurudisha Nyuma Kidogo, Kilichokufanya umtafute Vituo vya Polisi na Mahospitali Mume wako ni Kitu gani.
Shahidi: Kwa sababu tuliambiwa kuwa Walitolewa Moshi Kuja Dar es salaam na tulienda Vituo Vya Polisi Kwa Sababu tuliamini Kama wangetusaidia
Mallya: Vipi Kuhusu Ushiriki wa Ndugu zake Mwanamme
Shahidi: alikuja Mama yake, tukaenda naye Moshi
Mallya: Kwanini wewe namba ya Mume wako umesema huikumbuki kwa kichwa miye ya Mke wangu naikumbuka
Shahidi: Kwa sababu alikuwa na line Mpya aliyotoka Kuisajili
Mallya: Kwanini Unasema Ulipoenda Segerea hali yake ilikuwa tofauti
Shahidi: alikuwa amekonda sana na Macho yameingia Ndani Kama Yameganda, amekonda kwa kweli na Pia Nilimuona akiwa na alama Kwenye Mkono wakati anaenda Moshi alikuwa hana
Jaji: ulisema Uliona nini Kwenye mkono
Shahidi: alama ya Kovu kwenye Mkono, Awali alikuwa hana wakati anaenda Moshi
Mallya: ya kwangu ni hayo
Jaji: Asante sana Mallya
Jaji: pamoja na Mvua kutuharibia ratiba yetu, lakini tutabreak tena kidogo tutarejea Saa 6 Kamili, Jaji ananyanyuka anatoka.
------------------------------------------------------------------
Jaji amerejea
Shahidi anapanda tena Kzimbani
Kesi inatajwa na Washitakiwa wanakaa Kizimbani Kwao
Jaji: Wakili Nashon kama Unaswali lolote
Nashon: Sitokuwa na Swali Kwa Shahidi
Jaji: Wakili Fredrick Kihwelo kama Unaswali.?
Fredrick Kihwelo: sitokuwa na Swali kwa Niaba ya Mshitakiwa wa tatu
Jaji: Wakili Kibatala kwa niaba ya Mashtakiwa wa Nne
Kibatala: Shahidi Ulijisikiaje uliporudi Nyumbani Kukuta Nyumba yako Imevunjwa na Mume wako alikuwa hapatikani Muda wote
Shahidi: Niliogopa Kwanza Nilihisi ni wezi
Kibatala: Ulitegemea kuwa Polisi wanaweza kufanya hivyo.?
Shahidi: Hapana sikuwahi Kutegemea Polisi wanaweza Kufanya tendo hilo
Kibatala: Umeongelea kwamba Ulikuta Tv na Vingine Vipo, ila Kadi ya Pikipiki na Hati ya Kiwanja Vilikuwa Vimechukuliwa
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mpaka leo hii hujawahi kuambiwa kuwa nani anahivyo hivo vitu, Kituo cha Polisi Chalinze au afisa yoyote wa Polisi
Shahidi: Hakuna aliye wahi Kuniambia
Kibatala: Mpaka leo hii hujui nani wa Kumdai hivyo Vitu
Shahidi: Sahihi sijui nani nimdai
Kibatala: Kuna Mgogoro wowote wa Kiwanja sehemu unayoishi au Kupelekwa hata Kwa Mjumbe
Shahidi: Hapana
Kibatala: Ushawahi Kujua Kwanini Adamoo alisimamishwa kazi au Utumishi wake wa Kijeshi Ulivyokomea
Shahidi: Nafikiri huko kwenye Mambo ya Kijeshi tusiende Sana Miye sijui lolote kuhusu Jeshi
Kibatala: Sawa tuachane na hilo
Kibatala: nimesikia kuwa ulienda Kumtafuta Mumeo Vituo Vya Polisi, Naomba Nikuonyeshe Kielelezo Namba 1 Kitabu fulani Mahakama inampatia Kibatala Kielelezo DETENTION REGISTER
Kibatala: unasema ulienda Polisi ukaoneshwa Kijitabu kama hiki au Kinachofanana na Hiki na bado baada ya Kupekua hukuona Jina la Mumeo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: unasababu yoyote ya Kutunga Story ya Uongo kuwa Hukwenda Polisi Central alafu leo Uje useme ulienda Polisi Central, Je unasababu yoyote ya Kutunga.?
Shahidi: Hapana sina Sababu yoyote
Kibatala: Nimesikia Kuwa kilichowafanya Muanze Kutafuta Dar es salaam baada ya Mke wa Ling'wenya, Kuwasiliana na Dada yake Ling'wenya Kule Moshi, akasema kuwa Adamoo na Ling'wenya Wameletwa Dar es salaam, je nilikusikia Sahihi
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Nimekusikia Sahihi Kuwa Mlipita Kote ikiwemo Chang'ombe, Central Station, na Tazara pamoja na Vyumba Vya Kuhifadhia Maiti kwa sababu ya Kukosa Taarifa.?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: Mlilazimika Kufunguliwa Mwili Mmoja baada ya Mwingine Kwenye vyumba vya Kuhifadhia Maiti
Shahidi: Ndiyo Nililazimika Kufungukiwa Mahiti Moja baada ya Nyingine ilikuweza kuthibitisha kama Mume yupo huko
Kibatala: Ni sahihi Kwamba wakati unapitia hali hii ulikuwa na Miaka 25 tu.?
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: na Wakati huo ulikuwa na Mtoto Mdogo
Shahidi: Ndiyo
Kibatala: wakati huo Ulikuwa kwenye Ndoa kwa muda gani Mpaka unapitia Matukio haya Mazito
Shahidi: Mitatu
Jaji: Hesabu zenu zipo Vizuri.? kutoka 2016 August Mpaka 2020 ni Miaka Mingapi
Kibatala: Minne
Jaji: naona hakuna tatizo Mtu kukosea hesabu Mahakamani, Hilo swali tunaweza Kuliacha
Kibatala: ni Sahihi wakati nakuja kupekuliwa Ilikuwa ni Kabla ya Tarehe 09 au ni baada ya tarehe 09
Shahidi: ni baada ya Tarehe 09
Kibatala: Asante Mheshimiwa Jaji ni hayo tu
Jaji: Shahidi una nguvu za Kuendelea Kujibu?
Shahidi: Ndiyo tuendeleee
Jaji: wakili gani Serikali ataanza Kuuliza Maswali
Wakili Kidando: ataanza Jenitreza Kitali
Wakili wa Serikali: Ni sahihi Shahidi Umesema Adamu ni Mume wako
Wakili wa Serikali: Ni sahihi ujatoa Cheti Cha Ndoa
Wakili wa Serikali: Ni sahihi umesema Kuwa Adamu walikuaga wakati wanaenda Moshi Mwanzoni Mwa Mwezi wa nane
Shahidi: ni sahihi
Wakili wa Serikali: ni kweli umeeleza Kuwa walikuaga wakati wanaenda Kwa Mheshimiwa Mbowe
Shahidi: Sahihi
Wakili wa Serikali: ni kweli au Si Kweli Mume wako na Ling'wenya walikuwa marafiki sana
Shahidi: Ni kweli
Wakili wa Serikali: Mume wako pamoja na Ling'wenya waliondoka Pamoja Chalinze, Sahihi.?
Shahidi: Sahihi
Wakili wa Serikali: wakati Mume wako anajianda Kwa ajili ya Safari, Mazingira ya Nyumba yenu yakoje
Shahidi: Nyumba ya Vyumba Vinne, Kuna Sebule, Dinning na Choo
Wakili wa Serikali: Wakati Mumeo anajiandaa na Safari nitakuwa sahihi nikisema Kuwa Adamu alikuwa ndani ya Chumba wakati Mgeni akiwa Sebuleni
Shahidi: Sahihi Mgeni alikuwa sebuleni
Wakili wa Serikali: Katika Ushahidi wako Mwanzo Mpaka Mwisho ujasema ni lini walianza Safari
Shahidi: Sikusema, Sikumbuki ilikuwa tarehe ngapi
Wakili wa Serikali: nitakuwa sahihi nikisema kama ukumbuki tarehe na unachokisema siyo sahihi
Shahidi: sikumbuki tarehe lakini walianza Kusafiri pamoja Mwishoni mwa Mwezi wa Saba
Wakili wa Serikali: baada ya Adamu na Ling'wenya Kufika Moshi ulipewa taarifa kwamba Wamekamatwa.?
Shahidi: Niliambiwa
Wakili wa Serikali: aliyekwambia ni Mke wa Ling'wenya, nitakuwa sahihi kuwa Mtu aliyekwambia wamekamatwa Moshi siyo Mtu aliyekwepo wakati wanakamatwa Moshi
Shahidi: ni sahihi
Wakili wa Serikali: Naomba Nikurejeshe Nyuma, Wakati Mumeo anajianda na Safari, Ling'wenya aliakuwa sebuleni, Ni kweli Ling'wenya hakujua Vitu gani Vimewekwa Katika begi
Shahidi: ni sahihi hawezi Kujua
Wakili wa Serikali: Ni sahihi Kwamba hujaiambia Mahakama kwamba wakati Mumeao anapakia Vitu vyake alibeba Vitu hivi na hivi
Shahidi: Si kweli
Wakili wa Serikali: Ni kweli umesema Kwamba Adamu alipigwa Moshi Mpaka akatoa damu
Mallya: OBJECTION hicho anachouliza Tayari Mahakama ishatoa Malekezo kuhusu Here say
Jaji: Wakili wa Serikali
Wakili wa Serikali: labda Mahakama ituonyeshe kama Ilitoa Muongozo huo
Jaji: ngoja niseme kuwa wakati tunaanza zoezi nilisema Vitu ambavyo Shahidi anaweza asiulizwe ni Vile Vinavyotezwa Utu wake
Jaji: sasa Vingime Vyote unaweza Kuuliza na anaweza Kujibu
Wakili wa Serikali: ulisema ulisikia kuwa Adamuu amepigwa Mpaka Kutoa Damu
Shahidi: kweli
Wakili wa Serikali: Umesema Ulisema kuwa baada ya Kuwa hapatikani kwenye simu mlianza kumtafuta Vituo vya Polisi
Shahidi: Sahihi
Wakili wa Serikali: Mlianza kituo gani cha Polisi
Shahidi: Kituo cha Polisi Chang'ombe
Wakili wa Serikali: Mlipofika Kituo cha Polisi wewe na wenzako mlianza Kuomba Huyo Mtu aangaliwe kama yupo Kituoni hapo
Shahidi: Ndiyo Wakili wa Serikali: ilikuwa tarehe ngapi
Shahidi: tarehe 13 Mwezi wa 09
Jaji: Mwenzi wa Ngapi.?
Shahidi: Mwezi wa 08
Jaji: sasa niandike lipi Mwezi wa 08 au 09
Shahidi: Mwezi wa 08
Wakili wa Serikali: Utakubaliana na Mimi kuwa wakati Nyumba inasachiwa hukuwepo
Shahidi: ndiyo nimeeleza
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Maneno ya kwamba Kuna Vitu vimechukuliwa ni Maneno ya Kuambiwa
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Baada ya Kukosekana Adamu Mpaka wakati unamtafuta hukuwahi Kumtafuta Mheshimiwa Mbowe mbali na Kwamba walikwambia wanaenda Moshi kufanya kazi kwake
Shahidi: Ndiyo sikumtafuta
Wakili wa Serikali: ujaieleza mahakama kwamba Wakati Mnaenda Mochwari mlifuata Utaratibu wa kukagua
Shahidi: Nilifuata Utaratibu
Wakili wa Serikali: Lakini wakati unatoa Ushahidi Hukusema ni Taratibu zipi ulizifuata.?
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Wakati wote wa Shauri hili linaendelea Mahakamani ulipata kulifuatilia.?
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Kwa Njia gani
Shahidi : vyombo vya habari
Wakili wa Serikali: Kwa kuwa ulikuwa unafuatilia Kesi hii kwenye vyombo Vya Habari na Kwa kuwa Ushahidi uliokuwa Unaendelea Kuwa Adam Kasekwa kateswa, Ni sahihi Ulisikia
Shahidi: Nilisikia kupitia Vyombo vya Habari na Yeye pia aliniambia
Wakili wa Serikali: Ni sahihi kwamba Wakati Mumeo anaelekea Moshi alikuwa ni Mzima wa Afya na hakuwa na Majeraha
Shahidi: Ni sahihi
Wakili wa Serikali: wakati unamtembelea Segerea Uliona Makovu, Je uliyaona wapi
Shahidi: Niliona Kwenye Mikono
Wakili wa Serikali: Kwenye Mikono yote Miwili
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Wewe kama Mke wa Adamu kasekwa utakubaliana na Mimi kuwa Unaieleza Mahakama kama Adam Kasekwa aliwahi Kuwa na Makovu Mengine kabla ya wewe Kumkuta na hayo segerea
Shahidi: Ni sahihi
Wakili wa Serikali: Adamu Kasekwa alipokuwa Segerea, Mshitakiwa alimweleza kuwa amepigwa
Shahidi: Ndiyo baada ya kuona anachechemea
Wakili wa Serikali: lakini hukueleza Mahakama kama alipigwa Wapi na lini
Shahidi: Sikueleza lini
Wakili wa Serikali: Unaifahamu sana Dar es salaam
Shahidi: Kiasi Kidogo
Wakili wa Serikali: Ulisema Ulitembelea Vituo vya Tazara, Chang'ombe, Central na Oysterbay
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Hukuiambia Mahakama Sababu ya kwanini hukutembelea Vituo Vingie vidogo
Shahidi: Ni sahihi sikusema Sababu
Wakili wa Serikali: Ni sahihi ulimuona Adamu amakonda sana
Shahidi: ni Sahihi
Wakili wa sarikali: hukuieleza Mahakama kwanini alikonda
Shahidi: Ni sahihi sikueleza Sababu za Kukonda
Wakili wa serikali: naomba Niwachie wenzangu
Anasimama Wakili Robert Kidando
Wakili wa Serikali: Mpaka siku Nyumba yako inafanyiwa Upekuzi, Ni kweli ulikuwa ujui Adam yupo wapi.?
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Uwezi Kujua kama alikuwa ameridhia
Shahidi: Sijui
Wakili wa Serikali: Mpaka sasa Askari waliovaa Uniforms Ujui walikuwa ni akina nani.?
Shahidi: Sijui
Wakili wa Serikali: na Mpaka sasa wale waliovalia Kiraia hujui walikuwa wakina nani
Shahidi: Ndiyo sijui kwa sababu Sikwepo
Wakili wa Serikali: na pale Chalinze Mtaa wako Unapoishi unasema unaitwaje
Shahidi: Ramboni
Wakili wa Serikali: Na Nyumba yako bila shaka itakuwa na Grill/Geti
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: ulikuwa umelifungwa
Shahidi: hapana huwa naurudishia, Mlango ndiyo huwa nafunga
Wakili wa Serikali: Baada ya kwenda kwa Jirani yako Kuuliza alikwambia Mwenyekiti wa Mtaa alikwepo.?
Shahidi: Hapana alikwepo Mjumbe wa Nyumba 10
Wakili wa Serikali: Mpaka sasa yupo pale Chalinze
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Unasema uliambiwa Kuwa Wamechukua begi la Adamu alilotoka nalo Congo, Je lipo tofauti na Sare za Jeshi la JWTZ
Shahidi: Lipo tofauti na Mabaka Mabaka ya Tanzania
Jaji: weke Vizuri mabaka mabaka ya Nini, Isije kuwa unasema Watanzania Wanamabaka Mabaka
Mahakama Kichekooooooo
Shahidi: Mabaka Mabaka ambayo ni Maua ya Sare za JWTZ yapo tofauli na Mabaka mabaka ya lile begi
Jaji: hapo Umeweka Sawa
Wakili wa Serikali: Ni sahihi Ukumbuki tarehe ambazo waliondoka Kwenda moshi
Shahidi: Ndiyo Sikumbuki
Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Inaweza ikawa hata Mwishoni mwa Mwezi wa 07
Shahidi: Ndiyo inawezekana
Wakili wa Serikali: hujaieleza mahakama kama Mumeo aliondoka na kiasi gani cha fedha
Shahidi: Sijaeleza
Wakili wa Serikali: hujaeleza Kwamba wakati wanaenda Moshi Walitumia usafiri gani.?
Shahidi: Sijaeleza Ila walitumia Usafiri wa Basi
Wakili wa Serikali: umeeleza Polisi walichukua Kadi ya Pikipiki na Hati, ila hujasema Ni Pikipiki ya aina gani wala namba gani, Ujasema
Shahidi: Ndiyo Sijasema
Wakili wa Serikali: turudi kabla hawajaondoka Kwenda Moshi, ulisema walienda Kwanza Morogoro wakarudi
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Ila hujasema kwamba Morogoro walienda kufanya Nini.?
Shahidi: Sijasema
Wakili wa Serikali: kwa Sababu ulisema kadi ya Pikipiki ilichukuliwa, hujasema pikipiki hiyo ipo wapi
Shahidi: Sijasema
Wakili wa Serikali Tuje tarehe 05 Mwezi 08 2020 Kwamba Uliwasiliana na Adam Kasekwa kuwajulia hali wewe na Watoto, akasema subiri nitakupigia, Lakini Hakukupigia tena
Shahidi:Hakunipigia
Wakili wa Serikali: na hakukupigia
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: Ilipofika Jioni wewe Mwenyewe uliamua kumtafuta
Shahidi: Ndiyo
Wakili wa Serikali: hujasema mahakamani kwamba Kazi hiyo ya Ulinzi alikuwa ameianza
Jaji: Wakili tubreak Kidogo Kwa Saa 1
Jaji: tutaendelea Saa 8 Na Dakika 15 Kwa hiyo naharisha Shauri hili Mpaka Saa 8 na Dakika 15.
wewe unaenda lin?Mwendazake keshaenda kuzimu. Enzi zake angeshampigia simu Jaji kumwambia hapendezwi na namna na anvavyoendesha kesi hii.
Utaanza wewe ndugu yake na mwendazakewewe unaenda lin?
Badala yake wameweka shangazi kaja.Askari wetu wanatia aibu, hapo tena wameliona begi la Adamoo wakalipenda..
Wameliiba!!
Nilikutambua toka siku ya kwanza nilipokusoma humu JF, kuwa kati ya 'GTs' waliosalia JF.Samia ameishi kwenye uovu kwa miaka mitano. Ameuishi uovu kwa miaka 5. Ameufurahia uovu kwa miaka mitano. Hata akitaka kutoka, hawezi kitoka ghafla kwa 100%. Ni lazima ile roho ya uovu itaendelea kuwa ndani yake.
Hata pale anapokuwa na dhamira ya kutenda mema, kuna wakati atatumia uzoefu alio nao, ambao ni uovu.
Kwa hiyo kwenye hili kuna mkono wake na ile roho ya uovu aliyoiishi kwa miaka 5.
LOoooh, mkuu umefanya 'summary' inayohudhunisha sana!Siro na Samia walikosea sana kujitokeza hadharani na kuizungumzia hii kesi kua ushahidi upo,. Sijui walijiona akina nani kwamba watanzania na ulimwengu mzima unaweza kuhamini kauli zao, ona wanavyoumbuka
Unamkamata unaficha taarifa zake wakati ana familia, mke mtoto,wazazi kaka na eadogo zake, bado unaenda kwake unasachi bila yeye kuwepo u aondoka na hati ya nyumba pamoja na kadi ya pikipiki,. Bado mateso mliyompa, hati na kadi ya pikipiki havijulikani vilipo,
Bahati mbaya mtoto augue apoteze maisha kwa kukosa gharama za kulipia huduma, mke afariki kwa msongo wa mawazo, mwisho wa kesi adamoo aachiwe kwa kuonekana hana hatia, aisee
Akina Hamza mnawatengeneza wenyewe wakifanya tukio mnawatukana mpaka wazazi wao kua wana uzao wa hovyoo
Kama wewe ni mtoto wa mcheuko wa Mzee Aikaeli na hukuambulia urithi kutoka kwake mlaumu mamako Kwa kushangilia mshedede na kusahau kuomba urithi wako Kwa Mzee! Vinginevyo, endelea kupiga miayo na yowe but huna utakachoambulia kwani akili zako ni za urithi kutoka Kwa mamakoHuyo gaidi wanamchelewesha tu kama alifikia hatua ya kutapeli familia yake kwa kujimilikisha mali zote za urithi wampige haraka mvua 50
Siri gani watu wanatupwa angetupwa mjomba ako ungesema mambo ya siri za Nchi ni kikundi cha watu wachache wameharibu taswaira ya Taifa wacha watu wajue ikiwezekana wachukuliwe hatua..HIVI VYOMBO VYA DOLA HAVIJAGUNDUA TU KWAMBA HII KESI INAIVUA NGUO SERIKALI MBELE YA DUNIA NA KUFUNUA WAZI SIRI ZA SERIKALI NA NCHI? NAWAAMBIA HAO WATU WA KILA AINA WANAOIFUATILIA HIYO KESI WANAPATA TAARIFA MUHIMU MNO AMBAZO NI HATARI KWA NCHI KIUSALAMA. UTENDAJI WA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA UNAANIKWA WAZI. IPO SIKU TUTASHANGAA KITABU KINAANDIKWA MAMBO YA AJABU KUHUSU TANZANIA. JE, MNAWAFAHAMU VIZURI HAO WANAOHUDHURIA HAPO MAHAKAMANI? WENGINE NI KUTOKA NJE YA NCHI. HAO MAKOMANDOO WA JESHI WANAFUNUA SIRI AMBAZO HAZISTAHILI KUTOKA NJE YA JESHI LENYEWE. KWANINI SERIKALI INAKUBALI MAMBO YA SIRI ZA NCHI YAANIKWE HADHARANI?