Karibuni hapa kwa updates kutoka mahakama ya uhujumu uchumi kwenye kesi namba 16 ya ugaidi inayomuhusu mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu...
Watuhumiwa tayari wamefikishwa mahakamani, leo shahidi wa tatu upande wa utetezi ataanza kutoa ushahidi wake.
Mawakili upande wa Utetezi tayari wapo katika ukumbi wa Mahakama. Mawakili upande wa Mashtaka bado wapo Nje.
Jaji ameshaingia Sasa Mahakamani. kesi inatajwa.
Wakili wa Serikali: naomba radhi tumeingia wakati umeshaingia
Jaji: sawa
Wakili wa Serikali: Kidando Wakili wa Serikali anatambulisha wenzake
1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulimanywa Majigo
Kibatala anatambulisha Wenzake
Adv. Peter Kibatala
Adv. Jonathan Mndeme
Adv. Fredrick Kiwhelo
Adv. John Malya
Adv. Sisty Aloyce
Adv. Alex Masaba
Adv. Idd Msawanga
Adv. Gaston Garubindi
Adv. Evaresta Kisanga
Adv. Faraj Mangula
Adv. Maria Mushi
Adv. Bonifasia Mapunda
Wakili Dickson Matata: anaombewa Ruhusa Mdogo wake anafanyiwa Operesheni Hospitali ya Lugalo
Jaji: Wakili wa Serikali
Wakili wa serikali: Tumekuja kwa ajili ya kesi ndogo ambapo Shahidi wa tatu yupo tayari kuendelea Kutoa Ushahidi wake
Jaji: John Mallya
Mallya: Tunaye, na Shahidi yupo tayari kutoa Ushahidi
Jaji: anaandika Kidogo na Ukimya wa Mahakama
Jaji: Shahidi wa 3 upande wa Utetezi ambaye ameandaliwa Tafadhali anaweza Kuja
Shahidi Mdada anatokea Nyuma kabisa ya Chumba Cha Mahakama anaenda Kizimbani
Jaji: Shahidi upo Mahakamani ondoa Hofu, nitakuuliza Majina yako na Nitakuapisha, Wakili wa Utetezi atakuongoza na Mawakili wengine watakuuliza Swali na Mawakili wa Serikali watakuuliza Maswali, pia huna Haja ya Kuogopa, tupo hapa kutafuta Haki.
Jaji: Shahidi unaitwa nani
Shahidi: Lilian Kibona, Dini Mkristo Shahidi Naapa Mbele ya Mahakama hii kuwa Ushahidi nitakao toa utakuwa Ukweli na Ukweli Mtupu, Mungu ni Saidie.
Jaji: Liliani utachagua Kukaa au Kusimama, Hata Ukikaaa nitakuona.
Jaji: wakili Mallya endelea
Mallya: Shahidi Unaishi wapi
Shahidi: Chalinze Mkoa wa Pwani
Mallya: sehemu gani huko Chalinze
Shahidi: Ramboni
Jaji: ni Mtaa.?
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Unaishi na nani..?
Shahidi: Na mme wangu na Watoto ambaye kwa Sasa Mme wangu ameshikiliwa.
Jaji: ni Miongoni Mwa washitakiwa?
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Mme wako anaitwa nani?
Shahidi: Adamu Khalfani Kasekwa
Mallya: hapa nitakuwa namuita Mshitakiwa wa Pili nitakuwa namaanisha pia ni yeye
Shahidi:ndiyo
Mallya: Mmeoana lini, 05/08/2016, Ndoa Ya Kiserikali
Shahidi: Ndiyo
Mallya: Mlikuwa mnaishi wapi
Shahidi: Pale pale Chalinze
Mallya: unaweza Kukumbuka Mme wako alikuwa anafanya kazi gani wakati huo
Shahidi: Askari Jeshi la JWTZ, kikosi cha 92 Ngerengere
Mallya: alikuwa anafanya kazi gani Nyingine
Shahidi: alikuwa hana kazi Nyingine zaidi ya hiyo ya Serikali
Mallya: naruka nakuja 2020 Mme wako alikuwa anafanya kazi gani
Shahidi: alikuwa anafanya shughuli zake za Biashara
Mallya: Mwanzoni Mwa Mwezi wa Nane Mwaka 2020 unakumbuka Kilitokea Kitu gani kati yako na Mme wako
Shahidi: Mme wangu alikuwa Moshi, tulikuwa tunawasiliana naye Vizuri
Mallya: Kabla ya Kwenda Moshi mlikuwa na Hali gani kati yako na Mme wako
Shahidi: Palikuwa na Mawasiliano
Mallya: kabla hajaenda Moshi kitu gani kilitokea
Shahidi: Rafiki yake Ling'wenya waliwasiliana kuwa kuna Kazi imepatikana Moshi
Mallya: Unaweza Kukumbuka Siku na Saa ya hayo mawasiliano
Shahidi: Hapana sikumbuki
Jaji: unasema palikiwa na Mawasiliano Kati ya Mme wako na Ling'wenya .?
Shahidi: Ndiyo Kwamba Ling'wenya alimpigia Simu kuwa kuna kazi Imepatikana Moshi
Jaji: Ndiyo
Mallya: Simu zilikuwa zinapigwa kati ya Ling'wenya na Mme wako, wewe ulijuaje
Shahidi: Mimi Kama Mke wake alinishirikisha, Mimi kama Mke nilimruhusu
Mallya: Jambo gani lilifanyika, kabla ya Mme wako kwenda Moshi
Shahidi: Nakumbuka walikutana na Ling'wenya wakaenda Kwanza Morogoro, Wakarudi, Waliporudi wakajiandaa Wakaenda Moshi
Mallya: Hali ya Mme wako kiAfya Wakati anaenda Moshi hali yake ilikuwaje
Shahidi: Ilikuwa Nzuri inamruhusu kwenda Kufanya kazi
Mallya: Hali Nzuri unamaanisha nini ,Mwambie Mheshimiwa Jaji
Shahidi: haumwi na Kwamba anaweza Kwenda Moshi
Mallya: kitu gani kilifuata baada ya Kwenda Moshi
Shahidi: alinitaarifu kuwa amefika Moshi
Mallya: mlikuwa mnatumia Njia gani kufanya mazungumzo
Shahidi: kwa Njia ya Simu
Mallya: Siku ya Tarehe 05/08/2020 kitu gani kilitokea
Shahidi: alinipigia na akaongea na watoto, tulipokuwa tunaongea akasema Hebu subiri nikamsubiri
Mallya: ilikuwa Saa ngapi
Shahidi: Kama Saa Moja
Mallya: alipokwambia Subiri kidogo nitakupigia Kidogo kitu gani Kilifuata
Shahidi: Nilipoona Muda umeenda ilipofika Saa 10 ilibidi nimpigie, Simu iliita ikawa imepokelewa lakini Kila nikisema Hallo Sisikii Mtu akiongea
Mallya: Unaweza Kukumbuka namba ya Simu uliyopiga, ambayo ulipiga Ikapokelewa.?
Shahidi: Sikumbuki Kichwani lakini ipo kwenye Simu yangu
Mallya: Baadae kilifuata nini baada ya Simu kutokupokelewa
Shahidi: baadae Ikawa haipatikani
Mallya: kitu gani Kilifuata
Shahidi: kwa kuwa nilikuwa na namba ya Mwenzake Ling'wenya nikampigia Ling'wenya
Mallya: baada ya Kumpigia Ling'wenya.?
Shahidi: Ikawa inaita Mpaka jioni, Mpaka Usiku, Mpaka Kesho yake inaita haipokelewi
Mallya: Sasa wewe ulipata hisia gani baada ya kuona Inaita hadi Kesho yake haipokelewi
Shahidi: niliona labda ni Mambo ya Kazi, sikuwa na wasiwasi wowote
Mallya: Wewe ulichukua hatua gani..?
Shahidi: Sikuwa na namna yoyote zaidi ya Kusubiri simu kutoka kwao
Mallya: umesema una mtoto, anaumri gani
Shahidi: Miaka 3 na Miezi 9
Mallya: Nataka kukupeleka Tarehe 09 Mwezi 08 kitu gani Kilitokea
Shahidi: nakumbuka ilikuwa tarehe 09 mwezi 08 Mwaka 2020 niliamka Asubuhi ikiwa siku ya Jumapili, Mtoto alikuwa anasumbuliwa na tumbo
Jaji: Mtoto wa Jinsia gani
Shahidi: Wa kike
Mallya: kwanini Unakumbuka kuwa ilikuwa Siku ya Jumapili
Shahidi: Sababu ilikuwa Siku ya Ibada
Mallya: Ikawaje
Shahidi: Sikwenda Ibadani badala yake nikaenda Hospitali
Mallya: ikawaje huko Hospitali
Shahidi: Nilipokelewa
Mallya: Hospitali gani
Shahidi: Hospitali ya Serikali pale pale Chalinze
Mallya: baada ya Kupokelewa Hospitali
Shahidi: nilipatiwa Huduma nikarudi Nyumbani
Mallya: baada ya Kurudi Nyumbani
Shahidi: niliona Miguu ya watu kama Imekanyaga, Wakati natoka Nyumbani nilifunga Mlango lakini niliporudi nikakuta Milango ipo wazi
Mallya: Ule Mlango ulikuwa katika hali gani
Shahidi: Mlango ulikuwa wazi na Kitasa nikakuta kimevunjwa
Mallya: kitu gani kikatokea
Shahidi: kwa akili ya haraka haraka nilijua Wezi, Cha ajabu kila kitu nilikuta Vipo, Kitu kama Tv lakini vipo
Mallya: enheeee ikawaje
Shahidi: Nikaingia Chumbani nikakuta Nguo zimemwagwa Chini
Jaji: Za Mme wako
Shahidi: zote zimemwaga,na Mabegi yamefunguliwa
Shahidi: Kuna begi la jeshi alinunua Congo nilipokuja nikakuta halipo
Jaji: ukisema begi la jeshi alinunua Congo unamaanisha nini
Shahidi: Alinunua Congo Begi lenye Mabaka Mabaka ya Jeshi
Mallya: Kitu gani kilifuata
Shahidi: Nilienda Kuuliza Majirani zangu
Mallya: Jirani yako anaitwa nani.?
Shahidi: Judith Charles
Mallya: lengo la kwenda kwa Jirani lilikuwa nini
Shahidi: nilienda Kuuliza kama Mme wangu amekuja Nyumbani.? wamemuona.? kwamba kuna kitu huenda alikuja Kukitafuta kwa haraka haraka