PostGE2025 Maamuzi ya kuisimamisha nchi kwa hofu ya maandamano ni ishara ya udhaifu, si uongozi

PostGE2025 Maamuzi ya kuisimamisha nchi kwa hofu ya maandamano ni ishara ya udhaifu, si uongozi

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
8,355
Reaction score
20,792
Kwa siku kadhaa kumekuwa na gumzo kuhusu maandamano ya Dec 9. Watanzania wengi tulitarajia baada ya kilichotokea Oct 29, serikali ingekuja na mikakati mipya, yenye hekima na inayostahili nchi yenye utulivu kama Tanzania.

Lakini cha kushangaza mbinu zilezile zilizotumika mwishoni mwa Oktoba hadi Novemba, ndizo zinaonekana kurudi tena. Habari zinazoenea ni uwezekano wa curfew, kuzimwa kwa mawasiliano (hasa internet), na kuzuia shughuli za kawaida. Kama taifa, hili si jambo linalotia faraja. Dalili ni kughairishwa kwa mambo muhimu.

Tunajikuta kwenye wakati ambao vijana (hasa Gen-Z) wametengeneza presha kubwa ya kijamii. Na kwa bahati mbaya, kila dalili inaonyesha tunaelekea kurudia makosa yale yale makosa yanayoweza kuumiza watu na taifa.

Kwanini tunafika haku?

Tatizo kubwa linaonekana kuwa Viongozi wanadanganywa na kupewa taarifa zisizo sahihi kutoka kwa baadhi ya watu wa dola ambazo, kwa uhalisia, hazizidi 25% ya ukweli. Ukishindwa kuwa mkweli juu, wasaidizi wako nao hawawezi kuwa wakweli kwako. Hapa sababu ya nyie kudanganywa ni nyie wenyewe viongozi huko juu ni waongo sana.

#tathmini yangu fupi kuhusu maeneo yaliyokuwa na kashkash. : Ukweli kuhusu Oktoba 29

Hakukuwa na maandamano nchi nzima. Vurugu kubwa zilikuwa katika mikoa minne tu, na hata humo, ni baadhi ya maeneo:

Dar: Ubungo (ubungo, Kimara, Sinza, Mbezi Magufuli, Kibamba, Goba, Madale), Kinondoni (mazese,Tegeta, Bunju, Mbezi Shule – Africana), Ilala (buguruni, kigogo, mabibo, Gongo la Mboto, Chanika, Kinyerezi, Tabata).

Mikoa mingine mitatu nayo ilikuwa na maeneo machache yaliyoathirika.

Sasa mnajua Kupindisha ukweli hakuleti suluhu.

Nini kifanyike?

1. Wapeeni vijana kibali na ulinzi, si vizuizi. Wakiruhusiwa kuandamana kwa utaratibu na ulinzi wa kutosha, hoja zao mtakusanya kirahisi na nchi inaendelea salama. Huu ndio msingi wa demokrasia ya kisasa.

2. Jibuni hoja zao HARAKA na hadharani. Baada ya maandamano, viongozi wajitokeze wajibu hoja, waoneshe hatua, na hapo ndipo maridhiano ya kitaifa yanaweza kuanza. Hii si hoja ya kisiasa—ni hoja ya movement ya activism ya kizazi kipya...ipo hivyo world wide.

3. Kuwazuia kutatengeneza tarehe nyingine tu. Wasiporuhusiwa Desemba 9, hawatanyamaza. Watakuja tena, iwe April au mwezi mwingine. Tatizo sio tarehe, ni kusikilizwa.elewa neno KUSIKILIZWAA

4. Anzeni kuwa wakweli angalau kwa 75% viongozi mkiwa wakweli, waliopo chini yenu nao wataacha kuishi kwa uoga na kuanza kusema ukweli. Hilo peke yake linaweza kumaliza nusu ya migogoro ya nchi.

Tanzania ni yetu sote. Serikali ina wajibu wa kusimamia amani, haki, usalama na uhuru wa raia. Wananchi tuna wajibu wa kuilinda nchi yetu bila kuvuka mipaka na kwa ustaarabu.

Kukaa mezani na kusikilizana hakujawahi kumuumiza mtu—lakini hofu, mabavu na usiri vimewahi kuziumiza nchi nyingi duniani.

"Tuamue busara".
 
Eti watu wamelipwa kuandamana aisee Mimi sitaki Malipo yoyote ila nipo mstari wa mbele mpaka mtoke mtuachie taifa letu
 
Kiufupi, HATUNA viongozi kama taifa.Tuna watu wenye madaraka tu.Hili suala sio la polisi au JW etc..ni watu pale juu..wenye dhamana.
Hivi hawa watu kama wanashindwa kutatua matatizo yaliyoko wazi hivi..ILIKUWAJE WAKAFIKIA HIZO NAFASI WALIZONAZO.NI RUSHWA AU MFUMO USIOCHUJA UWEZO, BALI KUJUANA NA CONNECTION??
 
Serikali ipi? Madai cha kwanza waachie madaraka je wapo tyr? Ksha serikali ya mpito itakayoleta katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na uchaguzi urudiwe JE HAYA MADAI WAPO TYR KUYATEKELEZA HAO MAJIZI MAKUBWA MACCM.
 
Serikali ipi? Madai cha kwanza waachie madaraka je wapo tyr? Ksha serikali ya mpito itakayoleta katiba mpya, tume huru ya uchaguzi na uchaguzi urudiwe JE HAYA MADAI WAPO TYR KUYATEKELEZA HAO MAJIZI MAKUBWA MACCM.
Kuwa na serikali ya mpito sidhani mtu akishaapa ni ngumu sana kumuondoa kumwagika damu nyingi bure bora ruboreshe madhaifu yaliyopo.
 
Back
Top Bottom