Maamuzi ya kukurupuka yameigharimu stars yangu leo

Hata angekuwapo nani kipigo ni palepale, mpaka muache usimba na uyanga na muanzishe vyuo vya michezo kwa hivyo tuvumilie tu na tuombe kisago huko misri kisizidi mabao 5-0
Mkuu Misri hatuendi tena, tulishapigwa 3-0, hiyo mechi ilikuwa ni ya mzunguko wa mwisho. Nasikitika hii mechi ya mwisho tumefungwa mabao rahisi sana.
 
mi binafsi nilikaa kimya wakati watu wanapiga kelele tunataka kocha mzawa hasa waandishi wa habari, ukweli wanaojifanya wadau wa mpira hawajui kitu ukianzia na rais wa TFF nimesoma kwenye gazeti kocha anaulizwa kwanini amempanga Haji Mwinyi anasema alitaka kubalance timu ya taifa bara na visiwani naishukuru serikali ya awamu hii kujitoa kumlipa mshahara kocha wa stars kwani kodi zetu zingekuwa zinaenda bure.Tunatakiwa tuwe na mipango mirefu na mifupi hata kama kocha akija afatishe mipango inayoeleweka na sio kuanza upya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…