Maamuzi ya kukurupuka yameigharimu stars yangu leo

Maamuzi ya kukurupuka yameigharimu stars yangu leo

Penalty wanakosa ata mastaa wakubwa sembuse samatta? Kwaiyo tujadili kuhusu star sio samatta kakosa penalty
 
Hata angekuwapo nani kipigo ni palepale, mpaka muache usimba na uyanga na muanzishe vyuo vya michezo kwa hivyo tuvumilie tu na tuombe kisago visiwe vikubwa
 
Kwanza tuelewane kwamba, Taifa stars haina uwezo wa kuleta ushindani kwenye soka la ninataka kwa sasa, na hata mwakani!! Tunaweza kua tunawachezaji wazur wenyew viwango ila tumekosa mikakati.
Wachezaji hawajui majukumu yao wakiwa uwanjan, kwa mfano Leo, ni nani alikua ana jukum la kuziba nafasi ya Haji mwinyi na Juma(Leo hupanda sana labda kadi ya mapema ilimpa uoga) wanapoenda kushambilia? Kiukweli kulikua hakuna malengo, walikua wanacheza tu wakamilishe ratiba na wala tulivyokua tunaamini kua watafanya vizur!!
Kama tunataka kosonga mbele basi tuwekeze kwenye soka.la vijana...
 
Canavaro alikua captain tukala 7.
Canavaro alikua captain hata challenge hatukuchukua.

Toeni sababu zingine
 
bila unazi wala nini kama beki(syo kapteni tu).

hatukuwahi kudhalilishwa hv nyumbani mechi ya mashindano.akina drogba,etoo n.k
walikuwa wanaambulia sare tu.

2:0 shame on us
 
Hata angekuwapo nani kipigo ni palepale, mpaka muache usimba na uyanga na muanzishe vyuo vya michezo kwa hivyo tuvumilie tu na tuombe kisago huko misri kisizidi mabao 5-0


Huo usimba na uyanga unatugharimu kweli aisee
 
Ila kusema kwamba haji mwinyi alikuwa akifanya coverage n uongo huyo ndiye aliyezengua kweli Leo coz mtu anakama mechi zaid ya kumi hajaanza kwenye klabu yake Leo unakuja kumwanzisha? Huu n ujinga
Mpaka beki 3 anakuja kukava kwa beki wa kati jiulize Nyoni na Morris walikuwa wapi....
 
KwOTE="NGARUKA, post: 16400793, member: 224909"]bila unazi wala nini kama beki(syo kapteni tu).

hatukuwahi kudhalilishwa hv nyumbani mechi ya mashindano.akina drogba,etoo n.k
walikuwa wanaambulia sare tu.

2:0 shame on us[/QUOTE]
Kwa hiyo Canavaro alikua anacheza vizuri hapa home tu?
Algeria walipofunga goli 2 hapa bongo nani alikua beki au captain.
 
[/QUOTE]
Kwa hiyo Canavaro alikua anacheza vizuri hapa home tu?
Algeria walipofunga goli 2 hapa bongo nani alikua beki au captain.[/QUOTE]

Ukiacha ushabiki morali ya uchezaji imepungua sana.
tulipigwa 2 na algeria lakin mpaka dk 90 zinaisha 2;2.

jana ilikuwa 2:0 yaani 2 mzunguko+penati ya mwendokasi
 

Attachments

  • tmp-cam--1154242090.jpg
    tmp-cam--1154242090.jpg
    13.3 KB · Views: 25
kila kitu ni msingi,msingi wetu sisi ni mdomo na magazeti je vilabu vinafanya vizuri,Tff ipo vizuri wachezaji wetu wanaviwango tusidanganye hata angepangwa nani tungepoteza brazil ilipigwa saba,hakukuwa na sababu ila walizidiwa,unafikiri matokeo yale ya timu kufungana goli nane daraja la kwanza na Tff haikuwajibika stars itashinda labda mabosi wa tff wakawe mabosi wa caf tupangiwe mchekea
 
tusikae kumlaumu mwinyi tu.wale wenzetu waliiheshimu mechi huku sisi tukiwa tumeidharau hebu angalia viungo tuliowapanga ni wangapi nao walikuwa na viungo wangapi?.ndo maana walituzidi kwa kumiliki mpira na kupanga mashambulizi yao.mipira yote iliyokuwa inaenda kati ilikuwa inawakuta wao.tujifunze kuheshimu mechi tukumbuke hii mechi kwao ilikuwa ni kama fainali
 
Kila siku huwa nalia na TFF mbovu,TFF kupandisha hadhi wachezaji wabovu kwa kuwatumia marefa.Hatuna timu hapo,tena hizo goli ni chache sana.
 
Unyonge wetu kwa waarabu ndio faida yao.Labda mnaowaita wamchangani wakianza kukwea mapipa tutashinda.
 
Nyie endeleeni kuzogoa tu, ooh mara peneti ya mwendokasi! wenzenu wakija wanawabutua tu, wanasepa![emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Beki 3 ya undava na clear za uhakika ni Oscar joshua hawa akina mwinyi mara tshabalala hatutatoboa wanawaambia.

TFF kama imeshindikana tufanye CHAD STYLE basi ili tujijenge.
Siyo mnatuaminishaaaaaaaa halafu mnapigwa mzunguko tena nyumbani.
au mko bize na FIGISUFIGISU za uchaguzi wa wale jamaaa
ukiambiwa kalete mchezaj unaenda kumleta oscar joshua?!..poor timing ya mpira,control sifuri,anticipatioo zero
 
Tukate rufaa mechi irudiwe na Cannavaro arudishiwe ukapteni wake sasa maana hakuna namna.
 
Back
Top Bottom