Maamuzi ya utatu wa tai,dubu na dragon ya wajumbe vivuli wa amani/wa vita

Maamuzi ya utatu wa tai,dubu na dragon ya wajumbe vivuli wa amani/wa vita

Risen man

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
20,205
Reaction score
54,699
Naomba niwahabarishe kidogo tulichoamua na wenzetu tangu juzi ili kufikia makubaliano yatakayookoa pande zote.

Mimi nikiwa kiungo wa kati niliweza kushiriki na wenzangu kwenye kikao cha siri kilichoanzia kwenye simu mwisho tukakutana kwenye nchi moja ndogo ya ulaya.

Nikiwa kama mwakilishi wa Urusi nilipigiwa simu nyingi sana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani siku ile ya 3 ya vita akilalamika mbona tupo kimya kuhusu kinachoendelea mashariki ya kati, mimi nikamjibu wakati mnapanga mashambulizi hamkutujulisha kwanini sasa lawama?

Kwa kifupi wakati huo alihitaji kikao cha dharura kuwaleta pamoja dragon, dubu na tai ili kurejesha hali ya kawaida japo tayari kuna hasara zimeshatokea pande zote za watoto wetu.
Tulipanga siku ya kukutana lakini baada ya siku 2 tai walilalama hakuna muda wa kusubiri bora tuharakishe kikao sababu hali katika vurugu za wanetu zinatisha.

Tuliharakisha ndipo juzi tukakutana ikaamuliwa hawa watoto wameshakuwa watu wazima wote hivyo waache utoto wasije kutoana macho.
Tulikubaliana tai wamfunde kijana wao na dubu pamoja na dragon wamtulize kijana wao aliyechokozwa ili utulivu urejee

Kutokana na heshima ya tai ulimwenguni aliomba afanye igizo fulani ili kulinda heshima yake.

Kweli kikao kilienda vizuri tukampa kijana wetu taarifa akazipokea na kusema ikiwa ni hivyo kweli atakua tayari kwaajili ya vikao vingine vijavyo.

Igizo limefanyika jana usiku hivyo tunaangalia mienendo ya watoto wetu japo kuna changamoto ya tai kutoa maneno ya kutia hasira ila tunajitahidi kutuliza hali ya sintofaham.

Igizo lilikua tai atoke na msafara wa watema moto afike kwa kijana aliyechokozwa ajifanye kutema moto lakini sio moto kweli, na baada ya hapo atatoa onyo kwa kijana kwamba ukiendelea kumpiga kijana wetu tutarudi kukuvunja mgongo.

Huyu kijana wetu alipanga kumjeruhi tai kwa kua tayari kwa lolote tukamwomba atulie kwanza tuone kama tai atatii ahadi zake za kuigiza.

Kama ninavyoandika hapa, naweza kusema igizo limeenda vyema na kinachotakiwa kufanywa ni kuendelea kuwatuliza hawa vijana mpaka hali itakaporejea kuwa ya kawaida.

Ndugu zangu tai na kinda lake ni wachokozi hivyo tunajitajidi sana kwenda nao kwa hekima tusije kuleta balaa duniani!
Ni muhimu mkatambika na kuomba kwa imani zenu ili hawa watoto waache kurushiana moto sababu hata sisi tutashindwa kuvumilia mwisho tumkate tai mbawa zake.

Upande wetu (Urusi) ikiwa hali itaendelea kuwa mbaya, basi tutatoa msaada wa kuweka ulinzi kwenye anga la Iran kama vile marekani inavyofunga anga la Israel ili mashambulizi ya upande wa pili yasiwezekane.... Hatua ya pili itategemea ni hatua zipi zinazochukuliwa na upande wa NATO ambazo zitatulazimu na sisi kuchukua hatua hizohizo!

Iran ni mshirika wetu wa muhimu.

Voice of Russia
 
Back
Top Bottom