Afande ni neno lenye asili ya kituruki "efendi" likimaanisha cheo au ukubwa fulani miongoni mwa askari au watawala wa kituruki
Neno hili lililetwa Afrika Mashariki na askari wa kisudani waliokuwa sehemu ya jeshi la wajerumani, wengi wa askari hawa walikuwa wamepigana vita huko Misri ambako kwa wakati huo eneo hilo la afrika kaskazini lilikuwa chini ya utawala wa waturuki (Ottoman empire) hivyo kupelekea wao kujifunza baadhi ya maneno hayo na walipokuja Deutsche ostafrika (German East Africa) wakaanza kulitumia na sisi kuliadopt ktk majeshi yetu lkn kwa kubadilisha kidogo matamshi yake
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.