Maana halisi ya "Luxury Bus" ni nini?

Maana halisi ya "Luxury Bus" ni nini?

Hili halizingatiwi. Juzi kati baada ya kukosa magari yote sijui yalikuwa yamekodishwa kwenda wapi nimepigwa vibaya kuambiwa ni luxury nauli 33,000 Arusha Dar.
Kuingia ndani nusu nizimie basi chafu ni kama halijawahi kufanyiwa usafi, halina service yoyote..unaambiwa linaondoka saa 12 lkn linaondoka masaa matano baadae.
Nauli kila mtu kalipa tofauti..
Tupo tuliopigwa 33, wengine 25, 22 hadi.17.
Kundoka Arusha saa 2 asb kufika dar saa 5 usiku.

Osaka Express pambav zenu.
Hii nimeona mara nyingi sana ndio mana kujiuliza,nisije lalamika nikaonekana mshamba. Kweli Luxury haina AC? Ndani ofa chungwa 1 tu!!🤔 Inabidi mamlaka husika zisimamie hichi kiti vizuri mana raia wengi hawajui. Wengi wanaju ni upya wa basi
 
Hii nimeona mara nyingi sana ndio mana kujiuliza,nisije lalamika nikaonekana mshamba. Kweli Luxury haina AC? Ndani ofa chungwa 1 tu!![emoji848] Inabidi mamlaka husika zisimamie hichi kiti vizuri mana raia wengi hawajui. Wengi wanaju ni upya wa basi
Afadhali hata wewe ulipata ofa ya chungwa. Kwanza mi nisingepokea kwa uchafu ule.
Wanaoharibu ni wapiga debe..kupandisha nauli ili wao wapate cha juu. Kwenye usimamizi wa mabasi bongo bado sana.

Mimi ningeshauri luxury wawe na stand yao, semi luxury ya kwao na hayo mengine ya kwao. Ili mtu ukienda stand fulani unajua kabisa naenda kukutana na bus la aina gani.
 
Luxury zipo. Wewe sema hujawahi kuiona.
Nipo na BM hapa ni luxury ina sifa zote kasoro wifi ambayo wanazembea
Hii BM ni mtu wa pili nasikikia anaisifia,choo kipo?
 
Kwann serikali isimamie haya madaraja na kutoa muongozo kwa abiria? Wabongo wengi tunapigwa lakini hatujui pa kusemea ndio mana unaona kimya
Serikali inajali malipo yao tuu na makato likiingia na kutoka hata kile chama cha wamiliki wa magari ya abiria yule mwenyekiti wai hana time na kujali maslahi ya abiria
 
Kuna watu hawajui sifa za luxury bus, wakionjeshwa chungwa na pipi wakawekewa na muziki wa diamond basi kwao hiyo ni luxury,
Ni kweli.
Ni kwasababu mikoa wanayosafiri hakuna luxury buses.
 
Ni kweli.
Ni kwasababu mikoa wanayosafiri hakuna luxury buses.
Hahahaaa, mtu anasafiri kati ya Kongwa na Dodoma kwa mabasi yale ya kule, siku akipanda bus lenye AC tu anazunguka Kongwa nzima kutangaza amepanda luxury, na sembuse akibahatika kuwa na simu yenye android basi ni tabu, atasifia hilo bus kama lake vile
 
Back
Top Bottom