Maana halisi ya "Luxury Bus" ni nini?

Hii nimeona mara nyingi sana ndio mana kujiuliza,nisije lalamika nikaonekana mshamba. Kweli Luxury haina AC? Ndani ofa chungwa 1 tu!!🤔 Inabidi mamlaka husika zisimamie hichi kiti vizuri mana raia wengi hawajui. Wengi wanaju ni upya wa basi
 
Hii nimeona mara nyingi sana ndio mana kujiuliza,nisije lalamika nikaonekana mshamba. Kweli Luxury haina AC? Ndani ofa chungwa 1 tu!![emoji848] Inabidi mamlaka husika zisimamie hichi kiti vizuri mana raia wengi hawajui. Wengi wanaju ni upya wa basi
Afadhali hata wewe ulipata ofa ya chungwa. Kwanza mi nisingepokea kwa uchafu ule.
Wanaoharibu ni wapiga debe..kupandisha nauli ili wao wapate cha juu. Kwenye usimamizi wa mabasi bongo bado sana.

Mimi ningeshauri luxury wawe na stand yao, semi luxury ya kwao na hayo mengine ya kwao. Ili mtu ukienda stand fulani unajua kabisa naenda kukutana na bus la aina gani.
 
Luxury zipo. Wewe sema hujawahi kuiona.
Nipo na BM hapa ni luxury ina sifa zote kasoro wifi ambayo wanazembea
Hii BM ni mtu wa pili nasikikia anaisifia,choo kipo?
 
Ina Wi-Fi kweli au ndio danganya toto
Nipo kwa BM hapa VIP. WiFi hakuna. Labda kama ipo wanatubania. Kuna kipindi wanaanza ilikuwepo na wanatangaza kuwa ipo na password wanatoa
 
Kwann serikali isimamie haya madaraja na kutoa muongozo kwa abiria? Wabongo wengi tunapigwa lakini hatujui pa kusemea ndio mana unaona kimya
Serikali inajali malipo yao tuu na makato likiingia na kutoka hata kile chama cha wamiliki wa magari ya abiria yule mwenyekiti wai hana time na kujali maslahi ya abiria
 
Kuna watu hawajui sifa za luxury bus, wakionjeshwa chungwa na pipi wakawekewa na muziki wa diamond basi kwao hiyo ni luxury,
Ni kweli.
Ni kwasababu mikoa wanayosafiri hakuna luxury buses.
 
Ni kweli.
Ni kwasababu mikoa wanayosafiri hakuna luxury buses.
Hahahaaa, mtu anasafiri kati ya Kongwa na Dodoma kwa mabasi yale ya kule, siku akipanda bus lenye AC tu anazunguka Kongwa nzima kutangaza amepanda luxury, na sembuse akibahatika kuwa na simu yenye android basi ni tabu, atasifia hilo bus kama lake vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…