Maana halisi ya Rastafari

Maana halisi ya Rastafari

Ni mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana, Simba mshindi wa kabila la Judah, Most I

HaileSelassie.jpg
mkuu umeiwekea imani yako kwa mwanadamu?
 
Ninachoona Haile Selasie mnamfanya kama Mungu,halafu sidhani bila Bob Maley hi imani ingesambaa
 
one love man
:majani7: ila mjuekuna marastafari wazungu. NabangimuachekuvutaoneloveNabangimuachekuvutaoneloveNabangimuachekuvutapeaceandloveNabangimuachekuvuta

 
Rasta Bila Kuvuta Sijui Inakuaje? Akat Wana Utukuza Sana Mmea Na Bila Bob Cjui Ungeishia Wap Huo Urastafar
 
Kabla sijakujibu embu ukipata nafsi msikilize Alpha Blond-God is one,Jesus..
Luck Dube-Shembe is the way,Jah live...
Rastafari anaamini katika Umoja,amani na Upendo mpaka hapo tosha kuwa rastafari..
Pili style ya maisha pia ina-determine wewe ni rastafari(sio kuvuta bangi)
Ikiwa tunaamini katika Mungu mmoja mwenye majina tofauti wote ni wamoja basi Tupendane,tuwe Wamoja na Aman itawale maisha yetu


Ok
If so, God is 1,Jesus kuna post ya Dreadnought amejibu haile sellasie ni Bwana wa bwana simba wa Judah au mi cjaelewa
Inakuwaje hapa
 
Wanasema bila bob urasta ungekuwa wapi? Hawajui urasta ulikuwepo strong miaka mingi kabla ya kuzaliwa bob Marley. Na bob Marley Ame fanya dunia iwatambue marasta kitu ambacho sio important sana kwa marasta. Japo ni kizuri. Mnadhani kwa kuwa msingeujua urasta kutokea kwa bob Marley, ndio urasta usinge kuwepo?
Ngoja na me niseme moja basi.
Hivi bila babu zenu kuteswa na kunyimwa haki na wakoloni, hizo dini zenu sijui zingekuwa wapi.. Hhaaaa
Mila mijeledi ya waarabu, na vipigo vya wazungu..
 
kunakitu watu mnachanganya hapa na ndio kinasababisha mshndwe kuelewa utakuwaje muislam/mkristo na bado uwe rastafarai.. Rasta sio imani ni "way of life." hakuna dini inayoitwa rastafarai bali kunawatu wanaishi kirasta.

Mkuu soma vzr post
Amesema hii ni imani
 
Umejaribu kueleza kwa kiasi ila kuna mengine unatakiwa ujifunze zaidi Tunatambua uwepo wa Kristo (Messiah) kama alivyotabiriwa katika kitabu cha Nabii Isaya na tunafuata mafundisho yake ila sisi hatumsubirii arudi mara ya pili kwa sababu Alisharudi kama Ras Taffar Mackmanon- Emperor Haile Selassie The lion of Juda.

Aiseeeee
Nilikuwa cjui ndo raha ya jf
Cc Eiyer; Matola; ionlady
 
Mfano mdogo ni Mungu na Yesu, na Mtume Mohamed na Mungu,

Huwezi kwenda kwa Mungu bila kupita kwa watu hao,

Ndivyo ilivyo kwetu, Tumemchagua Haile awe kiongozi wetu atuongoze kwenda kwa Jah

Ok
Kumbe Mmemchagua nyinyi wenyewe
Sio km ametumwa na Mungu km mitume wengine
 
Ok
If so, God is 1,Jesus kuna post ya Dreadnought amejibu haile sellasie ni Bwana wa bwana simba wa Judah au mi cjaelewa
Inakuwaje hapa

Rastafarians wamemchagua King Haile Selassie kuwa kiongozi wao, ni sawa na Mohammad S.A.W kwa waislamu na yesu kwa wakristo.
 
Wanasema bila bob urasta ungekuwa wapi? Hawajui urasta ulikuwepo strong miaka mingi kabla ya kuzaliwa bob Marley. Na bob Marley Ame fanya dunia iwatambue marasta kitu ambacho sio important sana kwa marasta. Japo ni kizuri. Mnadhani kwa kuwa msingeujua urasta kutokea kwa bob Marley, ndio urasta usinge kuwepo?
Ngoja na me niseme moja basi.
Hivi bila babu zenu kuteswa na kunyimwa haki na wakoloni, hizo dini zenu sijui zingekuwa wapi.. Hhaaaa
Mila mijeledi ya waarabu, na vipigo vya wazungu..

Falme ya roma ilipofika Kushi ilikuta tayari masinagogi yapo!
 
Maana halisi ya neno RASTAFARIAN: ni imani ya mtu mweusi au mweupe inayotetea UTU wa MTU MWEUSI. MPIGANIA HAKI YA MTU MWEUSI huitwa RASTAMAN au RASTAWOMAN na kwa WATOTO wao huitwa RASTABABY.

Imani "kamili" ya Rasta ilianzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita huku kundi kubwa la waafrika waliokuwa mikononi mwa wakoloni walipoweza kuingia kwenye imani hiyo huku nchi ya JAMAICA ikiwa na wafuasi wengi. Dredy locks ni moja kati ya kitambulisho kikubwa cha Rastafarian,,lakini si kila mwenye dredy locks basi akawa Rastafarian kwani asilimia 25 ya Rastafarian hawana Dredy locks na ndipo tunapoona kwamba kufuga dredy si kuwa na imani ya Rasta bali matendo humpeleka mtu kwenye imani ya Rasta. Rastaman hupenda kujiajiri na mara nyingi hufanya shuhguli zake kwa kutumia mikono na si vifaa vya kazi na kati ya kazi za Rasta ni SANAA, wao hufanya aina zote za sanaa lakini kazi zote hizi Rasta hujiajiri na si kuajiriwa.

Moja kati ya nguzo kuu za Rastafari ni UPENDO na AMANI, Rasta hujaribu kutafuta amani popote ipatikanapo, tabia hiyo ya Rasta imewafanya Rasta kuheshimiwa popote pale waingiapo lakini baadhi ya jamii huwa tofauti na imani hii.

Imani ya Rasta chimbuko la asili ni Nimrodi binadamu wa kwanza mweusi na mtawala wa Babeli ya kale, na kutukia kwake kumechipuza kamili nyakati ambapo haki ya mtu mweusi ilipo potea na hatimaye jamii kubwa ya watu weusi kutafuta njia ya kutetea utu huo wa mtu mweusi.

GABRIEL HAIRE SELASIE aliyekuwa kiongozi wa nchi ya Ethiopia ni moja kati ya watu waliochangia kukuza imani ya Rasta ulimwenguni na ndipo jumuiya ya Rastafariani ilipoamua kumteua kuwa kiongozi wa Rastafarian ulimwenguni.

Rasta hutumia muda wa mapumziko kwa kusikiliza burudani ya nyimbo za rege walizo zitunga ambazo nyingi ya nyimbo hizo huwa za kuwapa moyo na kuwafariji watu wanyonge na wanaopuuzwa.

Rege kwangu nisehemu ya Ibada ya kweli ambapo hutumia mziki huo siku za jumamosi kama sehemu ya kuwasiliana na Mungu wangu, Hakika Mungu hunijibu tena LIVE.


Labda nipende kusema kuwa watu wengi wanafikiri kuwa Rastafari ni kuvuta Bangi na kuwa na dreads (Dreads ni muhimu).

Kuwa Rastafari nilazima uishi nakufuata yafuatayo:


Fuata sheria za Nazareti katika Bible(Rastafarian Bible).

Epuka vyakula najisi kama nguruwe, kambale n.k

Epuka intoxicants kama pombe, sigara, kahawa, coca cola na vyakula ambavyo sio natural na vyenye madhara mwilini.

Heshimu utamaduni wa Africa na kubali kuwa wanadamu wote asili yetu ni Africa na ndio Zion Yetu

MHESHIMU KING OF KINGS, THE LION OF JUDAH, ELECT OF GOD, RAS TAFARI MAKONEN, HAILE SELASSIE, THE POWER OF THE TRINITY, KING MESIAH FROM THE ROOT OF KING DAVID IN A SOLOMONIC LINEAGE.

Kuwa msafi, usimuudhi mtu, Heshimu imani za watu, usibague mtu kwa kuangalia imani, kabila wala rangi.

Jali Elimu kwa kuwa ndio msingi wa Haile kujikomboa.

Heshimu mother nature na usiharibu mazingira.

Usiue mnyama wala kumpiga bila sababu.


Heshimu dini/imani za watu wengine,

Tambua uwepo wa Yesu Kristu na Mtume Mohamed SAW (japo mafundisho yao usiyafue)

Epuka kugusa damu wala kunywa damu.

Heshimu Bendera ya Empire ya Ethipia na Rasta colour, usivae ovyo kama urembo,

Jali equality, kuwa natural na epuka vitu vya kemikali n.k

Tafari Makomein (Gabriel Haile Selassie) ni God incarnate.

Pengine hili swala la kumwabudu Haile Selassie limebaki kwa " Root Rastafarians" yaani mimi na wale walio devote maisha yao yote katika namna ya asili ya Rastafari.

Maisha yanabadilika halikadhalika mawazo na mitazamo pia.

Rastafari sasa inaonekana kuwa kama lifestyle na pengine ni jambo jema. Kuwa Rastafari kama Kebra(Rastafari Holy Book) inavyosema ni kuwa na namna ya maisha yaliyo nyofu.

Hii inatia ndani; upendo, heshima, na amani. Kwa Rastas tunasema " don't haffi dreadlocks to be rasta, a Rastaman is a conception of the heart"

Kaya ni "sakramenti" kwa maana ya kwamba inatumiwa wakati wa worshipping kwa dhumuni la ku "calm yourself" na kutafuta oneness na muumba "Jah".

Ikumbukwe kwamba, Rastafari sio organized religion lakini ni imani yenye tumaini tofauti na inabeba mafundisho mengi ya bible hasa old testament.

Hauitaji kuacha kazi, dini yako, mke wako/mume au umkane mtu fulani ili uwe rasta. Kuwa rasta ni kuishi maisha bora kama nilivyo taja hapo huu.

Mpende mzazi wako, jali utu wa mwanadamu na viumbe vingine hapo utakuwa Rastafari kwa matendo. Kuhusu ku "smoke Kaya" ni uamuzi japo wengi tunatumia.

Kuwa rastafari ni very hard, inabidi uwe makini na ukubali kupata chalenges nyingi za maisha na watu kukuhukumu kwa kukuangalia na wengine kukuona mjinga. Ila ni raha sana kwa kuwa utaishi maisha ya furaha bila kujali what they think.


BLESSINGS!

..........soma kipengele hicho kwa makini, na ndipo utajua post hii ni pumba !:loco::der:
 
The Rastafari movement is an Ethiopian-Hebrew spirituality that arose in the 1930s in Jamaica. It is sometimes described as a religion but is considered by many adherents to be a "Way of Life".
 
Back
Top Bottom