Malignant Tumor
Senior Member
- Apr 12, 2013
- 190
- 99
Kiongozi mbona unaongopa?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wala me nashangaa tu jeshi la Polisi liko wapi kuhusu ''Sakrament'' au wanaheshimu imani za watu?Kiongozi mbona unaongopa?
Ndo uhuru wa kuabudu au?Hata mimi nimesikia asubuhi kwenye BBC swahili nikashangaa hizo Imani zao kumbe wanasamini BANGI.
jogi we sakrament yako unaipatiaga wapi:majani7:nyie pambaneni na ushoga, ya bange hamyawezi kutokana na vichwa vyenu kufanana na vya wabunge wa bunge maalumu la katiba.
mmejaa dharau utadhani mnawamiliki miungu hata muwabeze wenzenu.
Maana halisi ya neno RASTAFARIAN: ni imani ya mtu mweusi au mweupe inayotetea UTU wa MTU MWEUSI. MPIGANIA HAKI YA MTU MWEUSI huitwa RASTAMAN au RASTAWOMAN na kwa WATOTO wao huitwa RASTABABY.
Imani "kamili" ya Rasta ilianzishwa zaidi ya miaka 100 iliyopita huku kundi kubwa la waafrika waliokuwa mikononi mwa wakoloni walipoweza kuingia kwenye imani hiyo huku nchi ya JAMAICA ikiwa na wafuasi wengi. Dredy locks ni moja kati ya kitambulisho kikubwa cha Rastafarian,,lakini si kila mwenye dredy locks basi akawa Rastafarian kwani asilimia 25 ya Rastafarian hawana Dredy locks na ndipo tunapoona kwamba kufuga dredy si kuwa na imani ya Rasta bali matendo humpeleka mtu kwenye imani ya Rasta. Rastaman hupenda kujiajiri na mara nyingi hufanya shuhguli zake kwa kutumia mikono na si vifaa vya kazi na kati ya kazi za Rasta ni SANAA, wao hufanya aina zote za sanaa lakini kazi zote hizi Rasta hujiajiri na si kuajiriwa.
Moja kati ya nguzo kuu za Rastafari ni UPENDO na AMANI, Rasta hujaribu kutafuta amani popote ipatikanapo, tabia hiyo ya Rasta imewafanya Rasta kuheshimiwa popote pale waingiapo lakini baadhi ya jamii huwa tofauti na imani hii.
Imani ya Rasta chimbuko la asili ni Nimrodi binadamu wa kwanza mweusi na mtawala wa Babeli ya kale, na kutukia kwake kumechipuza kamili nyakati ambapo haki ya mtu mweusi ilipo potea na hatimaye jamii kubwa ya watu weusi kutafuta njia ya kutetea utu huo wa mtu mweusi.
GABRIEL HAIRE SELASIE aliyekuwa kiongozi wa nchi ya Ethiopia ni moja kati ya watu waliochangia kukuza imani ya Rasta ulimwenguni na ndipo jumuiya ya Rastafariani ilipoamua kumteua kuwa kiongozi wa Rastafarian ulimwenguni.
Rasta hutumia muda wa mapumziko kwa kusikiliza burudani ya nyimbo za rege walizo zitunga ambazo nyingi ya nyimbo hizo huwa za kuwapa moyo na kuwafariji watu wanyonge na wanaopuuzwa.
Rege kwangu nisehemu ya Ibada ya kweli ambapo hutumia mziki huo siku za jumamosi kama sehemu ya kuwasiliana na Mungu wangu, Hakika Mungu hunijibu tena LIVE.
Labda nipende kusema kuwa watu wengi wanafikiri kuwa Rastafari ni kuvuta Bangi na kuwa na dreads (Dreads ni muhimu).
Kuwa Rastafari nilazima uishi nakufuata yafuatayo:
Fuata sheria za Nazareti katika Bible(Rastafarian Bible).
Epuka vyakula najisi kama nguruwe, kambale n.k
Epuka intoxicants kama pombe, sigara, kahawa, coca cola na vyakula ambavyo sio natural na vyenye madhara mwilini.
Heshimu utamaduni wa Africa na kubali kuwa wanadamu wote asili yetu ni Africa na ndio Zion Yetu
MHESHIMU KING OF KINGS, THE LION OF JUDAH, ELECT OF GOD, RAS TAFARI MAKONEN, HAILE SELASSIE, THE POWER OF THE TRINITY, KING MESIAH FROM THE ROOT OF KING DAVID IN A SOLOMONIC LINEAGE.
Kuwa msafi, usimuudhi mtu, Heshimu imani za watu, usibague mtu kwa kuangalia imani, kabila wala rangi.
Jali Elimu kwa kuwa ndio msingi wa Haile kujikomboa.
Heshimu mother nature na usiharibu mazingira.
Usiue mnyama wala kumpiga bila sababu.
Heshimu dini/imani za watu wengine,
Tambua uwepo wa Yesu Kristu na Mtume Mohamed SAW (japo mafundisho yao usiyafue)
Epuka kugusa damu wala kunywa damu.
Heshimu Bendera ya Empire ya Ethipia na Rasta colour, usivae ovyo kama urembo,
Jali equality, kuwa natural na epuka vitu vya kemikali n.k
Tafari Makomein (Gabriel Haile Selassie) ni God incarnate.
Pengine hili swala la kumwabudu Haile Selassie limebaki kwa " Root Rastafarians" yaani mimi na wale walio devote maisha yao yote katika namna ya asili ya Rastafari.
Maisha yanabadilika halikadhalika mawazo na mitazamo pia.
Rastafari sasa inaonekana kuwa kama lifestyle na pengine ni jambo jema. Kuwa Rastafari kama Kebra(Rastafari Holy Book) inavyosema ni kuwa na namna ya maisha yaliyo nyofu.
Hii inatia ndani; upendo, heshima, na amani. Kwa Rastas tunasema " don't haffi dreadlocks to be rasta, a Rastaman is a conception of the heart"
Kaya ni "sakramenti" kwa maana ya kwamba inatumiwa wakati wa worshipping kwa dhumuni la ku "calm yourself" na kutafuta oneness na muumba "Jah".
Ikumbukwe kwamba, Rastafari sio organized religion lakini ni imani yenye tumaini tofauti na inabeba mafundisho mengi ya bible hasa old testament.
Hauitaji kuacha kazi, dini yako, mke wako/mume au umkane mtu fulani ili uwe rasta. Kuwa rasta ni kuishi maisha bora kama nilivyo taja hapo huu.
Mpende mzazi wako, jali utu wa mwanadamu na viumbe vingine hapo utakuwa Rastafari kwa matendo. Kuhusu ku "smoke Kaya" ni uamuzi japo wengi tunatumia.
Kuwa rastafari ni very hard, inabidi uwe makini na ukubali kupata chalenges nyingi za maisha na watu kukuhukumu kwa kukuangalia na wengine kukuona mjinga. Ila ni raha sana kwa kuwa utaishi maisha ya furaha bila kujali what they think.
BLESSINGS!
je ni kweli sifa mojawapo ya rastafari lazima uvute bangi?
Nimemsikiliza vzr mwandishi wa BBC Leonard Mubali na amehudhuria ibada ya hao waabudu binadamu marasta!
Sijui nae kwa kuwa kahudhuria nae kapata sakramenti (ganja)?
Mi naona kama ni ujinga na kukosa fikra pevu out of the box! Hivi huyo Selasie nae alikuwa anakula ganja?
Hakuna cha amani wala nini jamaa wamepotea! Kova hebu peleka vijana wako pale wakakamate hawa wahuni na wakuambie hiyo mimea haramu inayoongeza idadi ya mataahira nchini wanaitoa wapi!
Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
Bangi kwetu ni sakramenti kama ilivyo kwa waamini wa dini ya ukristu,
Ni mmea unaoheshimiwa sana sana!
imani zote za miungu ni ujinga na kukosa fikra pevu, ukristo, uislam, budhism, sijui takataka zote ni ujinga!
Bangi kwetu ni sakramenti kama ilivyo kwa waamini wa dini ya ukristu,
Ni mmea unaoheshimiwa sana sana!
cc The Big Show, Boko Haram, Ritz, na wengine wote wadharauo imani za watu wengine