Maana ya baadhi ya maneno ya kiingereza

Hawa hawajuigi kuwa lugha inakua wakogo kuzamani tu
 
Lugha zote ziko hivyo na usishangae kukuta lugha rasmi (formal language) imebakia kuwa kwenye makabrasha tu haitumiwi na wazungumzaji wa kawaida wa lugha.

Hawa BAKITA mamisamiati yao mengi huwa wanabaki nayo huko kwao maana kwa kawaida huwa hayafiki huku mitaani. Mi huwa naona ni kama vile tu huwa wanapoteza muda bure!
 
Hayo maneno ya Kiingereza tunayoyatumia ni baada kuyatumia kwa muda mrefu ndio tukayazoea. Ila ya kiswahili yangepata muda nusu ya muda wa hayo ya Kiingereza tungeyazoea.

Live=mubashara.

Limepigiwa promo mpaka tumelizoea
 
Daaaaaaah!!! Yani misamiati mingine banah!!! Yani wanatunga wao wenyewe BAKITA, lakini cha kushangaza huenda hata wao wenyewe hawaitumii mitaani kama hali ya kuhimiza wengine kuweza kutumia. Utawakuta hata wao wanatumia Kiswa-English.
 
Ujinga mtupu
 
Vihamuzi ina sound kama dawa za nguvu za kiume. Tafrija mchapalo inasikika kama pati ya kupigana miti😀😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…