Maana ya mafanikio

Maana ya mafanikio

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Mafanikio ni dhana inayowachanganya wengi mno kuielewa na kuifafanua. Mara kadhaa nimekuwa nikiwauliza jamaa na marafiki ila wamekuwa wakinipa maana ambayo kwa kweli inaonesha mahitaji yao.

Kuna mtu aliniambia mtu akiwa na gari zuri, mke n.k ndiyo mafanikio lakini ukiangalia kwa undani utabaini hayo ni mahitaji yake tu.

Hali hii imenifanya kuendelea kuisaka fasiri ambayo angalau utaweza kuionjesha akili utamu wa maana lakini leo hatimaye nimebaini kuwa "Mafanikio ni huduma unayoitoa kwa wengine". Tuanzie hapo, tunaweza kuingia ndani zaidi.
Karibu.
 
Mafanikio ni utu, ubinadamu na kujali kwa kugusa maisha ya wengine wajisikie afadhali na kuepuka kuwaumiza.
 
Mafanikio kila mmoja uyatafsiri kwa upande wake
Kwa upande wangu mimi mafanikio ni hali ya kuishi maisha uliyokua unayatamani.
 
Hayo ni mahitaji yako.
Natamani yako ni mahitaji yako, ndiyo maana nyumba yako siyo lazima na mwingine aishi...n.k lakini mafanikio yako ni huduma unayotoa
Mafanikio ni utu, ubinadamu na kujali kwa kugusa maisha ya wengine wajisikie afadhali na kuepuka kuwaumiza.
Well said!.. ukifikia hatua hiyo ndipo nililoandika huduma ni sawa na ulivyoandika "kugusa maisha ya wengine"...asante sana Kaka
 
Back
Top Bottom