Maana ya neno 'kavazi'

Maana ya neno 'kavazi'

MWENDAKULIMA

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2009
Posts
951
Reaction score
355
Kwa siku mbili au tatu sasa hili neno 'kavazi' limekuwa likisemwa/kuandikwa kwenye vyombo vya habari.Nilianza kulisikia wakati wa uzinduzi wa 'kavazi' ya mwalimu Nyerere juzi na leo nimeona BBC dira ya dunia kuwa 'kavazi' imeshambuliwa huko Tunisia. Sasa nataka kujua 'kavazi' ndiyo makumbusho au ni nini hasa?
 
Kiswahili sanifu hakina neno KAVAZI, ila MAKAVAZI.

Kwa mujibu ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu ( Oxford-2010), MAKAVAZI ni mahali ambapo vitu vya kielimu hukusanywa, huchunguzwa na kuonyeshwa...

Kwa muktadha wa KAVAZI LA MWL NYERERE...waasisi wake wameona waite KAVAZI badala ya MAKAVAZI ili KUSISITIZA KWAMBA NI VITU VYA KIELIMU VINAVYOMUHUSU MWL JK NYERERE TU...

Tafakari...
 
Asante mkuu Intonjanda, ila maboresho ya 'kavazi la mwalimu Nyerere' hawajakitendea haki Kiswahili
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom