MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Siku kadhaa sasa nimeona kituo cha runinga cha Citizen TV Kenya kikipeperusha tangazo fulani la kumsifia rais wa Tanzania, kama njia moja ya kumkosha na kumpunguza hasira baada ya balozi wa Tanzania kuwalalamikia kwa wao kutumia maneno "ukaidi wa rais Magufuli" pale walipokua wanaeleza jinsi gani yeye amehamasisha Watanzania waendelee na maisha kama kawaida na kutegemea maombi kipindi hiki Corona inatesa dunia, kinyume na marais wote wa ukanda huu na duniani ambao kila mmoja alikua anatahadharisha wengine hata wakipiga lockdown kwenye mataifa yao.
Sisi Wakenya neno "ukaidi" hutumika pale mtu anakaidi na kupuuza ushauri wowote, shingo ngumu, yaani kwa kingereza tafsiri yake ni "stubborn - not to change one's attitude or position on something, especially in spite of good arguments or reasons to do so" kwa mfano, rais Magufuli alitanganza kanisani tena mbele ya vyombo vya habari kwamba yeye amekula mkate wa sakramenti bila kujali Corona maana corona itaungua kanisani.
Hivyo hapo tunasema alikaidi na kupuuza ushauri wa kitaalam na kuegemea kwenye mtazamo wa kidini, mimi binafsi ni Mkristo na ninamuelewa sana anaposema Corona itaungua kanisani, lakini hayo maneno yangetamkwa na rais Uhuru wa Kenya, yaani angetamani kuihama nchi maana angesemwa sana huku, tena zaidi ya "ukaidi wa rais Uhuru", maneno yangetumika makali sana na yenye hisia kali kali.
Sisi kwetu tunaamini urais ni taasisi, sio ofisi ya kuendeshwa kwa hisia za mtu au misingi ya kidini, maana nchi yetu hii tuna watu mamilioni ambao ni wafuasi wa dini zingine ambazo hazina habari na Yesu.
Raisi Uhuru hututangazia tuombe ila anahamasisha tahadhari tena kwa kusisitiza sana na kuongeza mikwara kwa wale watapatikana wakikiuka kanuni elekezi, ikiwemo utumiaji wa barakoa nchi yote, utakasaji wa mikono muda wote na mengine mengi.
Hivyo kwa rais kutangaza kinyume na tahadhari zinazohamasishwa na waziri wa afya, kawaida kwetu tunachukulia huo kama "ukaidi". Sasa Citizen wataendelea na hiyo misifa, lakini tatizo asilimia kubwa ya wanaoitazama ni Wakenya, wengi wanabaki kushangaa kipi kikubwa hapo na ndio maana wengi wanaeleza hisia zao kwenye Tweeter.
Kwa baadhi ya Wakenya kama mimi ambao tumewahi kuishi Tanzania, tutaelewa maana tunajua jinsi kule walivyo, yaani rais bado ana mamlaka makubwa na bado wanatumia katiba ya zamani na kumtaja rais lazima uwe makini sana, hata kwenye ulevi hauwezi kuthubutu, tumesoma habari za watu kutiwa lockup kisa tu walipiga picha kuta zenye nyufa kwenye majengo aliyozindua rais, hivyo ujasiri wa kutumia maneno kama "ukaidi wa rais" ni kitu kikubwa sana kwao.
Lakini kwa Wakenya ambao hawana habari na Tanzania na wamezoea uongozi wa kitaasisi chini ya katiba mpya, lazima washangae sana. Hivyo kwa tofauti hizi za kimtazamo, Watanzania mtuwie radhi, hilo neno "ukaidi" ni la kawaida sana huku kwetu pale unakaidi ushauri.
President Magufuli says coronavirus cannot survive in churches : The Standard