Maana ya neno "ukaidi" kwa mtazamo wa Kikenya, tunaomba Watanzania mtuwie radhi

Kha! Wakati balozi wenu mwenyewe alikwenda kulalamika kwenye kituo cha habari cha Citizen TV, wala hata haikua issue kwetu.
Balozi alitimiza tu wajibu wake.ila kwa sisi raia wala kwanza hata atujuangi hizo maneno.
Nyinyi mme mtusi rais wetu na bado mna weweseka kwa media every day.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Afu hatuna hata time na nyie....[emoji23]

am better here
 
Balozi alitimiza tu wajibu wake.ila kwa sisi raia wala kwanza hata atujuangi hizo maneno.
Nyinyi mme mtusi rais wetu na bado mna weweseka kwa media every day.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nenda kwenye jukwa lenu la siasa humu JF uone, yaani siku hiyo mlifungua uzi na kufikia jioni wachangiaji walikua wanachezea kwenye maelfu...hehehe
Sisi huku urais ni taasisi, wala huwa hatupi shida, nyie mumezoea kumtukana rais wetu, mara mnamuita mvuta bangi, teja n.k. ila kwetu hilo jambo ndogo sana maana kama ukweli anavitumia hata tukiweweseka kama nyie haitabadilisha kitu.
Rais wetu husemwa sana, ndivyo ilivyo desturi ya marais kusemwa kwenye mataifa yenye utawala wa demokrasia, ila nyie hamjazoea kitu kama hicho, mnalia sana ilhali kwanza hata hakutukanwa, kasemwa tu ni mkaidi, hilo neno nimewaletea kamusi yenu yenyewe na kuwaonyesha tafsiri yenu nyie wenyewe, inasema ni mtu anaayekinzana na ushauri, anapuuza ushauri wowote na kuenda kinyume na wengine.
Sasa rais wenu alikataa kuskliza ushauri wa waaalam na kusema Corona ikiingia kanisani itaungua, kule kwenye chimbuko la hizi dini tena ndani ya madhabahu watu wanaumwa Corona.
 
Wewe pungu two , hivi ulishawahi kuona chombo Cha habari TZ kimemuita mvuta bangi kiongozi wenu ? Usifananishe jf na vyombo vya habari lazima ukubar tatizo lugha inasumbua. Nakumbuka kipindi Cha nyuma wakenya walikuwa hawajui maana sahihi ya neno hayati , walikua wanatumia neno hayati Kama vile mtu mwenye wadhifa mkubwa serikalini, utasikia tunamuona hayati jomo Kenyatta pale anaingia bc wa Tanzania wote tupo[emoji87][emoji87][emoji87]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shubash,,hivi nyinyi nyang'au mna rais? Wakenya mnateseka sana na Tanzania,sijui ni kwa nini!!!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Standard swahili menya ni peel au husk, huwezi kumfundisha mtanzania lugha yake

Na hii google mislead ndio wanatumia chang'aa media zenu

Dude, menya kiswahili kwenye sentensi ni "kuongea kiswahili kwa ufasaha" ... inaweza kutumika hivyo pia...


Kumenya lugha ... ni kuzungumza lugha kwa ufasaha ... going to the details of understanding a language..

Kiswahili asili yake Lamu kaka.. Wacha kujiaibisha ....eti lugha ya mtanzania πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€

Si kila kitu Tanzania, Kenya tunasoma kiswahili as a compulsory lang from class 1 to form 4. ..(Kuandika Insha, Kiswahili Lugha na fasihi)...

Hata ukiskia tukionge sheng... its only that we don't care..
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Kiswahili na Kenya wapi na wapi? Eti kiswahili asili yake Lamu?

Kiswahili kina terminologies nyingi za Shona Zimbabwe kuliko hayo makabila yaliyopo Lamu, 80% ya terminologies za kiswahili ndio makabila yaliyopo Tanzania, upo hapo?

Hakuna Mkenya anayeishi kwa sasa anaweza kumfundisha mtanzania lugha yake, nah nah nah πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Swahili is an Arabic/Bantu Language... it borrows from both languages...and depending on the geographic
scattering of the different speakers over time, different dialects have risen...

But you can't claim that your dialect is the more original "kwanza kama wewe ni mtoka bara"...The only people who can lay claim are the coastal tribes... sasa Wasukuma na Wachaga ni waswahili pia??? πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Kiswahili si lugha ya Watanzani , ni lugha ya tribes za "East Coast of Africa", wengine ni borrowers
 
Mi nimekuelewa vr wakenya hua mnakiswahili kigumu sana kwa neno ukaidi Kenya ni la kawaida ila kwa huku mtu mkaidi tena kutumia kwa kiongozi sio zuri muungwana anapovuliwa nguo huchutama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nice write up, MK254 ila sidhani tatizo lilikuwa ni neno ukaidi. Huu mvutano wote na Citizen Tv ni kwasababu walimkashifu badala ya kumsifia. Huyo mzee anapenda sana kusifiwa hata pale ambapo sifa hazifai. Badala ya Ukaidi wa Magufuli wangeandika hivi; Magufuli ni jembe la kweli kwenye shughuli ya kufanikisha maambukizi zaidi ya virusi vya Corona. Hapo mzee lazima angewaalika ikulu akawazawadie tausi.
 
Tz Ina influence kubwa Sana ukanda huu... influence ya ujinga. Maxence Melo amafungwa miaka ngapi? Na ni JF tu Sio media.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…