diamond d
JF-Expert Member
- Dec 20, 2018
- 812
- 2,048
1 Wakorintho 13 (Biblia Takatifu)
¹ Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.
² Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.
³ Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.
⁴ Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
⁵ haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
⁶ haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
⁷ huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
⁸ Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.