Pre GE2025 Maanadamano yasiyoifanya Katiba Mpya kuwa ni ajenda kuu ni maandamano ya wasaka vyeo

Pre GE2025 Maanadamano yasiyoifanya Katiba Mpya kuwa ni ajenda kuu ni maandamano ya wasaka vyeo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Toka mwaka 1992 suala la katiba mpya muda hautoshi. Kisingizio Cha kuwa muda hautoshi wanaweza kukielewa mazombie.
Kila zama na zama zake, Chadema has never been serious, consistency!. Wanatishiaga nyau hivi hivi, wakikaribishwa mezani, wana fakamia, wana sahau.
P
 
Kila zama na zama zake, Chadema has never been serious, consistency!. Wanatishiaga nyau hivi hivi, wakikaribishwa mezani, wana fakamia, wana sahau.
P
Hata sielewi umemaanisha nini kwenye kila zama na zama zake. Tuchukulie cdm hawajawahi kuwa serious, nyie waandishi wa habari mna sheria kandamizi mnalia hadi leo hazijawahi kurekebishwa, je nyie mmeitwa meza ipi hadi kusahau yote? Na katiba mpya sio ya cdm, nyie wanasheria mmewahi kuidai na mmefikia wapi?
 
Duh...!. Haya...
P
 
Uchaguzi hauwezi kucheleweshwa kwasababu ni kwa mujibu wa katiba, ili uchaguzi uchaguzi ucheleweshwe lazima kufanyika minimum reforms za katiba.

Si lazima uchaguzi ufanyike 2024, hili nimelisema sana humu, Mabadiliko ya Sheria ya Uchaguzi: Je Tupige Ndege Wawili kwa Jiwe Moja kwa Uchaguzi Serikali za Mitaa/Mkuu, Ufanyike Siku Moja au Tuendeleze Mazoea? lakini linahitaji minimum reforms.

Ndicho nilicho shauri, chaguzi zote zifanywe siku moja na kusimamiwa na Tume moja huru na Shirikishi ya Uchaguzi ila inahitaji minimum reforms za katiba.

Haya tena yanatoka wapi?. What has degree za miaka 3 got to do with this?.
P

1. Mkuu hapo kwenye minimum reforms ndipo panapo ondoa u "Impossibility." Mfaransa anasema "c'est nes pas impossible."

"Tusukume yanayohitajika uchaguzi kuahirishwa ."

Haya tena yanatoka wapi?. What has degree za miaka 3 got to do with this?.
P

Mkuu hapa it was a gesture of humor tu. A joke kwenye reflection ya yale tunayoambiwa watanzania wote tusomeshwe kuhusu katiba ya zamani kwa miaka 3 kwanza, pamoja na kuwa ya Warioba ilishafikia hata hatua ya kuitwa katiba pendekezwa.

Katika mapambano hatuwezi kutupia nyuso za ndita au kutupia nyuso za mbuzi tu:

Katiba Mpya: Mapambano yako katika Hatua za Mwisho

Tuta quip, tuta crack jokes, na maisha yataendelea.

Katiba mpya ni kipaumbele.
 
1. Umoja ni nguvu, mawazo kama yako yanastahili kupigwa vita bila kuyaonea haya.

2. Kulikoni kutotafuta umoja kwenye tunayokubaliana bali utengano?

3. Maoni kama yako hayawezi kuwa msimamo wa chama chochote makini labda kama ni usanii tu.

4. Bila ya CHADEMA kuyakana hadharani mawazo kama haya, matokeo yake ni kutoeleweka chama kinataka au hakitaki nini.

5. Kwamba haifahamiki kuwa kwa adui yetu mmoja vita ya pamoja inatija gani? Madhara ya wazi ya kukosa ufahamu:

"Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama"
Umeelezea nadharia, in reality hilo haliwezekani kwa nchi yetu hii, watu wamekua wa kulalama tu kwenye social networks kwa sababu ni soft landing, majaribio ya kuandamana yote yameshindwa kisa ni uoga, kauli ya rpc mmoja pale Dodoma ilizima maandamano, uchaguzi mmoja mkuu pale mbeya ,siku ya uchaguzi walimwaga wanajeshi kwa kisingizio hewa (jeshi kuingia mitaani ni lazima bunge litoe kibali),ninaamini mapambano ya kipekee, Tanzania umoja ni zero
 
Mnafiki mkubwa. Umeambiwa Katiba mpya sio kipaumbele? Kasome Press release ya CHADEMA ya Leo. Usipende kuropoka bila kuwa na facts.

1. Mkuu kama alikuwa hajasoma hiyo press release je? Kama kumbe kipaumbele ni katiba mpya na anasema hicho hicho tatizo liko wapi? Kulikoni kuyapa ma CCM kitonga hivi?

2. Kwanini tusiwekeze kwenye madogo yanayo tuunganisha kupambana na adui yetu mkubwa kwanza, tukavaana sisi Kwa sisi tukisha malizana naye? Kulikoni hofu na insecurities hizi?

3. Kwa lugha kamw hizi tunayo nia ya kushirikiana na wadau wengine kwa dhati kweli? Au ni ujanja ujanja tu?

Jan 23/24, Maandamano yahusishe wadau wote

4. Kwa kauli ngumu hizi, nani atajumuika nasi wapi?
 
Umeelezea nadharia, in reality hilo haliwezekani kwa nchi yetu hii, watu wamekua wa kulalama tu kwenye social networks kwa sababu ni soft landing, majaribio ya kuandamana yote yameshindwa kisa ni uoga, kauli ya rpc mmoja pale Dodoma ilizima maandamano, uchaguzi mmoja mkuu pale mbeya ,siku ya uchaguzi walimwaga wanajeshi kwa kisingizio hewa (jeshi kuingia mitaani ni lazima bunge litoe kibali),ninaamini mapambano ya kipekee, Tanzania umoja ni zero

1. Positive thinking ni ufumbuzi wa mengi.

2. Majaribio ya kuandamana hayAjashindwa kwa uwoga. Bali kukosekana misimamo thabiti kwa tunayoyaamini.

3. Angalia misimamo ya watu kwenye dini zao. Wamefunzwa falsafa za dini zao vilivyo na wanaziamini. Wengine hata wakiitwa Imani kali!

4. Sisi tunazijua falsafa za vyama vyetu? Viongozi wetu wanazijua? Tunaziamini? Tunaweza vipi kupigania au hata kufia tusichokijua, kuikubali, kukithamini au kukiamini vilivyo?

5. Unapaona hapa:

Mbowe, Lissu wafundeni wafuasi Falsafa ya Chama

Matatizo na ufumbuzi wetu uko hapo.
 
Katika nchi yetu tatizo la msingi siyo sheria za uchaguzi, Tatizo la msingi ni katiba mbovu inayozaa mfumo mbovu wa uongozi na utawala, mfumo mbovu wa haki na mfumo mbovu wa uwajibikaji.

Nashangaa chama kikuu cha upinzani ambacho kinajua wazi kuwa mzizi wa fitina ni katiba mbovu, hakina interest ya kuifanya katiba mpya kuwa ndiyo KILIO KIKUU cha kuwaingiza watu barabarani, lakini chenyewe kinaweka mbele mambo ya uchaguzi as if uchaguzi ndiyo tatizo kuu.

Hii inatoa taswira gani?, inatoa Taswira kuwa viongozi wa CHADEMA wao kinachowakera zaidi hadi kupata ujasiri wa kutaka kuwaingiza watu mabarabarani ni sheria zinazowakwaza kuingia bungeni au kupata udiwani. Otherwise kama kweli wana uchungu na wananchi kwa ujumla wake kwa nini Maandamano wanayoitisha yasiwe na AJENDA KUU YA MSINGI AMBAYO NI KUDAI KATIBA MPYA?

Uchaguzi wa mwaka 2020 ulipofanyika, Magufuli akawapiga akina Mbowe na kitu kizito kichwani waliwaambia wananchi kuwa kamwe hawawezi kushiriki tena uchaguzi chini ya katiba ya sasa na tume hii ya uchaguzi. Sasa Magufuli hayupo, wanahisi wana chance ya kuingia mjengoni tena kwa hiyo wako tayari kusettle na "minimum" reforms za kuwawezesha kuingia tena mjengoni kula kodi za wananchi!.

Mimi nasema kama CHADEMA wanataka kuandamana kama chama ili watngenezewe sheria watakazozipenda za kuwawezesha kupata hivyo viti vya ubunge na ruzuku iongezeke, basi ni kheri kwao wacha waandamane, LAKINI sisi wananchi tatizo letu KUU na la MSINGI ni KATIBA MPYA!

BILA KUIFANYA KATIBA MPYA KUWA NDIYO AJENDA MAMA
ya maandamano basi haya maandamano ni JOKE yaani ni KICHEKESHO na ni muendelezo uleule tu wa wanasiasa kutaka kututumia wananchi kama ngazi ili kufikia malengo yao ya kisiasa ambayo kimsingi siasa ni ajira yao!.

Haitoshi kuchomekea vijmaneno vya hapa na pale kuhusu katiba mpya ili kulainisha mioyo ya watu, tunataka ajenda KUU iwe ni KATIBA MPYA.

Nje ya hapo, Mbowe na Wanachadema wenzako kama mnadhani uchaguzi ndiyo tatizo kuu nchini basi kaandamaneni. lakini nawajulisha tu kuwa Ajenda yenu imekaa kivyama, haijakaa kitaifa na kwa hiyo hata wanaCCM ambao wangewaunga mkono kuandamana kama ajenda yenu kuu ingekuwa ni KATIBA mpya hawataandamana kwa sababu mmeweka mbele mambo ya uchaguzi.
You are speaking for yourself - tatizo kuu la wananchi ni chakula na afya si katiba mpya. Katiba iliyopo inatosha imetuvusha mabonde na military hadi leo tuko wamoja taifa moja, si majirani zetu ni vikundi vya makabila tu. Cha kufanya wewe inoe Ilani ya CHADEMA 2025 kama kweli itawezekana aipeperushe mtu makini kama Msigwa au Lema wachana na hawa wenye matusi. Mkishashinda mtakuwa na Bunge na Rais mtaibadili Katiba kadirivmtakavyoona.
 
..Mbowe amesema Maaskofu na Mashekhe wakubwa hapa nchini walimfuata na kumsihi asitishe maandamano ya ukuta.

1. Kwanini Masheikh au Maaskofu ku override maamuzi ya chama?

2. Labda hata kwenye Maridhiano kumekuwa na uingiliwaji wa maamuzi na watu hawa hawa? Labda itabidi kupimwe tija ya interferences yao kama ni faida au liability?

3. Mwamakula, Ponda, Bagonza, Mwaipopo, Niwemugizi, au wale Masheikh ubwabwa wa kamati ya amani tusiosikilizana nao. Ni wepi waliomsihi?

4. Huu usiri na kubebana kwenye makapu hakuwezi kuwa na afya kwenye ukombozi.
 
You are speaking for yourself - tatizo kuu la wananchi ni chakula na afya si katiba mpya. Katiba iliyopo inatosha imetuvusha mabonde na military hadi leo tuko wamoja taifa moja, si majirani zetu ni vikundi vya makabila tu. Cha kufanya wewe inoe Ilani ya CHADEMA 2025 kama kweli itawezekana aipeperushe mtu makini kama Msigwa au Lema wachana na hawa wenye matusi. Mkishashinda mtakuwa na Bunge na Rais mtaibadili Katiba kadirivmtakavyoona.

Wanasema kwenye msafara was mamba na kenge huwapo kazini.
 
Kama imeonekana hii katiba ya sasa ina changamoto na zimeelezwa(hata kama na wachache wenye kujua) shida ipo wapi kuleta katiba mpya ambayo sote tutafaidika na hayo mabadiliko ya hiyo katiba mpya?

Mambo ya watu kujua katiba sijui yanatoka wapi kama ingekuwa muhimu watu wote kujua hii katiba ya sasa basi elimu hiyo ingetolewa kabla hata ya madai ya katiba mpya hajaja.

Watu wanataka katiba Kwa manufaa yao ya kisiasa and not Kwa watanzania trust me

Wanataka tume huru
Wanataka rais kushitakiwa
Wanataka serikali mseto

Yan mambo ya faida za kisiasa Tu
 
1. Mkuu hapo kwenye minimum reforms ndipo panapo ondoa u "Impossibility." Mfaransa anasema "c'est nes pas impossible."

"Tusukume yanayohitajika uchaguzi kuahirishwa ."

Mkuu hapa it was a gesture of humor tu. A joke kwenye reflection ya yale tunayoambiwa watanzania wote tusomeshwe kuhusu katiba ya zamani kwa miaka 3 kwanza, pamoja na kuwa ya Warioba ilishafikia hata hatua ya kuitwa katiba pendekezwa.

Katika mapambano hatuwezi kutupia nyuso za ndita au kutupia nyuso za mbuzi tu:

Katiba Mpya: Mapambano yako katika Hatua za Mwisho

Tuta quip, tuta crack jokes, na maisha yataendelea.

Katiba mpya ni kipaumbele.
👍👌👏🤣🆒
 
Watu wanataka katiba Kwa manufaa yao ya kisiasa and not Kwa watanzania trust me

Wanataka tume huru
Wanataka rais kushitakiwa
Wanataka serikali mseto

Yan mambo ya faida za kisiasa Tu
Hao wanasiasa kwa upande wao hayo ni mambo yenye kuwanufaisha zaidi kwao ila tatizo sie wananchi kuna wakati tunapigania masilahi ya wanasiasa zaidi kwa kuamini wanachokitaka wanasiasa ni kwa ajiri yetu.
 
Na hapo ndio tunapofeli
 
Na hapo ndio tunapofeli

Na tunaendelea kujifunza zaidi kuhusu wanasiasa.

yaani siku zote tunalilia katiba mpya hawajawahi kuitisha maandamano juu ya suala hilo. Ila leo Samia kawazidi ujanja kupitia delay tactics na kawapiga na kitu kizito kichwani kwenye mambo ya uchaguzi then hao wanakurupuka wanataka kutuingiza barabarani!.

Well kama wanataka tushiriki kiroho safi basi AJENDA KUU IWE NI KATIBA BAASI. Katiba mpya ikipatikana hayo mambo ya sheria za uchaguzi na mengineyo yatajiseti yenyewe vizuri.

By the way CHADEMA walishatuambia kuwa bila KATIBA mpya uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki, sasa iweje leo watwambie kuwa sheria za uchaguzi zikiwa nzuri basi mambo yakuwa safi?. Mambo yatakuwaje safi chini ya tume hii, chini ya jeshi hili la polisi, chini ya mahakama hizi?. hayo hayabadilishwi na hizi sheria wanazotaka zibadilishwe, hayo yanabadilishwa na katiba mpya. Ndiyo maana tunasema maandamano yahusu KATIBA mpya hapo yatakuwa na maana!
 
Back
Top Bottom