Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Ujauzito wa mwanamke hudumu kwa walau siku 280 tangu utungwe hadi siku ya kujifungua.
Ni muda mzuri unaopaswa kuchukuliwa kama sehemu ya maandalizi muhimu kwa mwanamke kabla ya kuuleta uhai mpya duniani.
Kuna mambo mengi yanayoweza kufanyika, baadhi yake ni haya-
Ni muda mzuri unaopaswa kuchukuliwa kama sehemu ya maandalizi muhimu kwa mwanamke kabla ya kuuleta uhai mpya duniani.
Kuna mambo mengi yanayoweza kufanyika, baadhi yake ni haya-
- Hudhuria kliniki za uzazi, pia pata chanjo zote muhimu zinazoshauriwa wakati wa ujauzito.
- Kutunza usafi wa via vya uzazi. Hii huwa ni changamoto kubwa kwa baadhi kutokana na kukua sana kwa tumbo. Mwanamme anaweza kuwa msaada katika kutunza usafi wa sehemu hii. Ni siha njema, pia huepusha magonjwa kama UTI, fangasi n.k
- Kutokujitenga na watu wa karibu, ni muhimu katika kuongozwa na kutiwa moyo.
- Lazima kujua mapema hospitali itayotoa msaada, mtu atakayekuongezea damu ikiwa atahitajika pamoja na kuandaa usafiri wa uhakika wa kukufikisha huko kituoni.
- Vitu kama kanga, begi la uzazi, pamba, pampasi na dela hufaa pia viandaliwe mapema.
- Pata muda wa kupumzika, kunywa maji mengi, kula mlo bora pia fanya mazoezi mepesi kila siku.