PreGE2025 Maandalizi ya Mikutano ya No Reforms No Election Kanda ya Kati yamekamilika, Moto Utawaka muda wowote kuanzia sasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kwahy hapo kila gari na mkoa wake? πŸ˜‚

Jamani tuongeze kuchangia tone tone, mambo n magumu kwenye akaunti
 
Kama mpaka leo una wasiwasi na uzalendo wa Freeman Aikaeli Mbowe, basi hata akifanya nini hautampa hiyo heshima unayozungumzia.
Tumalizane mkuu 'Fundi', Mbowe aliuvuruga mwenyewe uzalendo huo na heshima kubwa sana aliyokuwa nayo alipo kubali kuwa wakala wa Samia.
Hakuna yeyote aliye mwondolea hiyo sifa ya uzalendo. Alijiondolea mwenyewe.

Hili nalo nimemalizana nalo.
 
kwahiyo mahakamani hatuendi tena? siwatanyonga wakuu
 
Tumalizane mkuu 'Fundi', Mbowe aliuvuruga mwenyewe uzalendo huo na heshima kubwa sana aliyokuwa nayo alipo kubali kuwa wakala wa Samia.
Hakuna yeyote aliye mwondolea hiyo sifa ya uzalendo. Alijiondolea mwenyewe.

Hili nalo nimemalizana nalo.
Mlimtukana sana. Mlimvunjia na mnaendelea kumvunjia heshima. Na kila mkifanya hivyo ndio wengine tunavyozidi kumheshimu. Kwa unafik wenu mnajifanya kuwa bado anahitajika katika mpambano wenu. Hamjawahi kumheshimu na hata huyo wa sasa hamtasita kumchafua siku yake ikifika. Ndio hulka yenu.
Mchango wa Mbowe hautaondolewa na keyboard warriors kama sisi.

Amandla...
 
Mwaka 1977 wanawake 13 walikusanyika kwenye Plaza de Mayo mjini Buenos Aires wakiwa wamebeba picha za watoto wao walio amini kuwa serikali yao imewapoteza. Kila siku walikuwa wanasimama kimya katika eneo hilo huku wamebeba picha zao. Ingawa serikali iliwakamata na hata kuwaua ( iligundulika baadae kuwa walikuwa wanatupwa kutoka kwenye ndege) idadi yao ilizidi kuongezeka. Mchango wa wakina mama wa Plaza de Mayo katika kuondoa utawala wa kidikteta wa Argentina unathaminiwa sana duniani kote na ni mfano wa kuigwa.
Leo hii wazalendo wetu wanasema hatatetea haki yao ya kikatiba kwa sababu kuna askari wenye silaha ambao wanaamini wako tayari kuwapiga na kuwatupa rumande! Halafu wanawabeza wale ambao kwa miaka yote wamekuwa tayari kusimama na kuhesabiwa! Watu wa ajabu sana. Historia itawatendea haki.

Amandla...
 
Nani uyo ,au wazungumzia mwenda kuzimu?
Kiko wapi sasa na yale makelele yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…