Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,177
Vurugu na ukatili wa Vyombo vya Dola ni sehemu muhimu ya Serikali za kidikteta katika kupambana na wapinzani wao kwa kisingizio cha kulinda amani na usalama. Kuna kila dalili maandamano yaliyoandaliwa leo yatajibiwa kwa nguvu kubwa ya dola ili kutisha wananchi, maana yakiruhusiwa yatawapa “attention” kitu ambacho madikteta hudhani wao tu ndiyo wanastahili.
Hivyo basi nawashauri viongozi wa upinzani watayarishe maandamano mengine ya amani yanayowezekana nchi nzima tena kwa watu wote wazee, vijana, hata Watoto. Haihitaji nguvu na itatuma salaam nzito kwa serikali na viongozi wake. Aina hii ya maandamano haiihitaji kibali cha polisi, haiihitaji mkutano wala miji mikubwa pekee kuhusika. Ni maandamano yanayoweza fanyika nchi nzima na hata nje ya nchi kwa wakati mmoja na yanaweza fanywa hata kila wiki hata kwa mwaka.
Yatawakera watawala, watachukia, wataona gere, watatisha, watabeza lakini hawataweza kuumiza mtu. Ni maandamano ambayo hata wale walio ndani ya serikali wasiopenda udhalimu wanawezaa kushiriki bila woga wala kuhitaji ruksa. Yanaweza fanywa kanisani, msikitini, sehemu za kazi, sokoni, vituo vya mabasi, ndani ya mabasi, treni, vyuoni, mashambani, sehemu za starehe bila kubughudhi mtu isipokuwa watawala tu. Hayahitaji gharama za maandalizi, viongozi wa upinzani wanaweza kuyahutubia kidigitali.
Maandamano haya ni ya “rangi ya nguo”, ni aina ya maandamano ambayo imekuwa ikitumika dunia nzima kwa miaka mingi. Itangazwe tu na viongozi wa upinzani tarehe fulani kila anayeunga mkono hoja zifutazo avae mfano nguo nyeusi na kundelea na shughuli zako kama kawaida, iwe ni Tshirt, shati, suruali, kanzu, gauni, topu, sketi, baraghashia, baseball cap, msuli, skafu, hata leso mkononi, hata kitambaa chochote kilichochanwa toka nguo chakavu ila cheusi.
Hii inaweza pia kufanyika sehemu zile Jiwe, waziri mkuu wanapotembelea maeneo flani ya nchi kama wilaya, mikoa basi wakumbane na rangi ya nguo flani siku hiyo. Watanuna, watabeza, watatishia na wanaweza hata kuleta marufuku lakini ujumbe utakuwa unawafikia kila wananchi wanapoandamana kwa namna hii. Ni namna ya kura ya aina yake ambayo hata ikipuuzwa, kwa dhalimu na dikteta itawaumiza sana moyo (mwanzoni watazuga kutokujali). Itatoa mwanya wa kuanzisha debate ya mustakabali wa taifa letu, na pia itaonyesha ufa uliopo kati ya watawala na watawaliwa.
Maandamano haya yaendelee huku namna zingine za kudai haki zikisongeshwa kama kufungua kesi mahakamani etc. Tutafika tu.
Aluta Continua.