Brodre
JF-Expert Member
- Aug 23, 2012
- 2,585
- 1,771
Wanafunzi wa chuo cha IFM wanaandamana kuelekea kituo cha police Kigamboni kupinga maovu yanayofanywa na majambazi hapo chuoni. Ina aminika kuwa police wanajua waliofanya uhalifu huo na bado wamekaa kimya bila kuchukua hatua yoyote ile.
===============
UPDATES
===============
===============
UPDATES
===============
Wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wapo kwenye maandamano mda huu kuelekea kituo cha police Kigamboni kushinikiza jeshi la police liimarishe ulinzi katika makazi yao ya kupanga (hostels) kwani kwa sasa vitendo vya wizi wa laptops, simu za mikononi, fedha pamaja na ubakaji vimekithiri.Tukio la hivi karibuni baadhi ya wanafunzi wameibiwa mali zao pamoja na baadhi yao kubakwa/kulawiti na watu wanaodaiwa kuwa wezi.
nimefanikiwa kuongea na mwanafunzi wa ifm anasema kwa sasa wanaelekea wizara ya mambo ya ndani kuwasilisha matatizo ya ujambazi yaliyokithiri kwa wanafunzi waishio kigamboni, mbaya zaidi usiku wa kuamkia leo kuna wanafunzi wa kiume wamebakwa na kwa sasa wako muhimbili..
14/01/2013
Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wameandamana leo majira ya adhuhuri hadi kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara.
Wanafunzi hao walidai kuwam, siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu ni kuwa, siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndiyo siku wenzao wawili wakiume walipovamiwa na kulawitiwa.
Majambazi hao wamekua wakidai wapewe laptops, simu na fedha na kama mwanafunzi anakataa, humlawiti.
Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM alizungumza leo na Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo alisema, "Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo…" ndipo kamanda Kova aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane naye waende hadi Kigamboni kwenye Kituo waliporipoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.
Picha zifuatazo zimepatikana kwenye blogu ya Said Powa - Raha za Pwani.
(Bofya picha moja moja, kuzikuza kwa mwonekano mzuri zaidi).
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Ulinzi uliimarishwa nnje ya jengo la Wizara ya Mambo ya ndani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]"Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo"[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mitaa ya Posta jijini humo wakielekea kwenye kivuko cha Kigamboni ili kwenda kumuonyesha Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"]http://4.bp.blogspot.com/-f3eaqlBF-Wo/UPPXmTbb0yI/AAAAAAAAYgY/awAAboUBzd4/s1600/DSC_0063.JPG
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wakianza maandamano kuelekea Feli kwaajili ya kuvuka kwenda Kigamboni.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kova akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya kupata taarifa hizo ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja kwenda Kigamboni kufuatilia tukio hilo kwa pamoja.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mitaani Posta.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kova akishangiliwa wakati wa safari kuelekea Feli.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wakajazana kupita kiasdi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue![/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Hapa wakigoma kupungua kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Pamoja na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. Picha zote na Raha za Pwani, hii ni sehemu ya kwanza tutawaletea sehemu ya pili ya tukio hili ambalo hadi hivi sasa filamu inaendelea hapa feli na ikielekea Kigamboni.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Source: wavuti.com - wavuti