Maandamano IFM

Maandamano IFM

Brodre

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Posts
2,585
Reaction score
1,771
Wanafunzi wa chuo cha IFM wanaandamana kuelekea kituo cha police Kigamboni kupinga maovu yanayofanywa na majambazi hapo chuoni. Ina aminika kuwa police wanajua waliofanya uhalifu huo na bado wamekaa kimya bila kuchukua hatua yoyote ile.

===============
UPDATES
===============
Wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wapo kwenye maandamano mda huu kuelekea kituo cha police Kigamboni kushinikiza jeshi la police liimarishe ulinzi katika makazi yao ya kupanga (hostels) kwani kwa sasa vitendo vya wizi wa laptops, simu za mikononi, fedha pamaja na ubakaji vimekithiri.Tukio la hivi karibuni baadhi ya wanafunzi wameibiwa mali zao pamoja na baadhi yao kubakwa/kulawiti na watu wanaodaiwa kuwa wezi.

nimefanikiwa kuongea na mwanafunzi wa ifm anasema kwa sasa wanaelekea wizara ya mambo ya ndani kuwasilisha matatizo ya ujambazi yaliyokithiri kwa wanafunzi waishio kigamboni, mbaya zaidi usiku wa kuamkia leo kuna wanafunzi wa kiume wamebakwa na kwa sasa wako muhimbili..

attachment.php
attachment.php




14/01/2013


Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wameandamana leo majira ya adhuhuri hadi kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani wakiwa na madai ya kutopewa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara.

Wanafunzi hao walidai kuwam, siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu ni kuwa, siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndiyo siku wenzao wawili wakiume walipovamiwa na kulawitiwa.

Majambazi hao wamekua wakidai wapewe laptops, simu na fedha na kama mwanafunzi anakataa, humlawiti.

Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM alizungumza leo na Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo alisema, "Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo…" ndipo kamanda Kova aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane naye waende hadi Kigamboni kwenye Kituo waliporipoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.


Picha zifuatazo zimepatikana kwenye blogu ya Said Powa - Raha za Pwani.

(Bofya picha moja moja, kuzikuza kwa mwonekano mzuri zaidi).







[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Ulinzi uliimarishwa nnje ya jengo la Wizara ya Mambo ya ndani kufuatia kadhia hiyo ya wanafunzi.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kamanda wa Polisi wa Kanda maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova akimsikiliza Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane waende hadi Kigamboni kwenye Kituo walichoripoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]"Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatunaulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo"[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mitaa ya Posta jijini humo wakielekea kwenye kivuko cha Kigamboni ili kwenda kumuonyesha Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"]http://4.bp.blogspot.com/-f3eaqlBF-Wo/UPPXmTbb0yI/AAAAAAAAYgY/awAAboUBzd4/s1600/DSC_0063.JPG
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wakianza maandamano kuelekea Feli kwaajili ya kuvuka kwenda Kigamboni.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kova akitoa maelezo kwa waandishi wa habari juu ya hatua zitakazochukuuliwa baada ya kupata taarifa hizo ambapo aliwaamuru wanafunzi hao wote kwapamoja kwenda Kigamboni kufuatilia tukio hilo kwa pamoja.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mitaani Posta.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Tunaimba! Tunavuka bure Tunavuka bure kwenye Pantoni.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kova akishangiliwa wakati wa safari kuelekea Feli.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Wakajazana kupita kiasdi Kova akazuia kivuko kisiondoke hadi wapungue![/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Hapa wakigoma kupungua kazi iliyochukua zaidi ya Saa moja hadi kivuko kuendelea na kazi ya kuvusha abiria.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[TABLE="align: center"]
[TR="class: px"wysiwyg_dashes_tr""]
[TD="align: center"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Pamoja na kutakiwa kupungua hapa wengine walizidi kuendelea kuingia na kukijaza kivuko hicho. Picha zote na Raha za Pwani, hii ni sehemu ya kwanza tutawaletea sehemu ya pili ya tukio hili ambalo hadi hivi sasa filamu inaendelea hapa feli na ikielekea Kigamboni.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Source: wavuti.com - wavuti
 

Attachments

  • n1i.jpg
    n1i.jpg
    38.6 KB · Views: 1,482
  • n2.jpg
    n2.jpg
    19.7 KB · Views: 471
  • n3.jpg
    n3.jpg
    31.2 KB · Views: 452
  • n4.jpg
    n4.jpg
    48.3 KB · Views: 462
  • n5.jpg
    n5.jpg
    32.4 KB · Views: 1,492
Kwenda kituo cha polisi hadi wapande kivuko, kwa nini wasiende cha Selander Bridge?
 
Toa maelezo yakamilike mkuu yaani ulivyo post haaaaaaaa hata mtoto sio hivyo funguka basi ueleweke vizuri!😱:thumbdown::thumbdown:😱
 
ni yawanafunzi wakielekea kituo cha polisi Kigamboni kupinga maovu wanayofanyiwa na majambazi ya huko

Updates.
Sabavu ni kwamba polisi wanajua wahusika wanaovunja hostels za wanafunzi lakini wamekaa kimya na pia bad enough sa hivi majambazi wanahadi lawiti watoto wa kiume wanaokaa kigamboni ndo wanafunzi wanaenda kuomba haki ifanyike
wanaolawitiwa ni hao wanafunzi wa ifm au? mbona sijakuelewa mtoa thread
 
nimefanikiwa kuongea na mwanafunzi wa ifm anasema kwa sasa wanaelekea wizara ya mambo ya ndani kuwasilisha matatizo ya ujambazi yaliyokithiri kwa wanafunzi waishio kigamboni, mbaya zaidi usiku wa kuamkia leo kuna wanafunzi wa kiume wamebakwa na kwa sasa wako muhimbili..
 
Yaani hii nchi bila maandamano na kuzomea hakujatendeka kitu!
 
Wameshafika wizara ya mambo ya ndani pale karibu na exim tower, wanaimba nyimbo mbalimbali za malalamiko yao, niko eneo la tukio!
 
nimefanikiwa kuongea na mwanafunzi wa ifm anasema kwa sasa wanaelekea wizara ya mambo ya ndani kuwasilisha matatizo ya ujambazi yaliyokithiri kwa wanafunzi waishio kigamboni, mbaya zaidi usiku wa kuamkia leo kuna wanafunzi wa kiume wamebakwa na kwa sasa wako muhimbili..

Mh, hii ss kali!ndo imefikia huko
 
wanaolawitiwa ni hao wanafunzi wa ifm au? mbona sijakuelewa mtoa thread

baada ya hao majambazi kukosa vitu vya kuiba katika chumba cha hao wanafunzi ndio wakaamua kuwalawiti hao wanafunzi ambao walikua wako wa tatu, source: nimeongea na mwanafunzi wa hapo ifm
 
du jamani kigamboni my place ,early 2004 nikikaa huko hakukua na tabu yoyote ile sasa hivi its not a better place for the student to stay jamani,kwanza wale wenyeji wengi wamekimbizwa maeneo ya karibu sababu ya nyumba kupanda bei na wanafunzi wanazi aford tu,kupelekea wao kukaa maeneo ya mbali sana na mjini hii pia ni kero kwa wazawa wa eneo lile.swali je? wanaobakwa ni hao tu wa IFM maana pale ---- chuo kikuu cha MWALIMU NYERERE pia
 
Wanafunzi wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wapo kwenye maandamano mda huu kuelekea kituo cha police Kigamboni kushinikiza jeshi la police liimarishe ulinzi katika makazi yao ya kupanga (hostels) kwani kwa sasa vitendo vya wizi wa laptops, simu za mikononi, fedha pamaja na ubakaji vimekithiri.Tukio la hivi karibuni baadhi ya wanafunzi wameibiwa mali zao pamoja na baadhi yao kubakwa/kulawiti na watu wanaodaiwa kuwa wezi.
 
Yes,wameandamana mpaka makao makuu ya jeshi la polisi!


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Nipo hapa wizara ya afya naona wanafunzi wengi sana wakiimba na kuelekea wizarani nakwa kamanda kova.

Nilipo wahuliza tu wakasema kuwa wanafunz wanaoishi kigamboni
~ wanakuwa wakiibiwa sana
~ wanabakwa na kuingiliwa nyuma ya maumbile (kulawitiwa)
~ na sasa kuna habari mbaya sana na wanaelekea kigamboni.....
 
Kwa habari za sasa Kova amewachomolea na wamegeuza maandamano yao wanaelekea kigamboni kukinukisha huko

Naomba wanaulinzi mukaimalishe ulinzi..... mambo yanaweza kualibika soon na kuepusha misiba isiyokuwa ya lazimaa
 
Ni kama kawaida ya Polisi,taarifa zilishapelekwa lakini hakuna lolote lililofanyika...
 
Back
Top Bottom