Maandamano Makubwa Kata ya Olijoro Namba 5, Mkoani Manyara Wananchi Wafunga Barabara Kudai Maji, Polisi waingilia kati

Maandamano Makubwa Kata ya Olijoro Namba 5, Mkoani Manyara Wananchi Wafunga Barabara Kudai Maji, Polisi waingilia kati

Wananchi wa Kata ya Olijoro namba 5 Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambapo leo Agosti 26, 2024 yamefanyika maandamano makubwa ya Wananchi wakiishinikiza Serikali, Kuwapatia maji baada ya huduma hiyo kuikosa kwa muda mrefu sasa.

Wananchi na Viongozi wa Vijiji wamesema changamoto hiyo ni ya muda mrefu licha kuwepo kwa ahadi nyingi ambazo azijatakelezwa hadi sasa.

Aidha wamesema ndoo moja ya maji wanauziwa kwa shilingi 1500. Wananchi hao wamefika mbali zaidi wakidai hawajawahi kumuona mkuu wa Mkoa na Mbunge wa jimbo hilo katika kata yao.

Soma Pia: Manyara: Polisi watumia mabomu kutawanya wananchi waliozingira kituo cha Polisi wakimtaka mtuhumiwa aliyebaka na kumchinja mtoto wa miaka 6

Wamewataka viongozi wa mkoa huo wakiwemo Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kufika wajionee watu wanavyoumia kwa shida ya upatikanaji wa huduma muhimu ya maji.

BADALA YA KUWATAWANYA POLISI WANGEWAPELEKEA MAJI, NAAMINI WANGETAWANYIKA BAADA YA KUPATA MAJI.
MAGARI YA KUBEBA MAJI WANAYO ILA WAMEYATUMIA KUWEKA KEMIKALI NA KUWAMWAGIA! HAWAKUHITAJI KUOGESHWA.
 
Tenth largest economy in Africa, WTF???
 
Wananchi katika kijiji cha losinon kata ya oljoro wilayani simanjiro mkoani Manyara wamefanya maandamano ya kufunga barabara kwa zaidi ya masaa sita wakishinikiza serikali kutatua changamoto ya maji iliyopo wilayani kwa zaidi ya miaka 30, Mwenyekiti wa kijiji hicho Naini Pariti amesema kua wamekua wakiuziwa maji kwa shilingi 1500 lita moja .

Wamesema kua wanatakan mkuu wa mkoa wa Manyara afike na kuona wananchi hao wanavopata tabu na kusababisha vifo vingi vya mama na mtoto, Aidha meneja RUWASA wilayani Simanjiro mkoani Manyara Johanes Martin ametoa ahadi kwa wananchi hao ndani ya mieziu miwili kutatua changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kulaza mabomba yatakayo sambaza maji kijijini hapo.

Wananchi wameanza kuamka, just imagine miaka 30, na wabunge wanachaguliwa kila baada ya miaka 5
 
Hizi masndamano zitakuwa nyingi sana maana uvhawi wao wa mwenge unaishia nguvu!
 
Huyo bi Mkubwa anaangushwa na Makundi makubwa mawili.

1.Chawa -hawa ni wapumbavu wachache wenye ufinyu mkubwa wa akili na pengne watu wasiojitambua sana, watu hawa wanamuangusha Mama kwa sababu ya kumlevya sifa asizokuwanazo wanampa sifa ambazo zinafanya ajisahau na aoene kamalza majukumu yake kumbe uvundo tu.

2.Watenda kazi wake - Madiwani ,Wabunge ,wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, viumbe hawa wanamuangusha kwa sababu pengne hawamfikishii taarfa ya nn kinaendelea huko mikoani pamoja na changamoto mbalimbali za wananchi.
 
Anakubalije kuangushwa!! Si mseme tu ukweli.
 
Wananchi wa Kata ya Olijoro namba 5 Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara ambapo leo Agosti 26, 2024 yamefanyika maandamano makubwa ya Wananchi wakiishinikiza Serikali, Kuwapatia maji baada ya huduma hiyo kuikosa kwa muda mrefu sasa.

Wananchi na Viongozi wa Vijiji wamesema changamoto hiyo ni ya muda mrefu licha kuwepo kwa ahadi nyingi ambazo azijatakelezwa hadi sasa.

Aidha wamesema ndoo moja ya maji wanauziwa kwa shilingi 1500. Wananchi hao wamefika mbali zaidi wakidai hawajawahi kumuona mkuu wa Mkoa na Mbunge wa jimbo hilo katika kata yao.

Soma Pia: Manyara: Polisi watumia mabomu kutawanya wananchi waliozingira kituo cha Polisi wakimtaka mtuhumiwa aliyebaka na kumchinja mtoto wa miaka 6

Wamewataka viongozi wa mkoa huo wakiwemo Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya kufika wajionee watu wanavyoumia kwa shida ya upatikanaji wa huduma muhimu ya maji.

SIASA NI MCHEZO MCHAFU SANA HUO NI MPANGO UMEPANGWA, SOON MTAONA MRADI MPYA
 
Kuandamana ni haki yao ya kikatiba ili mradi hawavunji sheria. Serikali sikivu ya CCM ifanyie kazi madai yao kwa haraka.
 
Kwamba kuna uchaguzi unakuja na utafanyika kama ule wa 2020 na kama makondoo tutakuwepo?

Looh!

Hatujifunzi hata kutokea kwa wamasai?

Hii nchi itakombolewa na spirit kama hizi:

Hawa wakitaka katiba mpya leo, inatoka.

Muda wa kuweka matumaini yetu kwa wamasai tena wale wa vijijini!
 
Nchi hii kunashida Kila sehemu lakini wapuuzi utasikia wanasema mama anaupiga mwingi

Fikiria kukubali kwenda kwenye uchaguzi terms zile zile, wapi pana nafuu?

imhotep umasai ingekuwa chama, tusingejiunga?

Kwa hakika ukombozi uko huko.
 
Siyo kwa hasira hizo. Wamama watakuwa wananuka bila kuosha muda mrefu.
 
Back
Top Bottom