Maandamano makubwa ya kunusuru Hifadhi ya Ngorongoro

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Rasmi naomba kutoa kusudio langu la kuitisha maandamano makubwa ya kunusuru hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.

Nimeanza mchakato wa kuomba kibali polisi na mamlaka zingine husika ili kuitisha maandamano makubwa yatakayofanyika hivi karibuni ili kuishinikiza serikali iwaondoe binadamu wote waliomo ndani ya hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kwani ni dhahiri wakiachwa humo hifadhi hiyo itakufa. Nimefikia uamuzi huo baada ya kuona licha ya nguvu zoote ilizonazo Serikali lakini inasita kuzitumia kuwatoa hao jamaa.

Kama Serikali imeweza kuwatoa machinga waliokuwa wamezagaa kwenye miji yote nchini, kama serikali iliweza kuvunja makazi ya watu pale kimara Mbezi naamini hata hawa waliomo ndani ya hifadhi wataondolewa na hakutatokea madhara yoyote zaidi sana tutainusuru hifadhi yetu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Naomba watanzania wote wenye uzalendo na nchi hii mniunge mkono pindi nikikamlisha maandalizi yote muhimu ya maandamano hayo.
 
Kitenge na wenzie wana sura nyingi alafu uelewa hawana...issue kubwa ya so called journoz wa nchi hii uelewa sifuri kelele mingi.

Kasome kwanza alafu uje na mada yenye maana sio huu upuusi ulioandika
 
Una Ajira au unatumia siku yako kufanya, anyway Ngoja niulize swali kulingana Na level of your understanding:

"Toka J3 week iliyopita mpaka Jana J3 umeutumiaje muda wako? Do not include weekend"
Kuhusu ajira yangu haina uhusiano na kutetea maslahi mapana ya taifa langu najua ile hifadhi ikiachwa iharibiwe taifa litaingia hasara kubwa sana kuliko kuwaondoa hao waliovamia makazi ya wanyama
 
Haya, Mama Tanzania, wewe ni Mbatia nini?
 
Rasmi naomba kutoa kusudio langu la kuitisha maandamano makubwa ya kunusuru hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.

Nimeanza mchakato wa kuomba kibali polisi na mamlaka zingine husika ili kuitisha maandamano makubwa yatakayofanyika hivi karibuni ili kuishinikiza serikali iwaondoe binadamu wote waliomo ndani ya hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kwani ni dhahiri wakiachwa humo hifadhi hiyo itakufa. Nimefikia uamuzi huo baada ya kuona licha ya nguvu zoote ilizonazo Serikali lakini inasita kuzitumia kuwatoa hao jamaa.

Kama Serikali imeweza kuwatoa machinga waliokuwa wamezagaa kwenye miji yote nchini, kama serikali iliweza kuvunja makazi ya watu pale kimara Mbezi naamini hata hawa waliomo ndani ya hifadhi wataondolewa na hakutatokea madhara yoyote zaidi sana tutainusuru hifadhi yetu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Naomba watanzania wote wenye uzalendo na nchi hii mniunge mkono pindi nikikamlisha maandalizi yote muhimu ya maandamano
Unaonaje tukaandaa maandamano ya kuondoa binadamu wote nchini Tanzania, maana tunawanyima wanyama nafsi ya kujiachia
 
Umelipwa shilingi ngapi?
Hapa sio suala la kulipwa ni uzalendo tu kwa nchi yangu kwani naamini ni rahisi sana kuiharibi ngorongoro na ikafutika katika orodha ya idadi adhimu zilizoko duniani na msiweze kutengeneza nyingine. Nikuombe na ww ndugu yangu tuungane tuitetee hii hifadhi kwa manufaa ya vizazi vyetu vijavyo
 
Unaonaje tukaandaa maandamano ya kuondoa binadamu wote nchini Tanzania, maana tunawanyima wanyama nafsi ya kujiachia
Hiyo unayoleta ni mada nyingine sheria ilishatenga ngorongoro kuwa hifadhi ya wanyama na pia imetenga maeneo mengine kwa matumizi ya binadamu. Naomba uniunge mkono tunusuru hifadhi yetu.
 
Una Ajira au unatumia siku yako kufanya, anyway Ngoja niulize swali kulingana Na level of your understanding:

"Toka J3 week iliyopita mpaka Jana J3 umeutumiaje muda wako? Do not include weekend"
Yaweza kuwa unayemuuliza yupo level za juu sana yaani classified. Watch out!
 
Kuna uwezekano kuna Wafanya biashara wakubwa wanawatumia kwa kuwapa masai ng'ombe mpaka 1000 kwa masai mmoja kwa ajili ya malisho mule ndani, kama hunufaiki na ngorongoro na unatetea wale watu waendelee kuwepo basi hujui ulifanyalo.

Ni suala la muda tu, tusipowatoa sasa itafika kipindi huko mbele watatoka huku raia wakilaumu kwann haikufanyika huko nyuma au kivutio cha NGORONGORO kitakuwa ni masai tu na historia na si wanyama.
 
Hiyo unayoleta ni mada nyingine sheria ilishatenga ngorongoro kuwa hifadhi ya wanyama na pia imetenga maeneo mengine kwa matumizi ya binadamu. Naomba uniunge mkono tunusuru hifadhi yetu.
Ni mada inayounga mkono mada yako , kwani sheria si tumetunga sisi kama hiyo ilivyotungwa? Sasa ndio nauliza, unaonaje tukafanye maandamano kushinikiza kutungwa sheria ya kuwaondoa binadamu wote nchini Tanzania ili wanyama wajiachie kwa raha zao?
 
Ukiwa na mipango uanagawa kila eneo na matumizi yake hilo eneo ni KWAAJILI ya wanyama pori hao masai mimi naweza kujitolea kuwapa eneo langu hata bure
 
Rasmi naomba kutoa kusudio langu la kuitisha maandamano makubwa ya kunusuru hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.

Nimeanza mchakato wa kuomba kibali polisi na mamlaka zingine husika ili kuitisha maandamano makubwa yatakayofanyika hivi karibuni ili kuishinikiza serikali iwaondoe binadamu wote waliomo ndani ya hifadhi ya taifa ya Ngorongoro kwani ni dhahiri wakiachwa humo hifadhi hiyo itakufa. Nimefikia uamuzi huo baada ya kuona licha ya nguvu zoote ilizonazo Serikali lakini inasita kuzitumia kuwatoa hao jamaa.

Kama Serikali imeweza kuwatoa machinga waliokuwa wamezagaa kwenye miji yote nchini, kama serikali iliweza kuvunja makazi ya watu pale kimara Mbezi naamini hata hawa waliomo ndani ya hifadhi wataondolewa na hakutatokea madhara yoyote zaidi sana tutainusuru hifadhi yetu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Naomba watanzania wote wenye uzalendo na nchi hii mniunge mkono pindi nikikamlisha maandalizi yote muhimu ya maandamano hayo.
Wewe tukikutoa kwenye makazi yako utajisikiaje, au unaona raha tu likifanywa kwa wengine............kama mmechukua bahasha mjiandae kuzitapika.
 
Ukiwa na mipango uanagawa kila eneo na matumizi yake hilo eneo ni KWAAJILI ya wanyama pori hao masai mimi naweza kujitolea kuwapa eneo langu hata bure
Sawa, ndio nauliza sasa, unaonaje sisi kama Waafrika tukapanga Tanzania iwe ni eneo la wanyama pori na binadamu wote tuhamishwe hapa Tanzania, nadhani DRC wanaweza wakatupa eneo hata bure tukakaa huko, we unaonaje?
 
Unaonaje ukiandamana kwanza kusisitiza katiba mpya inayoamua kesho yako na watanzania wote.
Kwa uelewa wako unadhani kesho yangu ina mashaka? Tatizo la waathirika wa siasa wanasiasisha kila kitu. Ngorongoro inalipatia taifa letu fedha nyingi sana za kigeni kwa hiyo kuipigania hiyo ni muhimu ili isijekuharibiwa kizembe.
 
Sawa, ndio nauliza sasa, unaonaje sisi kama Waafrika tukapanga Tanzania iwe ni eneo la wanyama pori na binadamu wote tuhamishwe hapa Tanzania, nadhani DRC wanaweza wakatupa eneo hata bure tukakaa huko, we unaonaje?
Kwa hiyo wewe ni mkongo ndio maana hauna uchungu na rasilimali za Tanzania?
 
Back
Top Bottom