Maandamano sio Njia sahihi ya kupingana na huu utawala dhalimu

passioner255

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2019
Posts
6,881
Reaction score
13,096
Maandamano sio njia sahihi ya kuleta mabadiliko kwa sababu utasababisha umwagaji damu jambo ambalo ni mtaji kwa hao watu. Mfano maandamano yaliyopita hajakuleta mabadiliko bali wadhalimu wanaendelea na udhalimu wao kama mnavyoona.

Umwagaji damu kwa hao watawala dhalimu ni mtaji yani ni utoaji Kafara kwani wote hao ni watumishi wa mamlaka ya giza ndiyo maana hawaogopi kuua ndo maana sasa hivi wanasema hadharani kuwa watawaua waandamanaji na wanasema wataua zaidi ya walivyoua Mwanzo.

'Njia pekee ni Kumuomba Mungu asimamishe watu wake kwenye hizo nafasi za juu na watumike kuleta mabadiliko na kuwaangusha wadhalimu wote'.

Nina uhakika hilo linafanyika kwa sababu Mungu amesikia kilio cha watu wake waliouawa na hizi tawala dhalimu na ambao tupo hai ni suala la muda tu.
 
Kanuni ya Asilimia 3.5 (3.5% rule): Hii ni sheria au nadharia ya Sayansi ya jamii ya mtaalamu wa jamii Erica Chenoweth inayoeleza kuwa endapo asilimia 3.5 (3.5%) ya wananchi katika nchi itashiriki kikamilifu katika maandamano au kampeni za amani, harakati hizo hazijawahi kushindwa kuleta mabadiliko ya kisiasa au kupindua serikali.
 
Kanuni ya Asilimia 3.5 (3.5% rule): Hii ni sheria au nadharia inayoeleza kuwa endapo asilimia 3.5 (3.5%) ya wananchi katika nchi itashiriki kikamilifu katika maandamano au kampeni za amani, harakati hizo hazijawahi kushindwa kuleta mabadiliko ya kisiasa au kupindua serikali.
Hizo ni kwa nchi zinazowajali wananchi wake ila kwa nchi zetu hizi za kiafrika maandamano yatasababisha mauaji ya kimbari /watu wengi na hao wadhalimu wataendelea kubaki madarakani.hao hawajali wananchi wanajijali wao.
 
Maandamano sio njia sahihi ya kuleta mabadiliko kwa sababu utasababisha umwagaji damu jambo ambalo ni mtaji kwa hao watu. Mfano maandamano yaliyopita hajakuleta mabadiliko bali wadhalimu wanaendelea na udhalimu wao kama mnavyoona.

Umwagaji damu kwa hao watawala dhalimu ni mtaji yani ni utoaji Kafara kwani wote hao ni watumishi wa mamlaka ya giza ndiyo maana hawaogopi kuua ndo maana sasa hivi wanasema hadharani kuwa watawaua waandamanaji na wanasema wataua zaidi ya walivyoua Mwanzo.

'Njia pekee ni Kumuomba Mungu asimamishe watu wake kwenye hizo nafasi za juu na watumike kuleta mabadiliko na kuwaangusha wadhalimu wote'.

Nina uhakika hilo linafanyika kwa sababu Mungu amesikia kilio cha watu wake waliouawa na hizi tawala dhalimu na ambao tupo hai ni suala la muda tu.
Sawa mkuu, ila ni Wapi waliwahi kuangusha/ kuondoa utawala dhalimu na katili kwa maombi??!
 
3.5% ya watu wazima Tanzania ni kama watu milioni 2. Wakiandamana watu milioni 2 kwa wiki mbili mfululizo Dar, Dodoma, Mwanza, Arusha na Mbeya hakuna namna serikali ya CCM itaweza kukataa kufanyia kazi madai yao au serikali kubadilishwa kabisa. Issue ni kwamba watu kuandamana kwa kiwango hicho kwa sasa Tanzania ni kama ndoto.
 
Unaamini katika uwepo wa MUNGU?kama unamuamini Mungu hilo jambo linawezekana.kwa nchi kama Tanzania ambapo utawala wa kisheria haupo watu wakiandamana watauawa sana na wataendelea kubaki madarakani ila nchi zenye utawala wa kisheria maandamano yanaweza kufanya kazi.
 
Watanzania hawawezi kuandamana hata kwa siku3 mfululizo.
 
Maandamano sio njia sahihi ya kuleta mabadiliko kwa sababu utasababisha umwagaji damu jambo ambalo ni mtaji kwa hao watu. Mfano maandamano yaliyopita hajakuleta mabadiliko bali wadhalimu wanaendelea na udhalimu wao kama mnavyoona.

Umwagaji damu kwa hao watawala dhalimu ni mtaji yani ni utoaji Kafara kwani wote hao ni watumishi wa mamlaka ya giza ndiyo maana hawaogopi kuua ndo maana sasa hivi wanasema hadharani kuwa watawaua waandamanaji na wanasema wataua zaidi ya walivyoua Mwanzo.

'Njia pekee ni Kumuomba Mungu asimamishe watu wake kwenye hizo nafasi za juu na watumike kuleta mabadiliko na kuwaangusha wadhalimu wote'.

Nina uhakika hilo linafanyika kwa sababu Mungu amesikia kilio cha watu wake waliouawa na hizi tawala dhalimu na ambao tupo hai ni suala la muda tu.
Achana na issue za MUNGU katika mapambano. Pendekeza njia nyingine siyo maombi. Acha hiyo kitu. Kama maandamano hayawezi, basi maombi ndiyo ubatili kabisa.
Pendekeza another alternative.
 
Unaamini katika uwepo wa MUNGU?kama unamuamini Mungu hilo jambo linawezekana.kwa nchi kama Tanzania ambapo utawala wa kisheria haupo watu wakiandamana watauawa sana na wataendelea kubaki madarakani ila nchi zenye utawala wa kisheria maandamano yanaweza kufanya kazi.
Mungu hata kama yupo hasaidii kwenye siasa kubadili mambo, hakuna ushahidi hali ya kisiasa au maendeleo ya nchi fulani kubadilishwa na mungu au maombi. Mungu ni kwa ajili ya kuwapa matumaini tu binadamu wanapopitia mambo mazito na kutuliza hisia za watu kwa mambo yasiyoeleweka kama mwanzo wa ulimwengu na maisha.
 
Achana na issue za MUNGU katika mapambano. Pendekeza njia nyingine siyo maombi. Acha hiyo kitu. Kama maandamano hayawezi, basi maombi ndiyo ubatili kabisa.
Pendekeza another alternative.
Mimi naamini katika Mungu.ila ukweli ni kwamba maandamano kwa Tanzania hayawezi kufanikiwa na wengi watauawa.
 
Maandamano sio njia sahihi ya kuleta mabadiliko kwa sababu utasababisha umwagaji damu jambo ambalo ni mtaji kwa hao watu. Mfano maandamano yaliyopita hajakuleta mabadiliko bali wadhalimu wanaendelea na udhalimu wao kama mnavyoona.

Umwagaji damu kwa hao watawala dhalimu ni mtaji yani ni utoaji Kafara kwani wote hao ni watumishi wa mamlaka ya giza ndiyo maana hawaogopi kuua ndo maana sasa hivi wanasema hadharani kuwa watawaua waandamanaji na wanasema wataua zaidi ya walivyoua Mwanzo.

'Njia pekee ni Kumuomba Mungu asimamishe watu wake kwenye hizo nafasi za juu na watumike kuleta mabadiliko na kuwaangusha wadhalimu wote'.

Nina uhakika hilo linafanyika kwa sababu Mungu amesikia kilio cha watu wake waliouawa na hizi tawala dhalimu na ambao tupo hai ni suala la muda tu.
Mungu yupi sasa
 
Unaamini katika uwepo wa MUNGU?kama unamuamini Mungu hilo jambo linawezekana.kwa nchi kama Tanzania ambapo utawala wa kisheria haupo watu wakiandamana watauawa sana na wataendelea kubaki madarakani ila nchi zenye utawala wa kisheria maandamano yanaweza kufanya kazi.
Hujanijibu mkuu. Nimeuliza tu ni wapi/ nchi gani ishaondoa utawala dhalimu kwa maombi/sala?? Hayo ya kuamini au kutoamini wala hayana shida sana maana nchi yetu haina dini ila wanachi wake wanadini tofautitofauti so, hata hayo maombi ungetupendekezea yapitie imani gani ili tupeleke maombi yetu yajibiwe na Mungu.
 
Achana na issue za MUNGU katika mapambano. Pendekeza njia nyingine siyo maombi. Acha hiyo kitu. Kama maandamano hayawezi, basi maombi ndiyo ubatili kabisa.
Pendekeza another alternative.
Kwa hali ilivyo hakuna njia nyingine kweli, ya kujiuzulu si kweli ya wabunge kupiga kura ya kuto kuwa na imani hola , impeachment nayo ishafeli
 
Hujanijibu mkuu. Nimeuliza tu ni wapi/ nchi gani ishaondoa utawala dhalimu kwa maombi/sala?? Hayo ya kuamini au kutoamini wala hayana shida sana maana nchi yetu haina dini ila wanachi wake wanadini tofautitofauti so, hata hayo maombi ungetupendekezea yapitie imani gani ili tupeleke maombi yetu yajibiwe na Mungu.
Kwenye Biblia kama unaiamini kila muda Taifa la Israel walipotaka mabadiliko walimlilia Mungu,walitubu na mabadiliko yakaja.
 
Sasa hili sio taifa la Israel la Wayahudi, ni taifa la Waislamu, Wakristo, Wahindu, Wabudha, Wapagani, Atheists n.k Kama hata huyo mungu au miungu kweli yupo/wapo na anashughulikia/wanashugulika na mataifa sema atashughulikaje/watashugulikaje na taifa la namna hii.
 
Back
Top Bottom