Kijana wa Ifoza
JF-Expert Member
- Oct 31, 2025
- 1,180
- 2,302
Kwani unataka kusema serikali ya Burkina Faso iliyoangushwa na nguvu ya umma mnamo Oktoba 2014 ilikuwa inajali wananchi wake?Hizo ni kwa nchi zinazowajali wananchi wake ila kwa nchi zetu hizi za kiafrika maandamano yatasababisha mauaji ya kimbari /watu wengi na hao wadhalimu wataendelea kubaki madarakani.hao hawajali wananchi wanajijali wao.
Mkuu passioner255, ninaheshimu mtazamo wako lakini naomba kutofautiana nawe kwa hoja zifuatazo. Maoni yako yanaangukia kwenye mtego mkubwa sana wa kisaikolojia ambao watawala dhalimu wanataka wananchi wauamini: WOGA.Maandamano sio njia sahihi ya kuleta mabadiliko kwa sababu utasababisha umwagaji damu jambo ambalo ni mtaji kwa hao watu. Mfano maandamano yaliyopita hajakuleta mabadiliko bali wadhalimu wanaendelea na udhalimu wao kama mnavyoona.
Umwagaji damu kwa hao watawala dhalimu ni mtaji yani ni utoaji Kafara kwani wote hao ni watumishi wa mamlaka ya giza ndiyo maana hawaogopi kuua ndo maana sasa hivi wanasema hadharani kuwa watawaua waandamanaji na wanasema wataua zaidi ya walivyoua Mwanzo.
'Njia pekee ni Kumuomba Mungu asimamishe watu wake kwenye hizo nafasi za juu na watumike kuleta mabadiliko na kuwaangusha wadhalimu wote'.
Nina uhakika hilo linafanyika kwa sababu Mungu amesikia kilio cha watu wake waliouawa na hizi tawala dhalimu na ambao tupo hai ni suala la muda tu.
Usa ndio inawategemea Israel matajiri wengi ni wayahudi na wanamaarifa makubwa sana.Walimlilia Mungu gani?
Hao Israel mbona siku hizi hawamtegemei huyo Mungu tena na badala yake wanamtegemea US?
Amka toka usingizini kumekucha.Usa ndio inawategemea Israel matajiri wengi ni wayahudi na wanamaarifa makubwa sana.
Swali ni kwamba utaweza kuandamana kwa kwa siku hata zaidi ya 3 mfululizo huku ukibishana na watu ambao kuua kwao siyo kazi?watanzania sina uhakika kama tunaweza.narudia kusema Hao hawana uwezo wa kunilipa kwa hela ya damuKwani unataka kusema serikali ya Burkina Faso iliyoangushwa na nguvu ya umma mnamo Oktoba 2014 ilikuwa inajali wananchi wake?
Rais Blaise CompaorΓ© alikuwa dikteta aliyetawala Burkina Faso kwa mkono wa chuma kwa miaka 27 tangu mwaka 1987. Alikuwa hajali mtu na alijijali yeye mwenyewe, kiasi cha kutaka kubadili katiba ili abaki madarakani milele. Wananchi walipoamua kuingia barabarani na kuchoma moto majengo ya bunge, dikteta huyo hakuwa na ujanjaβalilazimika kukimbia nchi ndani ya siku chache tu. Hiyo ilikuwa nchi ya Kiafrika, na utawala ulikuwa dhalimu kupindukia, lakini nguvu ya umma ilishinda.
Mifano mingine ya hapa hapa Afrika inabomoa kabisa hoja yako:
Hakuna utawala dhalimu duniani unaojali wananchiβiwe Ulaya au Afrika. Watawala dhalimu wote tabia zao zinafanana: wanajijali wao wenyewe na wanatumia vitisho vya mauaji kulinda matumbo yao. Tofauti haipo kwenye tabia ya watawala, bali ipo kwenye ujasiri wa wananchi. Ukweli ni kwamba, madikteta wa Kiafrika wanaangushwa kila siku na nguvu ya umma pale wananchi wanapoamua kukataa woga.
- Sudan (2019): Omar al-Bashir alikuwa dikteta wa kijeshi aliyetawala kwa miaka 30 na alikuwa anaua watu bila huruma. Lakini maandamano endelevu ya wananchi barabarani yalimng'oa madarakani. Kwani yeye alikuwa anajali wananchi?
- Misri (2011): Hosni Mubarak alitawala kwa miaka 30 kwa msaada wa jeshi katili na usalama wa taifa wenye nguvu kubwa. Maandamano ya siku 18 tu ya wananchi yalimfanya aondoke madarakani.
NB: Narudia tena kusema wewe unajifanya unawapenda watanzania lakini haya maandishi yako yanaonekana ni mmoja ya wale watu wa system. Kama si kweli ni prove mimi wrong.
Sure.Nature itaamua tu
Ova
Mkuu, nchi inakoelekea ni Kubaya, kwa umri nilojaaliwa kidogo Kuna ukatili mkubwa sana. Matukio kama ya Mzee Kibao, Padre Kitima, Polepole, Lissu mpaka leo hakuna aliekamatwa na kushtakiwa,Sasa hapo maombi ya nani yatakubaliwa? Au Mungu hupokea maombi yapi kati ya maombi ya wananchi wengi wanaopata shida na ukatili wa moja kwa moja kutoka kwenye utawala au hao kina Mwamposa wanaofaidika na utawala dhalimu? Sabab Mungu anaona yanayotendeka na mateso wanayopitia watu wake. Atakuwa mjinga sana kupokea maombi ya Mwamposa na Mwaipopo ambao anawaona wanafaidika na utawala katili na kuacha maombi ya wengi wanaoteseka. Mkuu hii dunia ni katili sana na ukichunguza kwa makini ukishakuwa duniani kuna mambo ni maamuzi yako na siyo swala la Mungu na ingekuwa Mungu anasikiliza na kutekeleza maombi ya watu sidhani kama hii dunia ingekuwa hivi sbabu maombi ya wengi ni juu ya kuishi kwa amani,upendo na haki kwenye jamii.
Karibia asilimia 50 ya matajiri Marekani ni wayahudiAmka toka usingizini kumekucha.
Ndio maana nakwambia toka usingizini kumekucha,hujui hata unacho kiongea.Karibia asilimia 50 ya matajiri Marekani ni wayahudi
Kuna vitu vinachekesha ikiwemo iyo hoja dhaifu ya mtoa mada 'tumuachie Mungu 'Sawa mkuu, ila ni Wapi waliwahi kuangusha/ kuondoa utawala dhalimu na katili kwa maombi??!
Watanganyika mimi na wewe na yule ni midabwadaWatanzania hawawezi kuandamana hata kwa siku3 mfululizo.
Mkuu, inaonekana bado hujasoma vizuri hiyo mifano niliyokupa hapo juu, au unajifanya huielewi makusudi. Swali lako linaonyesha wazi jinsi ulivyotekwa akili na propaganda ya watawala dhalimu inayojengwa juu ya WOGA. Unaniuliza kuhusu kuandamana siku tatu mfululizo kupinga watu wanaoua, kwani nchi nilizokutajia walikaa masaa mawili tu barabarani?Swali ni kwamba utaweza kuandamana kwa kwa siku hata zaidi ya 3 mfululizo huku ukibishana na watu ambao kuua kwao siyo kazi?watanzania sina uhakika kama tunaweza.narudia kusema Hao hawana uwezo wa kunilipa kwa hela ya damu
Mwambie atasubiri kama vile anavyomsubiri Yesu miaka 2000 imeshapitaUkisubiri kila kitu Mungu akufanyie,Utasubiri saana na pengine isitokee
Mkuu hapa ndo tunahitaji kupata suluhu ya hayo matatizo ila kwa njia uliyopendekeza ya kuacha maandamano ya amani na kufanya maombi tu kwangu naona si mbinu sahihi ndo maana hata wewe mwenyewe umekosa hata mfano mmoja wa nchi iliyojikomboa kwa maombi kutokana na ukatili wa watawala. Tuangalie njia nyingine ukiachia hiyo ya Maandamano na Maombi, nadhani tuanzie hapo sababu kupiga magoti,kusujudu kwa kukesha makanisani tukilialia kumuomba Mungu aondoe huu utawala sidhani maana utawala huu ni wa mda mrefu na uovu wao ni wa mda sasa. Mungu anawaondoaje CCM nzima? Kwa gharika kuu au moto kutoka mbinguni kama Sodoma na Ghomora?? Tuje na suluhisho jingine tu.Mkuu, nchi inakoelekea ni Kubaya, kwa umri nilojaaliwa kidogo Kuna ukatili mkubwa sana. Matukio kama ya Mzee Kibao, Padre Kitima, Polepole, Lissu mpaka leo hakuna aliekamatwa na kushtakiwa,
Miaka ya 80s na 90s yaani hata ukiokotwa mwili usiojulikana lazima uchunguzi ufanyike na watuhumiwa wapatikane,
Sasa hivi watu wanapotea kama kuku hakuna anaejali,
ππππUsa ndio inawategemea Israel matajiri wengi ni wayahudi na wanamaarifa makubwa sana.
Unaiita maandamano ya amani lakini wenyewe hawayataki watu wakiandamana kutatokea mauaji ya Halaiki na wenyewe watabaki madarakani kwa sababu wanajeshi na polisi.Mbaya zaidi watanzania hamuwezi kukaza hata siku 3 .tutafute mbinu nyingine.Mkuu hapa ndo tunahitaji kupata suluhu ya hayo matatizo ila kwa njia uliyopendekeza ya kuacha maandamano ya amani na kufanya maombi tu kwangu naona si mbinu sahihi ndo maana hata wewe mwenyewe umekosa hata mfano mmoja wa nchi iliyojikomboa kwa maombi kutokana na ukatili wa watawala. Tuangalie njia nyingine ukiachia hiyo ya Maandamano na Maombi, nadhani tuanzie hapo sababu kupiga magoti,kusujudu kwa kukesha makanisani tukilialia kumuomba Mungu aondoe huu utawala sidhani maana utawala huu ni wa mda mrefu na uovu wao ni wa mda sasa. Mungu anawaondoaje CCM nzima? Kwa gharika kuu au moto kutoka mbinguni kama Sodoma na Ghomora?? Tuje na suluhisho jingine tu.
Hamtaki au na wanainfluence kubwa sana mpaka Marekani anapigana vita vyao wanaitawala Marekani.ππππ