Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Jambo lolote ukitaka kulifanya basi lifanye kwa sababu madhubuti na ikiwezekana pima nguvu itakayokuunga mkono.
Watanzania wote wanaumizwa na vifo vya wenzao na hasa vikiwa vya kutekwa.
Pamoja na hivyo Chadema kutaka kukitumia kifo cha Ali Kibao kama gia ya kupindua nchi hakujawahamasisha watu wengi.
Tangu mwenyekiti wa chama hicho atoe tamko lake la dharau kwa raisi ukipita mitaani huoni hiyo hamasa ya kushiriki maandamano yenye bango alilotangaza.
Chadema ikipenda kupata vuguvugu la watu kuandamana wasubiri tukio jengine la kuwavuta watu wengi na kwa hoja madhubuti.
Kwa hili la safari hii badala ya kuungwa mkono wanaweza wakakuta wananchi wanasaidiana kuwarushia madongo watakaoingia barabarani pamoja na kuwazomea.
Nahofia tamko la mwenyekiti litakivunjia hadhi chama chake kuliko safari yoyote iliyopita huko nyuma na sijui kulikuwa na kikao cha maamuzi au ilimtoka tu akiwa jukwaani.