Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Hatujakuomba ufafanuzi.Kuna mtu anaweza kudhani maandamano ya Kenya ni sheria ya fedha (Finance Bill) hapana!.
Maandamano hayo yana sura ya ukabila wa wazi ambao Naibu Rais anaujenga kupitia watu wa mlima, kwa maana ya wakikuyu. Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa siku za karibuni amekuwa akiimarisha siasa za ukabila kwa kutetea wakikuyu(watu wa mlima) akihitaji wapate zaidi katika mgawo wa raslimali dhidi ya makabila mengine.
Pia, maandamano hayo yameandaliwa na wakikuyu, lakini wajaluo wa Raila hawajaandamana. Si maandamano ya kitaifa. Ni jitihada za Naibu Rais kuonyesha kwamba bado ana nguvu, na Rutto asimdharau.
Tuangalie picha ya ndani ya maandamano, hao waandamanaji ni kama jini makata au subiani, wanatumwa, na wanatumika kutimiza ajenda ya ukabila na wako katika rescue mission ya Naibu Rais.
Katika siasa, hakuna tukio la bahati mbaya, all are staged and scriptured
Hao wa milimani ni raia wa nchi gani? Weka huo muswada hapa tuusome na tuchambue madai ya wanaoupinga...
Punguza kiherehere