Maandamano ya Kisiasa ndîo huomba Kibali Kwa Polisi. Maandamano ya wananchi hayaombagi Kibali Kwa Polisi au serikali. Boss haombi Kibali Kwa mtumishi.

Maandamano ya Kisiasa ndîo huomba Kibali Kwa Polisi. Maandamano ya wananchi hayaombagi Kibali Kwa Polisi au serikali. Boss haombi Kibali Kwa mtumishi.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MAANDAMANO YA KISIASA NDÎO HUOMBA KIBALI KWA POLISI. MAANDAMANO YA WANANCHI HAYAOMBAGI KIBALI KWA POLISI AU SERIKALI. BOSS HAOMBI KIBALI KWA MTUMISHI.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Maandamano ya Kesho kutwa tarehe 23/09/2024 siô maandamano ya wananchi isipokuwa maandamano ya Kisiasa yaliyoratibiwa na CHADEMA.
Hayawezi kufanikiwa Kwa sababu yanahitaji mambo meñgi ya msingi ili yaweze kufanikiwa.
Jambo la Kwanza NI Agenda, agenda ya maandamano ni kutokomeza Mauaji na utekaji, lakini Suluhu ya maandamano hayo Kwa Mujibu wa CHADEMA ni kuangushwa Kwa Utawala wa Rais Samia Kwa kauli Mbiu "SAMIA MUST GO"
Agenda pekee haitoshi katika kufanikisha maandamano.
Kûna sababu ñyiñgine àmbayo ni UUNGWAJI MKONO NA WANANCHI.
Kipengele Hiki ndicho ambacho kitafelisha hayo maandamano.

CHADEMA ni Chama kilichosajiliwa na serikali. Hivyo kinafuata maelekezo na masharti ya serikali ikiwemo kuomba vibali vya shughuli Zake. Hiyo pekee inaweza Kutoa pîcha kuwa maandamano hayo hayatafanikiwa.

Maandamano ya Chadema yataungwa na makundi Fulani ya wananchi ikiwemo wanachadema wènyewe, waliolewa agenda ya Chadema lakini siô wanachadema na wale waliodhurika na matendo ya utekaji na mauaji.
Maandamano ya tarehe 23 yatakosa uungwaji mkono WA kundi kûbwa la Wana CCM na baadhi ya vyama vingine vya upinzani.
Hii itapunguza kiwango cha mafanikio.

Kupanga tarehe ya maandamano pia ni ishara ya kuyafelisha maandamano. Yàani tukio litokee Leo au màtukio yatokee Leo alafu tarehe ya maandamano ipangwe Wiki tatu zijazo. Ari, shauku na Hasira za Watu automatically zitapoa.

Maandamano ya Wananchi hayahitaji ruhusa ya Polisi, sijui usalama au serikali. Hayahitaji KIBALI

Wananchi wanapochoka na kutaka Jambo Fulani Hawana huo Muda wa kuomba ruhusa Kwa uongozi wowote àmbao waô wènyewe ndîo wameuweka.

Kikawaida maandamano ya Wananchi Polisi na serikali haiwezi kuyashinda na haijawahi kuyashinda. Kûna mambo MAWILI kwèñye maandamano ya Wananchi.

1. Serikali kutekeleza matakwa ya Wananchi ili maandamano yakome.

2. Serikali kukaza Buti Kisha Wananchi waiangushe serikali.
Hatua hii NI hatua ya juu zaidi àmbapo husababisha machafuko ndàni ya nchi hasa vita ya wènyewe Kwa wènyewe.
Nchi kupasuka na vipande vipande,
Nchi kutotawalika.
Makundi ya Waasi yanayoipinga serikali.
Yàani hatua hii huwa mbaya zaidi.

Mfano wa maandamano ya Wananchi NI kama maandamano ya Wananchi wa Ngorongoro(Wamasai wa Ngorongoro). Pale ilikuwa ni mambo MAWILI, serikali ikaidi Moto uwake iwezekana Wamasai wa Ngorongoro watafute namna ya kujitenga na kuunda Taífa Lao. Bahati nzuri NI jamii Moja, ndugu, lugha Moja hivyo kukabiliana nao NI Kazi Kwa sababu watapigana Kufa kupona.

Wananchi wanapounganishwa na tatizo Moja huwa tayari Kwa kukabiliana na yeyote Bila kujali Matokeo.

Hii NI kusema Sisi watañzania siô Ndugu ila Kisiasa NI ndugu. Yaani Sisi NI ndugu kimaslahi.

Ukitaka ujue watanzania siô Ndugu isipokuwa ndugu Kisiasa. Angalia matukio yanayotokea. Mtanzania anaweza kutekwa au kuuawa lakini watanzania Wengine wakakaa kimya na Wala wasione uchungu Kwa Kifo cha Mtanzania mwenzao.

Anatekwa wakwanza, wapili, Watatu, wanne, kimya. Hii NI kiashiria kikubwa kuwa Hakuna undugu Baina ya watañzania.

Lakini Jana Hapa nimeona Huko umasaini Watu wamezuia Barabara, wameandamana, Kisa na mkasa Watoto wawili wametekwa. Yàani wawili tuu wametosha kufungua maandamano.

Huko Simiyu nako Hali ilikuwa hivyohivyo. Wale ni ndugu.

Ikifika Wakati Wananchi wakajiona ndugu ndîo itakuwa mwisho wa dhulma, uonevu na ukandamizaji.

Nawatakia Sabato Njema.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
 
Hakika mkuu..Maandamano ya Chadema hayawezi kufanikiwa..mpaka pale wananchi watakapo amua wao wenyewe.

Unaona Wamasai pale Ngorongoro
Hawafiki hata Laki Mbili lakini ungetaka uone Moto wa Nguvu ya umoja Watu wasingesikiliza matakwa Yao Kwa kutumia mabavu ungeona Moto.

Yàani watañzania Milioni 60 hawawezi kuwashinda Watu Laki Mbili weñye umoja.

Hapo Akili ni kuwakubalia alafu kuwapunguza Ñguvu Kwa kuwakabili kidôgo kidogo
 
Tatizo lako mleta mada utakuwa huna gari
Unajua Barabara zinasimamiwa na sheria za usalama barabarani? Wasimamizi wa sheria za usalama barabarani ni polisi

Huwezi ibuka tu ukaingiza maandamano barabarani bila kufuata sheria kuomba polisi yawe ya kidini,kisiasa,nk kwa wasimamizi wa sheria za barabarani
 
Tatizo lako mleta mada utakuwa huna gari
Unajua Barabara zinasimamiwa na sheria za usalama barabarani? Wasimamizi wa sheria za usalama barabarani ni polisi

Huwezi ibuka tu ukaingiza maandamano barabarani bila kufuata sheria kuomba polisi yawe ya kidini,kisiasa,nk wasimamizi wa sheria za barabarani

Wewe ndio hujui unachokozungumza lakini sikulaumu.

Wananchi ndio huunda serikali.
Wananchi ndio hujenga hizo Barabara.
Wananchi ndio huzaa Polisi na wanajeshi na hivyo vyombo vya Dola.
Wananchi ndio huwalipa Polisi na serikali.

Wananchi ndio huamua sheria Fulani ifanye kazi au isifanye kazi.
Sheria hutungwa kulingana na Mila, desturi na tamaduni za wananchi.

Bado sikulaumu kwa sababu uelewa wako ndipo ulipoishia.

Ukiambiwa ueleze ujumbe wa ulichokisoma sidhani kama utaweza kufafanua
 
Wewe ndio hujui unachokozungumza lakini sikulaumu.

Wananchi ndio huunda serikali.
Wananchi ndio hujenga hizo Barabara.
Wananchi ndio huzaa Polisi na wanajeshi na hivyo vyombo vya Dola.
Wananchi ndio huwalipa Polisi na serikali.
Ujinga mtupu umeandika kwani wafanyakazi wa serikali sio wananchi? Wanalipa kodi kupitia mishahara yao kuendesha serikali na kujenga hizo barabara kupitia direct ns indirect tax

Polisi na wanajeshi sio wananchi? Wanalipa kodi pia kuendesha serikali na kujenga hizo barabara kupitia direct na indirect tax
 
Ujinga mtupu umeandika kwani wafanyakazi wa serikali sio wananchi? Wanalipa kodi kupitia mishahara yao kuendesha serikali na kujenga hizo barabara kupitia direct ns indirect tax

Polisi na wanajeshi sio wananchi? Wanalipa kodi pia kuendesha serikali na kujenga hizo barabara kupitia direct na indirect tax

Sasa unauliza maswali àmbayo yanamajibu ndàni yake?
Huelewi hata unachokieleza. Embu soma ulichoandika
 
Back
Top Bottom