Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Mkuu ipo namna hii.Wewe inaonekana utakuwa na kitu kikubwa unakijua juu ya mkwamo wa vyama vya upinzani. Ebu weka kilakitu wazi mkuu ili tujue wengi
Chama cha Mapinduzi na serikali yake imewaandaa makada wake ambao hawaonekani sana frontier waingie upinzani kisha wakiwa huko wanawezeshwa kujenga hoja dhidi ya uongozi na hoja hizo mara nyingi effects zake ni duni.
Wanaaminiwa na kuingia kwenye nafasi za uongozi kwenye vyama na kinachoendelea ni kuhakikisha unapofika muda muafaka wa kufanya waliloagizwa ikiwemo kuvujisha siri za mikakati na vikao. Wakimaliza ngwe wanarudi home kuzawadiwa vyeo.
Akina Katambi, Mtatiro, Kitila na wengine ni ushahidi wa hili.
Kuna mengine mengi sana yanaendelea yanaogofya sana ila yanafanyika ili kuua upinzani wenye tija kwa nchi.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama baadhi vimeshageuzwa jumuiya za Chama (invisible) na wanafanya vizuri kweli