Maandamano ya kudai katiba mpya Eswatini yadaiwa kumfanya Mfalme Mswati III kukimbia nchi

Maandamano ya kushinikiza katiba mpya nchini Eswatini huenda yamemlazimisha Mfalme Mswati kukimbia nchi ,kwa mujibu wa Shirika la utangazaji la Afrika Kusini SABC.

Licha ya Vikosi vya usalama vya Eswatini-zamani ikiitwa Swaziland kutumia nguvu kupambana na waandamanaji uharibifu bado unaendelea.

Maandamano haya kwa kiasi kikubwa yamefanywa na vijana na yalishika kasi mwishoni mwa juma lililopita, licha ya jitihada za serikali za kupiga marufuku maandamano.

Waandamanaji hao wamekuwa wakimtaka Mfalme Mswati atoe nafasi kama sehemu ya mageuzi ya kidemokrasia, pamoja na uchaguzi huru na wa haki.

Chanzo: BBC Swahili
 
Yanayojiri Eswatini
Viongozi wa maandamano ya umma ambayo yamedumu kwa siku 3 wametangaza kuwa Mfalme Mswati III ameikimbia nchi na sasa amejificha nchini Afrika Kusini. Waandamanaji wanataka mabadiliko ikiwemo kuruhusu siasa za vyama vingi, na wananchi kuchagua Waziri Mkuu.
 
Dah, ivi amefanikiwa kimbia na wake zake wote? ama mmoja tu alompenda?
 
Yanayojiri Eswatini
Viongozi wa maandamano ya umma ambayo yamedumu kwa siku 3 wametangaza kuwa Mfalme Mswati III ameikimbia nchi na sasa amejificha nchini Afrika Kusini. Waandamanaji wanataka mabadiliko ikiwemo kuruhusu siasa za vyama vingi, na wananchi kuchagua Waziri Mkuu.
 
Fasta wawarukie wale Malkia wake atarudi...
 
Huyu bwege ametiana sana
 
Safi sana, na hii ni habari njema Sana kwa wanamageuko duniani kote

Wauza siraha tunaombea mandamano yaongeze nguvu kiduchu tu kuelekea kwenye machafuko ili tujipatie faida na kupunguza mzigo kwenye maghala!

Kazi kwenu Waafrika maana mlishashindwa kujitawala,
 
Hizo ni tetesi nimekaa Manzini miaka kadhaa. Watu wa Swaziland ni mafala kuliko hata watanzania. Jeshi na Polisi kote King Mswati kaweka familia yake ya Dlamini. Hakuna wa kumtoa wala kumtikisa. Subirini muone.
 
Dah blaza mwana kaacha vidosho wote kakimbia.. Hebu tufanye namna tukaokoe jahazi
Ni njia yako mkuu hiyo ukiwa unaenda bondeni pitia huko uache ukooπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸƒπŸƒπŸƒ au siku hizi huendagi bondeni??
 
mapinduzi sio lazima kwenye ballot box, wakizingua mnalianzisha.
 
Hivi tukimuashia moto Maza si kesho tu tutasikia yupo Unguja.

Yaani jamaa shababi kapigwa mkwara tena kwenye social media kakimbia nchi?? Huyu jamaa mzembe sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…