Maandamano ya Mabango kumtoa Rais Afrika ni kupoteza muda

Arsenal Gunner

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2022
Posts
10,891
Reaction score
17,718
Mimi binafsi naona kama maandamano ya amani ni ujinga na kupoteza mda.

Africa huwezi mtoa mtawala Kwa maandamano ya kubeba mabango naamini Desemba 9 watakufa watu na hamna kipya kitakachotokea yaani adui anabeba bunduki wewe unabeba bango.

Eti ukamtoe sifanyi huu ujinga mimi watu wamekufa kama kuku na hawakua na silaha yeyote halafu Mange alivyo mjinga hajalisema jeshi Kwa ujinga lilioufanya anaanza kupromote maandamano mengine

Nasema Mange njoo uandamane mwenyewe bhana

Hatuwezi kufa kijinga tena kama mpaka Leo waandamanaji hawajajua wanaenda kukutana na majangili yenye kutetewa na mtawala feki, hamna ukombozi hapo
 
Kama unataka silaha wala hayo sio maandamano ni (Jeshi / Military / Paramilitary) inayoweza kuendesha Guerrila warfare kama walivyofanya kina Kagame, Castro, Museveni, n.k. ni tofauti na jambo unalosema wewe unataka maandamano kuyafanya kama a military / paramilitary en-devour... Sasa sijui kiongozi wenu ni nani, silaha mnazo kiasi gani na mkishachukua nchi anaingia nani....

In short unachohubiri hapa ni kufanya wrongs mbili ili iwe right; wakati unachosema ni uhaini na maandamano ni Haki yako; na since kuna vichaa wanaoua watu na wana itchy fingers ndio maana binafsi sijamshauri mtu atoke, ila kila nayetoka ninamuelewa na namuunga mkono kwa kupigania Haki yake na inabidi alindwe na sio kupigwa...
 
Alindwe na nani ,?
 
Mimi binafsi naona kama maandamano ya amani ni ujinga na kupoteza mda.

Africa huwezi mtoa mtawala Kwa maandamano ya kubeba mabango naamini Desemba 9 watakufa watu na hamna kipya kitakachotokea yaani adui anabeba bunduki wewe unabeba bango.

Eti ukamtoe sifanyi huu ujinga mimi watu wamekufa kama kuku na hawakua na silaha yeyote halafu Mange alivyo mjinga hajalisema jeshi Kwa ujinga lilioufanya anaanza kupromote maandamano mengine

Nasema Mange njoo uandamane mwenyewe bhana

Hatuwezi kufa kijinga tena kama mpaka Leo waandamanaji hawajajua wanaenda kukutana na majangili yenye kutetewa na mtawala feki, hamna ukombozi hapo
We kaa tulia na watawala wanaokulisha, wengine tutaandama....nyie subirini maandamano ya kumpongeza daktari wa mchongo samuya kwakupata kura hewa ml 32!
 
Alindwe na nani ,?
Unadhani kwanini dunia nzima inapiga kelele na kila mwenye akili zake anapigia kelele kilichotokea na mauaji yaliyofanyika Tanzania ?!!! - Sababu kilichofanyika sio kwa kigezo chochote chini ya jua...

LAKINI - Unadhani Castro, Museveni, Kabila, Kagame na wengine wengi wangezimwa na kutokuweza kufanikiwa na lengo lao kuna mtu angepepesa macho au angesema ni uwanja wa mapambano ?

Sasa wewe unataka kulinganisha moja na lingine na kufanya hivyo hata nyenzo hauna kama za hao waliofanikisha dhamira yao.
 
Naimani watu walijifunza kitu tarehe 29,wao walienda kuandamana wenzao wakaja na risasi za kuwaua...imani yangu inaniambia huwezi fanya kosa mara mbili ushaona mwenzako alikuja kwania ya kukuua afu unapewa chance yapili ya kujiuliza eti unaenda tena ukiwa mikono mitupu hiyo najua haiwezekani...watu wanaplan zao na hapo ndipo tutakuja kukaa meza moja kunzungumza pale ambapo wote mtawala na mtawaliwa kuna kitu amekipoteza.
 
Kikawaida rais akishakataliwa na wananchi kuingia barabarani huwa anatakiwa kufungasha virago na kusepa na sio kung'ang'ania na kuanza kupambana na wananchi
Jiulize kwani maraisi wanaokimbia huwa hawana majeshi au huwa hawawezi kukodisha majeshi ya kuwalinda?? Ustaarabu huwa ni kusepaaaaaaa
Ving'ang'anizi huwa yanawakuta yaliyowakuta akina gadafi,sadam huseni na hata huyo wazir mkuu wa nepal hao ni kwa uchache tu!!
 
Chawa katumwa kukatisha watu tamaa.

Yeye anafikiri silaha zinashushwa na malaika kwa ajili ya Policcm tu na genge la Abdul.

Kasahau dunia ni kubwa sana wewe ukijua hili wenzako wanajua lile.

Tukutane field 9D.
Ingieni na mabango tupu halafu muone kifuatacho ITV
 
Mimi binafsi naona kama maandamano ya amani ni ujinga na kupoteza mda.

Africa huwezi mtoa mtawala Kwa maandamano ya kubeba mabango naamini Desemba 9 watakufa watu na hamna kipya kitakachotokea yaani adui anabeba bunduki wewe unabeba bango.

Eti ukamtoe sifanyi huu ujinga mimi watu wamekufa kama kuku na hawakua na silaha yeyote halafu Mange alivyo mjinga hajalisema jeshi Kwa ujinga lilioufanya anaanza kupromote maandamano mengine

Nasema Mange njoo uandamane mwenyewe bhana

Hatuwezi kufa kijinga tena kama mpaka Leo waandamanaji hawajajua wanaenda kukutana na majangili yenye kutetewa na mtawala feki, hamna ukombozi hapo
Umetoa milio ya kila aina lkn hujatoa solutions!!!
 
Naona bado wanakusanya na kodi, kwa maana wanakosa legitimacy pia wanapotea za hayo mamlaka
 
Ni vyema ukafunga Bakuli lako.

InaumaSana/ItHasAForkVery
 
Back
Top Bottom