Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Dare to know๐
Najiuliza tu hivi kwa jinsi Chadema ilivyo kama kweli wangemkamata mwana ccm akiwa na begi la kura feki wangemuacha salama kweli? Kama tu sasa hivi wanadiriki hata kutumia picha za mauaji ya nchi nyingine kutaka kuaminisha umma kuwa Tanzania kuna mauaji makubwa je wangeshindwa hata kumpiga picha mwanaccm au polisi au mtumishi wa tume ya uchaguzi aliyekutwa na kura feki?
Chadema wanaprint kura feki halafu wanajifanya wamezikamata, ili aliyekamatwa nazo hawamuoneshi na wala hawamchukulii hatua zozote. Wanaenda mbali na kukimbilia kuzichoma kura ikiwa ni kidhibiti cha ushahidi wao. Hawa jamaa wanatufanya watanzania watoto na mazoba wa kiwango cha juu.
Naandamana mimi,sio wewe,ni mimi..na atakaeuwawa ni mimi sio wewe...sitaki ushauri wako..keep it for yourself!
#Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana #Nitaandamana
Tuwaonee huruma tu. Kwanza CDM wameingia uchaguzi kila mtu na vyake. Mgombea hata kampeni moja hana m/ kiti wala katibu wa kitaifa. Mgombea hakumnadi mgombea ubunge hata mmoja kwenye jukwaa la kampeni. Watarajia nini hapo? Halafu leo wanaonyesha kura feki halafu wenyewe wanazichomq moto. Huo ni usanii. Utachoma exhibit kweli??? Watanzania iko akili. Alianza mange kimambi hawa watakuwa hali mbaya zaidi. Watanzania HATUDANGANYIKI.Najiuliza tu hivi kwa jinsi Chadema ilivyo kama kweli wangemkamata mwana ccm akiwa na begi la kura feki wangemuacha salama kweli? Kama tu sasa hivi wanadiriki hata kutumia picha za mauaji ya nchi nyingine kutaka kuaminisha umma kuwa Tanzania kuna mauaji makubwa je wangeshindwa hata kumpiga picha mwanaccm au polisi au mtumishi wa tume ya uchaguzi aliyekutwa na kura feki?
Chadema wanaprint kura feki halafu wanajifanya wamezikamata, ili aliyekamatwa nazo hawamuoneshi na wala hawamchukulii hatua zozote. Wanaenda mbali na kukimbilia kuzichoma kura ikiwa ni kidhibiti cha ushahidi wao. Hawa jamaa wanatufanya watanzania watoto na mazoba wa kiwango cha juu.
This is Sovereign state just to make the point open and clear.US na UK wamejipanga kuhakikisha uhuni unakomeshwa. Watahakikisha JPM anaondoka Ikulu. Just a Matter of time
Kawaandikie watu wa FacebookHizi propaganda mfu unazo kopi toka vigazeti vya Musiba zinajaza server bure!
Hawa wahuni siku hizi wanakopi ngojera na propaganda za vijarida uchwara vya Musiba wanakuja ku paste humu!!!!Huu ni ugolo mtupu. Maelezo mareeefu kumbe takataka tupu! Pumbavu kabisa.
Any dictatorial regime that torments it's innocent citizens cannot claim sovereigntyThis is Sovereign state just to make the point open and clear.
Kabla sijaendelea kusoma Comments niseme tuu ni kama upo akilini mwangu best.Tarehe 31 Oktoba tumeshuhudia kuitishwa kikao cha waliokosa nafasi mbalimbali za ubunge na urais ili kutangaza kufanya maandamano siku ya tarehe 2/11/2020. Tangu kuanzishwa kwa uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, vyama vya upinzani havijawahi kukubaliana na matokeo katika kila sehemu walizoshindwa. Kwa miaka ya nyuma viongozi wa juu wa vyama vya CHADEMA, CUF na ACT-Wazalendo walizoea kushinda na kurudhika na matokeo huku wakisaini malipo ya mishahara na posho za ubunge kila mwezi bila kujali majimbo ambayo wengine walipoteza katika vyama vyao.
Sote tunafahamu kuanguka kwa wenyeviti wa vyama kama Zitto Kabwe na Freeman Mbowe kumekuwa na mshtuko kwa watanzania kutokana na umaarufu na umashuhuri walionao kwa taifa lakini sio suala linalowashangaza wapiga kura katika majimbo yao kutokana na hali ya ushawishi wao ilivyopungua huko majimboni.
Suala tunalotakiwa kujiuliza juu ya uamuzi wa kuandamana, Je! Tunaandamana kwa lengo la kutafuta demokrasia au tunatumia kivuli cha demokrasia kutetea maslahi binafsi ya viongozi wa vyama vilivyoanguka? Ni kwa nini picha za mauaji yaaliyotokea nchi nyingine zitumike kuidanganya umma wa watanzania na jumuia za kimataifa kuwa mauaji haya yanatokea Tanzania? Majibu ya maswali haya yanatupekea kuamini kuwa nia si demokrasia bali ni maslahi binafsi.
Tukumbashane tu nchi ya Marekani na Kenya ndizo zimekuwa vinara wa ufutiliaji na ukosoaji wa uchaguzi huu. Taasisi kama FICHUA TANZANIA na TANZANIA ELECTION WATCH zimeonyesha kuwa na usajili kutoka serikali ya Kenya na ndizo zimekuwa zikiongoza mashambulizi dhidi ya ushindi wa CCM.
Sababu kubwa ambayo watanzania wanatakiwa kuielewa ni maslahi binafsi ya nchi kama Kenya na USA. Itambulike kwamba kuna vita kubwa kiuchumi na watu hawa wanaopanga kuandamana wamekuwa wakitumika kwa muda mrefu ili kuuza nchi yetu kwa ajili ya uchu wa madaraka na maslahi binafsi kwani wamekuwa wakipokea fedha nyingi ili kufanikisha vurugu kupitia mitandao ya kijamii. Kwa muda wa miaka mitano, Tanzania chini ya uongozi wa Magufuli, imeshuhudia mtazamo wa nchi kujitegemea kiviwanda na mikakati ya ujenzi wa miundombinu wezeshi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda imekuwa sumu kwa taifa la Kenya kwa sababu Tanzania imekuwa mnunuzi mkubwa wa bidhaa kutoka Kenya. Uwekezaji wa viwanda Tanzania ni mwiba kwa viwanda vya nchi hiyo.
Kwa upande wa Marekani (USA), sera ya demokrasia hutumika kama njia ya kuingilia kwenye nchi nyingi lakini kwa undani huwa ni maslahi ya kiuchumi na uwezo wa kutawala nchi za Africa. Suala kubwa ni kuvunjwa kwa mkataba mbovu wa SYMBION chini ya utawala wa Dr. John Magufuli. Hali hii imepelekea USA, kupiitia Balozi wake nchini Tanzania Dr. Donald J. Wright, kutumia mwamvuli wa demokrasia kuchafua serikali ya Tanzania baada ya kufuta mkataba huo. Katika mkataba huu tuliibiwa zaidi ya bilioni 6 kila mwezi na kuuziwa umeme kwa gharama kubwa sana. Watu kama MANGE KIMAMBI kupitia account za mitandao ya kijamii wa INSTAGRAM na GOODLUCK HAULE, KIGOGO2014, FATMA_KARUME, HILDERNEWTON21, JJMNYIKA kupitia account ya TWITTER ndio wamekuwa wakitumiwa sana kuhakikisha wanaharibu amani na kuchafua jina la Tanzania ndani na nje ya nchi.
Ikumbukwe kuwa vurugu za nchini Libya zilianza kwa maandamo ya kile kilichotajwa demokrasia lakini baadae mataifa makubwa yakiongozwa na marekani yalivamia kijeshi kupitia nafasi ya vurugu zilizoanzishwa na walibya wenyewe. Muda mfupi baadaye, uzalishaji wa mafuta ulishuka kwa kasi kutoka katika nchi iliyokuwa na hazina kubwa ya mafuta Africa na kuifanya nchi yenye uchumi unaosuasua ukiambatana na vita kabla ya Marekani kurudi na kukiri kufanya makosa katika uvamizi huku wakiiacha nchi wa Libya ikiendelea kuangamia kutokana na madhara ya vita hivyo.
Hali itakuwa hivyo Tanzania endapo tutawafuata wanaotaka kuandamana kwa maslahi binafsi.
Ukisikiliza kampeni zilivyokuwa zikiendeshwa kwa upande wa vyama vya upinzani, mtakubaliana na mimi kuwa mgombea wa CHADEMA alipanga kuandaa maandamano kwa kuwa alijua hawezi kushinda. Mara kadhaa amekuwa akihubiri kuwa iwe kwa amani au kwa vita anataka kushinda uchaguzi huu.
Hii iliashiria malengo ya kuharibu amani tangu siku ya kwanza. Ikumbukwe tu katika mpango huu, hata kama Jeshi halitaingilia kati, Vikundi maalumu vya CHADEMA na ACT-Wazalendo vimeandaliwa ili kuanzisha vurugu na kuwapiga waandamanaji wenzao ili kuonyesha jamii ya kimataifa kuwa Tanzania kuna vurugu. Tuepuke hili kwa nguvu zote ili kuondoa maslahi binafsi ya Freeman Mbowe, Maalim Seif, Tundu Lissu na Zitto kabwe.
Ifahamike tu kuwa Robert Amsterdam, mwanasheria na wakili wa Tundu Lissu, ambaye kwa sasa yupo Uturuki baada ya kuondoka aliwekwa kwa ajili ya kuhakikisha anafanikisha zoezi la kuleta vurugu na kuiacha Tanzania katika mazingira ya sintofahamu kabla ya mataifa makubwa kuingia na kuiba mali za nchi hii kupitia vita.
Niwapongeze watanzania kwa kutokubaliana na mkakati huu wa mataifa makubwa. Niwakumbushe tu huu ni wakati wa kuwaonyesha mabeberu namna watanzania tulivyo na umoja na tunavyoweza kuamua masuala yetu wenyewe bila kuwategemea wao ambao wanatuletea masharti ya ushoga na kutuibia malighafi kwa kigezo cha kupigania demokrasia.
Conspiracy theory; upinzani ukishindwa huwa kuna sababu, lakini wao wakishinda huwa ni haki yao. Upinzani Tanzania haujawahi kukubali matokeo ya uchaguzi wa rais tangu uchaguzi huo uanze takriban miaka 25 iliyopita.Tafadhari usiseme wananchi wameamua. Sema TISS na NEC
You gonna formulate all narratives. But the truth is. Treason for CCM is comingConspiracy theory; upinzani ukishindwa huwa kuna sababu, lakini wao wakishinda huwa ni haki yao. Upinzani Tanzania haujawahi kukubali matokeo ya uchaguzi wa rais tangu uchaguzi huo uanze takriban miaka 25 iliyopita.
Wahuni wengi tu wa ccm walikamatwa na mabegi yaliyojaa kura zilizokwishapigwa kwa ccm, wakaokolewa na washirika wao policcm - ambao pia walikuwa nazo.. Mwanza Kuna mmoja alipigwa sana, aliponea chupuchupu kuchomwa motoNajiuliza tu hivi kwa jinsi Chadema ilivyo kama kweli wangemkamata mwana ccm akiwa na begi la kura feki wangemuacha salama kweli?
Mkuu, usiongelee mambo usiyojua.. Kwenye uchaguzi huu kuna wananchi wengi wasio na hatia wameuawa Pemba, Tarime, Rorya, Mtwara, nk..wanadiriki hata kutumia picha za mauaji ya nchi nyingine kutaka kuaminisha umma kuwa Tanzania kuna mauaji makubwa
Hata mimi najiuliza angetangazwa Zitto, Mbowe bado wangejivua hizo nafasi? Wawaache na wenzao wale mema ya nchi tu hakuna namna.Hapo ni maslahi binafsi. Mbona serikali za mitaa waliacha lipite ?Halafu eti wanazuia wake wabunge wasiende kuapa. Mbowe acheni ubinafsi. Waacheni walioshinda waende. Nyie mliokatwa piaganieni haki huku nje.
Kwenye serikali za mitaa mliwatoa wenzenu mhanga kwa sababu nyie mlikuwa hamgombei. Sasa yamewakuta mnalia lia.