Uchaguzi 2020 Maandamano ya tarehe 2 Nov: Je, Ni Demokrasia au waliokosa wanapigania Maslahi Binafsi?

Uchaguzi 2020 Maandamano ya tarehe 2 Nov: Je, Ni Demokrasia au waliokosa wanapigania Maslahi Binafsi?

Huu upepo utapita tu, wengine tumesharudi kwenye hapakazi mode ila wengine bado wako kwenye political mode. Pole zenu sana.
 
mda huu watu 3 wamejeruhiwa vibaya baada ya kumwaga matunda Katika soko dogo hapa mtaa wa shunu, hadi sasa hali si rafki kwa wakaazi wa mtaa huu

CDM mbona fujo hivi?? Haya ndio maandamano ya amani??
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya demokrasia ya kupiga kura na demokrasia ya kukubali matokeo. Nadhani ni wakati wa kukubali matokeo kwasababu kura zilihesabiwa kwa uwazi mbele ya mawakala wa vyama vyote.. sidhani kama ni haki kutuharbia biashara zetu na mabomu yenu ya machozi.
 
mda huu watu 3 wamejeruhiwa vibaya baada ya kumwaga matunda Katika soko dogo hapa mtaa wa shunu, hadi sasa hali si rafki kwa wakaazi wa mtaa huu

CDM mbona fujo hivi?? Haya ndio maandamano ya amani??
Hakuna maandamano ya amani. Wangekuja kuniharibia biashara yangu ...ningewaingiza olimpiki
 
Abroad asylum seekers are struggling as much as they can to turnish our country. This is because they want to frame themselves as dissidents!

If you want to leave for your so called green pasture abroad just follow the friendly procedure, which will not harm your fellow countrymen. No one is restricting you to leave the country peacefully !
 
Conspiracy theory; upinzani ukishindwa huwa kuna sababu, lakini wao wakishinda huwa ni haki yao. Upinzani Tanzania haujawahi kukubali matokeo ya uchaguzi wa rais tangu uchaguzi huo uanze takriban miaka 25 iliyopita.
Unaonaje ukitoka nje ya boksi?
 
Hatuandamani ili kupiga picha. Tunaandamana ili kupinga udhalimu. Vyovyote vile, ni lazima kama binadamu tuliopewa akili na Mungu tupinge udhalimu kwa namna zote.
Niko hapa nasubiri wenzangu tuandamane. Mnafeli wapiiii? Mbona humu mnaongea kwa hisia kali lakini lodi hamtokeiiii?
Nimechoka kusubiri
 
The US Problem is not Tanzania Election Results but Termination of Symbion Power Project.

The CCN on October 30, 2020 published an article titled as, US cites credible allegations of fraud in Tanzania election.

The article alleged that there were serious doubts about the credibility of Tanzania’s presidential election while the leading opposition candidate urged countries not to recognize the results.

The article cited the US embassy in Tanzania saying that there had been credible allegations of significant election –related fraud and intimidation when voters were electing a president and lawmakers.

The statement from the US embassy in Tanzania should be taken as hypocrisy as voters elected the president and lawmakers peacefully. The same embassy itself released the statement on October 29th saying that the vote was peaceful and orderly in Tanzania mainland and Zanzibar.

Nevertheless, the question should be is the US really concerned about Tanzanian election results or it is using it as the pretext of hiding her interest in Tanzania.

The answer is obvious NO. The US is using the Tanzania election results to hide their interests in Tanzania.

The US still concerned with the fate of its dubious Symbion Power project that Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) terminated its contract in 2016 after discovering that the company was siphoning taxpayers’ money by charging billions of shillings a day while making a loss to TANESCO and disrupting power availability in the country.

After the contract was terminated, the US Symbion Power Tanzania Ltd on 13 March 2017 filed a request for arbitration at the International Chamber of Commerce (ICC) in Paris claiming breach of contract due to non-payment by Tanzania Electricity Supply Corporation (TANESCO) for power from the 126MW Ubungo plant (AE 331/1).

Symbion claimed that TANESCO had refused to pay for its power since the contract was agreed, claiming variously that the power purchase agreement (PPA) had been “put on hold”, never been signed or, later, that it had been rescinded.

In early 2011, Symbion had acquired a 120MW natural gas-fired power plant in Ubungo, Dar es Salaam.

Symbion also constructed two emergency power plants at Dodoma (55MW) and Arusha (50MW) to deliver power to the national grid during several years of drought when shortage of water in key dams and waterways depleted the hydroelectric resources available in the country.

The contract was for 15 years.
It was officially launched in 2013 by then the US President Barack Obama when the visited Tanzania under the name “the US Government’s Power Africa Initiative.

So, one can easily see why the US is not happy with the fifth government’s decision to terminate the symbion power project which was launched by the US President.

The four-year dispute with Symbion Power, an American power producer that develops and operates projects in several African countries is central cause for the anger.

Due to this, last month the US congress about the political and economic developments in Tanzania passed the resolution.

The House resolution 1120 Cites reports of corruption and harassment of U.S. companies operating in Tanzania
Several commercial disputes exist between US and Tanzania.

The four-year dispute with Symbion Power, an American power producer that develops and operates projects in several African countries is central among them.

The dispute is about the breach of a 15-year power purchasing agreement for the Ubungo power plant. The company alleged that the Tanzanian annulled the contract without giving neither cause nor compensation despite the efforts by the company to seek a mutually agreed to solution.

In the submission to the Office of the United States Trade Representative, Symbion questioned the eligibility of Tanzania to export duty-free apparel to the U.S under the African Growth and Opportunity Act (Agoa). As an AGOA beneficiary, Tanzania exported apparels worth $40 million to the U.S, supporting thousands of Tanzanian jobs.

The resolution by the Congress pointed out that Tanzania has adopted and enforced repressive laws limiting freedom of the press, and expression, assembly, and association.

The US House of Representatives voted for H. RES. 1120, a leading Democrat Rep. Karen Bass (D-CA) and Rep. Chris Smith (R-NJ) sponsored it. The passing of the resolution will empower the Trump administration to take the necessary legal justifications to impose economic and other punitive sanctions on Tanzania. Sanctions could affect several economic activities particularly major mining firms with operations in Tanzania.
 
Symbion ni mradi wa wana-CCM na mabeberu wa Kimarekani.
 
Hatuandamani ili kupiga picha. Tunaandamana ili kupinga udhalimu. Vyovyote vile, ni lazima kama binadamu tuliopewa akili na Mungu tupinge udhalimu kwa namna zote.
Mbona hujaonekana field? Mnapishana tu kwenye threads Jamii forums.. Maandamano ya kwenye simu yana impact ndogo sana ndo maana hua unatakiwa kuyatoa mtandaoni kuyapeleka field(barabarani). Au hayakuwa kwa masrahi ya mwananchi wa kawaida!
 
Tarehe 31 Oktoba tumeshuhudia kuitishwa kikao cha waliokosa nafasi mbalimbali za ubunge na urais ili kutangaza kufanya maandamano siku ya tarehe 2/11/2020. Tangu kuanzishwa kwa uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995, vyama vya upinzani havijawahi kukubaliana na matokeo katika kila sehemu walizoshindwa. Kwa miaka ya nyuma viongozi wa juu wa vyama vya CHADEMA, CUF na ACT-Wazalendo walizoea kushinda na kurudhika na matokeo huku wakisaini malipo ya mishahara na posho za ubunge kila mwezi bila kujali majimbo ambayo wengine walipoteza katika vyama vyao.

Sote tunafahamu kuanguka kwa wenyeviti wa vyama kama Zitto Kabwe na Freeman Mbowe kumekuwa na mshtuko kwa watanzania kutokana na umaarufu na umashuhuri walionao kwa taifa lakini sio suala linalowashangaza wapiga kura katika majimbo yao kutokana na hali ya ushawishi wao ilivyopungua huko majimboni.

Suala tunalotakiwa kujiuliza juu ya uamuzi wa kuandamana, Je! Tunaandamana kwa lengo la kutafuta demokrasia au tunatumia kivuli cha demokrasia kutetea maslahi binafsi ya viongozi wa vyama vilivyoanguka? Ni kwa nini picha za mauaji yaaliyotokea nchi nyingine zitumike kuidanganya umma wa watanzania na jumuia za kimataifa kuwa mauaji haya yanatokea Tanzania? Majibu ya maswali haya yanatupekea kuamini kuwa nia si demokrasia bali ni maslahi binafsi.

Tukumbashane tu nchi ya Marekani na Kenya ndizo zimekuwa vinara wa ufutiliaji na ukosoaji wa uchaguzi huu. Taasisi kama FICHUA TANZANIA na TANZANIA ELECTION WATCH zimeonyesha kuwa na usajili kutoka serikali ya Kenya na ndizo zimekuwa zikiongoza mashambulizi dhidi ya ushindi wa CCM.

Sababu kubwa ambayo watanzania wanatakiwa kuielewa ni maslahi binafsi ya nchi kama Kenya na USA. Itambulike kwamba kuna vita kubwa kiuchumi na watu hawa wanaopanga kuandamana wamekuwa wakitumika kwa muda mrefu ili kuuza nchi yetu kwa ajili ya uchu wa madaraka na maslahi binafsi kwani wamekuwa wakipokea fedha nyingi ili kufanikisha vurugu kupitia mitandao ya kijamii. Kwa muda wa miaka mitano, Tanzania chini ya uongozi wa Magufuli, imeshuhudia mtazamo wa nchi kujitegemea kiviwanda na mikakati ya ujenzi wa miundombinu wezeshi kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda imekuwa sumu kwa taifa la Kenya kwa sababu Tanzania imekuwa mnunuzi mkubwa wa bidhaa kutoka Kenya. Uwekezaji wa viwanda Tanzania ni mwiba kwa viwanda vya nchi hiyo.

Kwa upande wa Marekani (USA), sera ya demokrasia hutumika kama njia ya kuingilia kwenye nchi nyingi lakini kwa undani huwa ni maslahi ya kiuchumi na uwezo wa kutawala nchi za Africa. Suala kubwa ni kuvunjwa kwa mkataba mbovu wa SYMBION chini ya utawala wa Dr. John Magufuli. Hali hii imepelekea USA, kupiitia Balozi wake nchini Tanzania Dr. Donald J. Wright, kutumia mwamvuli wa demokrasia kuchafua serikali ya Tanzania baada ya kufuta mkataba huo. Katika mkataba huu tuliibiwa zaidi ya bilioni 6 kila mwezi na kuuziwa umeme kwa gharama kubwa sana. Watu kama MANGE KIMAMBI kupitia account za mitandao ya kijamii wa INSTAGRAM na GOODLUCK HAULE, KIGOGO2014, FATMA_KARUME, HILDERNEWTON21, JJMNYIKA kupitia account ya TWITTER ndio wamekuwa wakitumiwa sana kuhakikisha wanaharibu amani na kuchafua jina la Tanzania ndani na nje ya nchi.

Ikumbukwe kuwa vurugu za nchini Libya zilianza kwa maandamo ya kile kilichotajwa demokrasia lakini baadae mataifa makubwa yakiongozwa na marekani yalivamia kijeshi kupitia nafasi ya vurugu zilizoanzishwa na walibya wenyewe. Muda mfupi baadaye, uzalishaji wa mafuta ulishuka kwa kasi kutoka katika nchi iliyokuwa na hazina kubwa ya mafuta Africa na kuifanya nchi yenye uchumi unaosuasua ukiambatana na vita kabla ya Marekani kurudi na kukiri kufanya makosa katika uvamizi huku wakiiacha nchi wa Libya ikiendelea kuangamia kutokana na madhara ya vita hivyo.

Hali itakuwa hivyo Tanzania endapo tutawafuata wanaotaka kuandamana kwa maslahi binafsi.

Ukisikiliza kampeni zilivyokuwa zikiendeshwa kwa upande wa vyama vya upinzani, mtakubaliana na mimi kuwa mgombea wa CHADEMA alipanga kuandaa maandamano kwa kuwa alijua hawezi kushinda. Mara kadhaa amekuwa akihubiri kuwa iwe kwa amani au kwa vita anataka kushinda uchaguzi huu.

Hii iliashiria malengo ya kuharibu amani tangu siku ya kwanza. Ikumbukwe tu katika mpango huu, hata kama Jeshi halitaingilia kati, Vikundi maalumu vya CHADEMA na ACT-Wazalendo vimeandaliwa ili kuanzisha vurugu na kuwapiga waandamanaji wenzao ili kuonyesha jamii ya kimataifa kuwa Tanzania kuna vurugu. Tuepuke hili kwa nguvu zote ili kuondoa maslahi binafsi ya Freeman Mbowe, Maalim Seif, Tundu Lissu na Zitto kabwe.

Ifahamike tu kuwa Robert Amsterdam, mwanasheria na wakili wa Tundu Lissu, ambaye kwa sasa yupo Uturuki baada ya kuondoka aliwekwa kwa ajili ya kuhakikisha anafanikisha zoezi la kuleta vurugu na kuiacha Tanzania katika mazingira ya sintofahamu kabla ya mataifa makubwa kuingia na kuiba mali za nchi hii kupitia vita.

Niwapongeze watanzania kwa kutokubaliana na mkakati huu wa mataifa makubwa. Niwakumbushe tu huu ni wakati wa kuwaonyesha mabeberu namna watanzania tulivyo na umoja na tunavyoweza kuamua masuala yetu wenyewe bila kuwategemea wao ambao wanatuletea masharti ya ushoga na kutuibia malighafi kwa kigezo cha kupigania demokrasia.
Watz wamekataa maandamano. Wanasaccos waiteni mabeberu wakina Amsterdam waje waandamane wao!
 
Back
Top Bottom