Maandamano yanayoendelea yatufunze kuona haki za binaadamu kwa jicho pevu

Maandamano yanayoendelea yatufunze kuona haki za binaadamu kwa jicho pevu

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Katika nchi zinazoendelea watu wamekuwa wakiuawa na watu wasiojulikana au wengine wakifa mikononi mwa polisi.

Watu wamekuwa hawaoni umuhimu wa kuikumbusha serikali kuhusu hayo kwa visingizio kuwa aliyekufa au kuonewa alikuwa akifanya kazi fulani, tabia fulani au alikuwa na itikadi fulani hivyo wengi huona wanaokufa mikononi mwa polisi wanastahili kufa.

Hali hii kwa upande wetu imefanya uonevu uongezeke kwa kuwa watu wengi wakifa mikononi mwa mamlaka hakuna anayesimama kudai haki iliyoporwa.

Haki ya kuishi ni haki ya kila binaadamu, bila kujalisha ana tabia yake, itikadi au kazi. Pia serikali za Afrika zinaweza kujifunza kitu kwenye yanayoendelea katika maandamano yanayoendelea katika nchi hizo yanayosisitiza haki.

George Floyd inasemekana alikuwa ni 'PornStar' kitu ambach kibongobongo wangedhani ana haki ya kufa na hakuna ambaye angedai haki yake, au kama walivyo baadhi ya watu humu jamvini walioanza kusema kuwa jamaa alikuwa PornStar wakidhani kuwa inatosha kuwa sababu ya yeye kuuawa.

Hali inaonyesha kwa kiasi kikubwa nchi zinazoendeleahu-justify mauaji ya watu kwa sababu za kiitikadi au kitabia ili wasiweze kumpigania mtu, hata hao watu wa haki za binaadamu wamekuwa hawayapi uzito baadhi ya mambo ambayo nayo yapo katika haki za binaadamu kwa sababu tu ya kuwa judgemental.

Hivi karibuni nchini, Polisi waliwauawa waliosemekana kuwa ni majambazi, lakini bunduki na silaha nyingine waiziona baada ya kusachi, hii inamaanisha kuwa wale jamaa hawakuwashambulia polisi, sasakama hawakuwashambulia polisi kwa nini waliuawa, askari akasema Mwenye ndugu yake jambazi aende kuchukua maiti Muhimbili, hakusikika mtu kukemea tabia hii.

Washukiwa wa ujambazi na hata raia wamekuwa wakifa mikononi mwa polisi hata kama hawajawashambulia polisi, hali inayoshangaza katika kipengele kipi tunapata haki ya kuua hata kabala ya mahakama haijapitisha uamuzi wake.

Hizi zote ni haki za binaadamu lakini watu watasema, yule alikuwa jambazi, kahaba, mpinzani, nk kuwa kigezo cha haki yao kuuawa.

Wakati serikali inajifunza jinsi ya kuhandle maandamano, sisi tujifunze kutokuwa judgmental linapokuja suala la kupinga uonevu, tupunguze EGO ya kudhani kwamba fulani anaweza kuonewa ila mimi sitakiwi kuonewa, uonevu unapaswa kupigwa kwa nguvu zote kwa dimensions zote.
 
Back
Top Bottom