Baada ya takafuri nzito, kwa kiasi fulani maandanano yetu kupitia maoni yetu hapa JamiiForums yameanza kufanikiwa.
Tunaona viongozi walio na akaunti verified JF wanajitokeza kuandika masuala ya kisera na kujaribu kushirikisha umma kwa majadiliano mfano waziri wa Fedha ndugu Mwigulu Lameck Nchemba.
Pia tumeona baadhi ya maoni ya raia hapa JamiiForums yanafanyiwa kazi kwa kasi, mfano kutumbuliwa Nape Moses Nnauye
Tuendelee na maandamano yetu hapa JamiiForums ili tume huru ya uchaguzi ipatikane. Tuendelee na maandamano wakurugenzi Ma-DED makada wa CCM wasisimamie chaguzi majimboni.
Tuendelee kupiga kelele kwa maandamabo hapa JF wizara ya TAMISEMI isihusike na mchakato mzima wa uchaguzi wa 2024 wa viongozi wa vitongoji, vijiji na mitaa.
Tuendelee na maandamano hapa JF kupinga watu kuchukuliwa mitaani bila mashahidi kuwepo yaani majirani, mabalozi wa mitaa n.k ili watu wasiojulikana pia askari polisi wasitumie mamlaka vibaya.
Tuendelee kuandamana hapa JF kufuatilia utendaji wa mfumo wa haki jinai unapokengeuka
Au maandamano yetu hapa JamiiForums hayaleti yale tunayotamani, tutoke mtandaoni kuingia barabarani kama GEN-Z ikiwa viongozi wa serikali hawasikii maandamano yetu mrandaoni?