professional Driver
JF-Expert Member
- Sep 23, 2022
- 2,959
- 3,510
Hahahaha fanya kua umeeleweka alafu jiulize mwenyewe je alie laaniwa anaweza kua msaada tenaKama bado yupo Muislam anayeutumia huu mstari kujastify uninga wake basi kweli huyu anahitaji maombi. Nitakufafanulia kwa faida ya wote wenye upeo mdogo kama wako.
Wagalatia 3:13
13 Kristo alitukomboa katika laana ya torati, kwa kuwa alifanywa laana kwa ajili yetu; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti;
14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
Biblia inapozungumzia habari za Yesu kutukomboa inazungumzia Yesu kubeba dhambi zetu pamoja na laana zake ili sisi tuhesabiwe haki mbele za Mungu. Yesu hakuwa na dhambi lakini alikubali kusulubiwa ili achukue dhambi zetu na laana zetu.
Kwa hiyo kwenye huo mstari Paulo anajaribu kuwafafanulia wagalatia ni situation ipi inathibisha kuwa Yesu alibeba laana zao. Ndipo anapowaonyesha kuwa imeandikwa Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti.
Mstari unaofuata unaeleza kwanini Yesu pale msalabani alibeba laana za watu wote.
Biblia inasema
14 ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani.
So maana yake ni kwamba Yesu alisulubiwa kwa kuchukua dhambi zetu na laana zote zinazotokana na kutokufuata torati ambazo kimsingi zilikuwa zinawazuia watukupokea Baraka za ibrahimu na kupokea ahadi ya Roho Mtakatifu.
Sasa usipoelewa hapo najua ni ubishi tu lakini sitashangaa kwa sababu mgekuwa sio wabishi muda huu mngekuwa mahampokea kristu.
Mwanzo uliuliza kua Yesu ndio Mungu nani kamlaani sasa kupitia uo mstari na maelezo yako utupe jibu
Je Mungu kaamua kujipa laana mwenyewe