Tetesi: Maaskofu Katoliki wadaiwa kukutana na kujadili juu ya mkataba wa Serikali ya Samia na waarabu wa DP World

Habarini wapendwa kanisa kama taasisi imara itakaa na kupitia kwa kina kile walichokikosoa kwenye mkataba wa dp world na samia km kweli yamefanyiwa kazi au kiini nacho tu.

Ikumbukwe mkataba haujaonyeshwa kwa umma ila viongozi wamekuwa wakitamka yale yaliyomo kwenye mkataba.

Kwa kuwa bunge halitimizi wajibu wake kanisa linawajibu wa kufanya kazi bila kuwa na konakona.

Katibu wa TEC alitoa muda kwa Maaskofu kupitia mikataba iliyosainiwa kabla ya kukutana.

Mungu ni mwema.
Itakuwa ni kazi njema na iliyotukuka
Kwa sasa Tanzania Mkombozi ji Chadema na TEC tu.

Vile vyombo vyetu tulivyoamini vimeungana na wezi
 
Mi ningekuwa Samia ningelifuta kanisa katoliki halafu nione kama wataenda mahakamani. Sema tu ukilifunga unapukutisha ajira za mapadre na maaskofu mana huku mtaani hawaajiriki. Hakuna kampuni inayotaka elimu ya theology
Hahhaa eti Elimu ya Theology
 
Kanisa halina sababu yoyote ya kushindana na serikali.
Kanisa linatakiwa lisimame katika kweli ili taifa lipate uzima.
Maneno ya Yesu Kristo, " Mimi ndiye KWELI na UZIMA,.........
Ameeni ameen Mtumishi na Hiyo ndio Utume wa Kanisa
 
Naweza nikaamini .

Maana kanisa katoliki lina mfumo ndani ya mfumo.

Hawa sio wa kupuuza hata kidogo.
 
Hivi unajua walokole wamekuwa wengi siku hizi na wanatokea hukohuko catholic baada ya kuona Hilo siyo kanisa Bali ni utapeli tu na ubabe usiyokiwa na maana. Lini kanisa likatunishiana msuli na serikali wakati hata mungu ameshasema ya kaisali mpe kaisali na ya mungu yabaki kuwa ya mungu. Kanisa limekiw ala kiasiasa zaidi kuliko mambo ya rohoni. Ndo mana watu wanatafuta rescue kupitia ulokole au wanamtafuta mungu wa kweli kupitia ulikole
Kwa hiyo unataka kusema Tabia njema ni za Mungu na Tabia mbaya ni za Kaisari
 
Pumbavu, kuna tofauti gani kati ya serikali,bunge,na mahakama? Wakatoliki ni watanzania,kwa nini mambo yanayotokea Tanzania yasiwahusu? Yamuhusu nani sasa?
Kuna mipaka ya wakatoliki kwa maana ya uongozi wa kanisa katika kuingilia kinachofanyika serikalini.

IGA iliweza kuonwa na kila mtu na DPW akawa hana taabu kwani zile ni kanuni tu hazina masuala nyeti ya kibiashara.

Hakuna atakayekuja kuona kilichoandikwa kwenye mikataba hii ya kibiashara iliyosainiwa pale ikulu, hilo nakuhakikishia.

Halafu hao maaskofu wanamkosea heshima Rais kwa sababu ya uislam wake sio kwa sababu nyingine yoyote. Angekuwa hai JPM angeshaifanya hiyo biashara muda mrefu sana uliopita na kusingekuwa na suala la waraka kusambazwa makanisani.
 
Kwa fikra zako upo sahihi.Na ninaamini umepata taarifa jinsi nchi inavyowalipa mabilioni ya fedha za bure kabisa hao inaoingia nao mikataba mibovu kwa siri!Unadhani hali hiyo ya kuficha mikataba Ina afya kwa nchi na wananchi?Na ukiangalia vizuri hadi unajiuliza kama waliotia saini makubaliano wana visasi na nchi yao au uelewa wa wanayoyajaza ni tatizo?
 
Kwa fikra zako upo sahihi.Na ninaamini umepata taarifa jinsi nchi inavyowalipa mabilioni ya fedha za bure kabisa hao inaoingia nao mikataba mibovu kwa siri!Unadhani hali hiyo ya kuficha mikataba Ina afya kwa nchi na wananchi?Na ukiangalia vizuri hadi unaniuliza kama waliotia saini makubaliano wana visasi na nchi yao au uelewa wa wanayoyajaza ni tatizo?
Mkataba wa kibiashara unazo siri nyingi kati ya pande mbili kwa maana ya serikali na kampuni husika.

Kuna faida anapewa mwendeshaji kama DPW ambazo waendeshaji wengine mfano hawa wanaotafutwa kupitia tender zilizotangazwa, hawazijui hizo faida na wanatakiwa wasizijue.

Yapo mambo ambayo DPW anakubaliana na Tanzania kibiashara ambayo kampuni nyingine hazitakiwi ziyafahamu.

Tusipende kuangalia suala la mkataba kwa mtazamo huo mmoja kwamba nchi inawalipa mabilioni kwa makosa yanayokuwepo kwenye mikataba, pia tuangalie na leo na kesho pande hizi mbili za kibiashara zina uhusiano gani.

Huo mkataba wa kibiashara ukiwekwa wazi, mimi na wewe tutakuwa na msaada gani juu ya vipengele vilivyomo?. Kwamba tunalipa mabilioni kwa yanayoandikwa kwenye mikataba sio nongwa wala kigezo cha kuzilazimisha mamlaka zikaweka kila kitu wazi, hilo ni kosa la kisheria kuruhusu mkataba wa kibiashara uliosainiwa mbele ya rais ukajadiliwa na umma kupitia JF na facebook.

Tutakuwa ni taifa fulani la kipuuzi sana tukijadili commercial agreements ambazo zinakwenda kutekeleza biashara ya TPA.
 
elimu elimu elimu mikataba ya kimataifa wasifikirie ni sawa mikataba ya ajira hata mikataba ya ajira ni siri baina ya mwajiri na mwajiriwa
 
Upo sawa kabisa. Lowassa hakukosea hata kidogo alipoziongelea zile elimu tatu pale Jangwani mwaka 2015 wakati wa kampeni.

Huwezi kujadili commercial agreement hadharani kama vile ni mkataba wa kupangisha nyumba za uswahilini.
 
Hao hao walio walikwa chamwino kula pilau

Ccm Ni kichwa kigumu
 
Nipo pamoja na kanisa katoliki
Mkataba ulipaswa uwe wazi kwa maslahi ya Taifa
 
hakuna cha maslahi wala chochote zaidi ya mrija kukatwa bass imetosha mulichokipata kinatosha kwa mfano tu nyumbani kwako pana upenyo nyani anapitia hapo kujichukulia japo kitu ili ale kisha wewe upazibe hapo mahali atakuvamia kupitia mlango wa mbele elewa hilo
 
elimu elimu elimu mikataba ya kimataifa wasifikirie ni sawa mikataba ya ajira hata mikataba ya ajira ni siri baina ya mwajiri na mwajiriwa
haya kuna ndege imetua hapo kia imekuja na wawekazi kutoka america tuangalie tec wapo wateme cheche kabla au munaonaje kwa maslahi hao ni wazungu wanatupiga risasi huko kwao kila kukicha
 
Upo sawa kabisa. Lowassa hakukosea hata kidogo alipoziongelea zile elimu tatu pale Jangwani mwaka 2015 wakati wa kampeni.

Huwezi kujadili commercial agreement hadharani kama vile ni mkataba wa kupangisha nyumba za uswahilini.
Tusiwe tunajikaririsha vitu kwa sababu ya mahaba ya aliyeongea.Kuna faida gani ya hizo siri kama kila mara tunapelekwa kwenye hasara,aibu na kuonekana hatuna uwezo wa kutumia akili kwa kiwango stahiki?Na wanaoleta kadhia hizo ikumbukwe ni wale tunaowaita nguli wa taaluma husika au wanasiasa tu.
 
Mkataba wa kibiashara unazo siri nyingi kati ya pande mbili kwa maana ya serikali na kampuni husika.

Kuna faida anapewa mwendeshaji kama DPW ambazo waendeshaji wengine mfano hawa wanaotafutwa kupitia tender zilizotangazwa, hawazijui hizo faida na wanatakiwa wasizijue.

Yapo mambo ambayo DPW anakubaliana na Tanzania kibiashara ambayo kampuni nyingine hazitakiwi ziyafahamu.

Tusipende kuangalia suala la mkataba kwa mtazamo huo mmoja kwamba nchi inawalipa mabilioni kwa makosa yanayokuwepo kwenye mikataba, pia tuangalie na leo na kesho pande hizi mbili za kibiashara zina uhusiano gani.

Huo mkataba wa kibiashara ukiwekwa wazi, mimi na wewe tutakuwa na msaada gani juu ya vipengele vilivyomo?. Kwamba tunalipa mabilioni kwa yanayoandikwa kwenye mikataba sio nongwa wala kigezo cha kuzilazimisha mamlaka zikaweka kila kitu wazi, hilo ni kosa la kisheria kuruhusu mkataba wa kibiashara uliosainiwa mbele ya rais ukajadiliwa na umma kupitia JF na facebook.

Tutakuwa ni taifa fulani la kipuuzi sana tukijadili commercial agreements ambazo zinakwenda kutekeleza biashara ya TPA.
Kwa hiyo ni vema zaidi tuendelee na siri zenye hasara kila leo!?
 
Tusiwe tunajikaririsha vitu kwa sababu ya mahaba ya aliyeongea.Kuna faida gani ya hizo siri kama kila mara tunapelekwa kwenye hasara,aibu na kuonekana hatuna uwezo wa kutumia akili kwa kiwango stahiki?Na wanaoleta kadhia hizo ikumbukwe ni wale tunaowaita nguli wa taaluma husika au wanasiasa tu.
Tunalipa mabilioni kwa sababu ya uzembe wetu lakini pia kuuweka mkataba hadharani wakati umesainiwa mbele ya mkuu wa nchi ni uzembe mwingine, tena una hasara za kiwango kile kile kama ile tunaoupata baada ya wanasheria wetu kushindwa kesi huko nje.
 
Habarini wapendwa kanisa kama taasisi imara itakaa na kupitia kwa kina kile walichokikosoa kwenye mkataba wa dp world na samia km kweli yamefanyiwa kazi au kiini nacho tu.

Ikumbukwe mkataba haujaonyeshwa kwa umma ila viongozi wamekuwa wakitamka yale yaliyomo kwenye mkataba.

Kwa kuwa bunge halitimizi wajibu wake kanisa linawajibu wa kufanya kazi bila kuwa na konakona.

Katibu wa TEC alitoa muda kwa Maaskofu kupitia mikataba iliyosainiwa kabla ya kukutana.

Mungu ni mwema.
km mkataba haujaoeshwa kwa umma huo wanaoujadili wameutoa wapi, labda huo utakuwa mkataba wa ndoa kati ya babako na mamako. Kweli akili ndogo huuhangaisha mwili. Mtu km wewe ingekuwa bora wazazi wake wangetumia condom asizaliwe mpumbavu km wewe
 
Back
Top Bottom