Maaskofu Wakatoliki Zambia: Hali iliyojitokeza baada ya uchaguzi imeweka mashaka kuhusu uadilifu wa mchakato huo

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Baraza la Maaskofu Katoliki Zambia (ZCCB) limeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu mwenendo wa uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 13, 2026, likisema hali iliyojitokeza baada ya uchaguzi imeweka mashaka kuhusu uadilifu wa mchakato huo.

Katika taarifa yao ya kichungaji yenye kichwa “Peace sown by peacemakers brings a harvest of justice”, maaskofu hao wamesema hawazungumzi kwa maslahi ya chama chochote cha siasa au mgombea, bali wanatetea Katiba, utawala wa sheria na haki ya kila Mzambia kuhakikisha kura yake inahesabiwa na kuheshimiwa.

Soma: Uchaguzi Zambia 2026: Matokeo kutoka majimbo 135 kati ya 226, Hichilema aendelea kuongoza

Maaskofu hao pia wameeleza masikitiko yao kuhusu uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) wa kusimamisha uhesabuji na kutangazwa kwa baadhi ya matokeo ya uchaguzi mnamo Agosti 14, 2026, kufuatia taarifa za vurugu dhidi ya maafisa wa uchaguzi na madai ya wizi wa nyaraka za uchaguzi.

Taarifa hiyo inasisitiza umuhimu wa kulinda amani, haki na uwazi katika mchakato wa uchaguzi, huku ikitaka mamlaka husika kuhakikisha kila kura ya wananchi inahesabiwa kwa usahihi na matokeo ya uchaguzi yanaaminika.

1786947005919.png

1786955801124.png

1786955928977.png

1786947013660.png
 
Hili kanisa huku afrika limeamua kufanya siasa, kuhubiri injili imeshindikana?
 
Hao maaskofu huko Zambia ndiyo waamuzi, nchi ya kikristo hiyo
 
Nilidhani kwa huku Tz shida ya hilo kanisa ni issue ya bandari.
 
Hili kanisa huku afrika limeamua kufanya siasa, kuhubiri injili imeshindikana?
Wako sahihi kabisa, wasisubiri hadi watu wauane ndio waanze kulalamika ni jukumu la watumishi wa Mungu kukemea uovu bila kujali unafanywa na nani.

Watumishi wa Mungu wanaokaa kimya ni watumishi wa uongo na kwa hili tunaliunga mkono kanisa katoliki hasa katika bara la Afrika.
 
Kote tz na Zambia wanajihusisha na siasa kwa ajili ya mirija hazina
 
Back
Top Bottom