Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Hili kanisa huku afrika limeamua kufanya siasa, kuhubiri injili imeshindikana?
Hao maaskofu huko Zambia ndiyo waamuzi, nchi ya kikristo hiyoBaraza la Maaskofu Katoliki Zambia (ZCCB) limeeleza wasiwasi mkubwa kuhusu mwenendo wa uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 13, 2026, likisema hali iliyojitokeza baada ya uchaguzi imeweka mashaka kuhusu uadilifu wa mchakato huo.
Katika taarifa yao ya kichungaji yenye kichwa “Peace sown by peacemakers brings a harvest of justice”, maaskofu hao wamesema hawazungumzi kwa maslahi ya chama chochote cha siasa au mgombea, bali wanatetea Katiba, utawala wa sheria na haki ya kila Mzambia kuhakikisha kura yake inahesabiwa na kuheshimiwa.
Soma: Uchaguzi Zambia 2026: Matokeo kutoka majimbo 135 kati ya 226, Hichilema aendelea kuongoza
Maaskofu hao pia wameeleza masikitiko yao kuhusu uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) wa kusimamisha uhesabuji na kutangazwa kwa baadhi ya matokeo ya uchaguzi mnamo Agosti 14, 2026, kufuatia taarifa za vurugu dhidi ya maafisa wa uchaguzi na madai ya wizi wa nyaraka za uchaguzi.
Taarifa hiyo inasisitiza umuhimu wa kulinda amani, haki na uwazi katika mchakato wa uchaguzi, huku ikitaka mamlaka husika kuhakikisha kila kura ya wananchi inahesabiwa kwa usahihi na matokeo ya uchaguzi yanaaminika.
Ya kaisari mpe kaisari,ya Mungu mpe Mungu-mtoto wa bikira mariaUnaweza kutaofutisha injili na siasa ?
Wako sahihi kabisa, wasisubiri hadi watu wauane ndio waanze kulalamika ni jukumu la watumishi wa Mungu kukemea uovu bila kujali unafanywa na nani.Hili kanisa huku afrika limeamua kufanya siasa, kuhubiri injili imeshindikana?
Kote tz na Zambia wanajihusisha na siasa kwa ajili ya mirija hazinaWako sahihi kabisa, wasisubiri hadi watu wauane ndio waanze kulalamika ni jukumu la watumishi wa Mungu kukemea uovu bila kujali unafanywa na nani.
Watumishi wa Mungu wanaokaa kimya ni watumishi wa uongo na kwa hili tunaliunga mkono kanisa katoliki hasa katika bara la Afrika.
... walipoambiwa na Vatican wajitegemee ndo balaa limezidi!Hili kanisa huku afrika limeamua kufanya siasa, kuhubiri injili imeshindikana?
Injili lhuubiriwa pia kwa vitendoHili kanisa huku afrika limeamua kufanya siasa, kuhubiri injili imeshindikana?
Sio kweli, anayepinga lazima atakuwa ni jihadist tu hilo liko wazi kabisa.Kote tz na Zambia wanajihusisha na siasa kwa ajili ya mirija hazina
Uganda tu ndo wako kimyaIla wakatoliki wanajitahidi sana kifokea ubadhirifu kwenye mataifa,hii nzuri sana.
Sijaona siasa hapoHili kanisa huku afrika limeamua kufanya siasa, kuhubiri injili imeshindikana?
Ila umeona injili ya matayo?Sijaona siasa hapo
Ya kaisari mpe kaisari ya Mungu mpe Mungu-yesuInjili lhuubiriwa pia kwa vitendo