Naomba niseme mimi ni mkiristo tena Mseminari safi, niliyefunzwa nikafunzika. Ila naomba niseme MAASKOFU ni wanafiki.
Wakati wa bunge la Katiba, hatukuona kiongozi yeyeto wa dini ya Kikristo amabye alitoka nje kuungana na UKAWA, inakuwaje leo wanasema Katiba ni ya chama kimoja? Naomba niseme karibia viongozi wote wa dini ni wanafiki tu. Kitu kimoja amacho naamini kuwa wanaweza kuwadanganya wanadamu lakini sio MUNGU, Sizungumzii tu katika hili la kupinga katiba bali katika mambo mengi. Mimi huwa nawaona ni wa kawaida sana.
Kama kweli wanamaono toka kwa MUNGU kwanini wasingesimama kipindi kile na kukemea kisawasawa? na wangewaamuru wanaowakilisha watoke.
Naomba nisimulie kitu kimoja.
Wakati tukiwa seminarini pale Mbalizi Siminari, tulikuwa na Mkuu wa seminari (RECTOR) kwa sasa ni marehemu alikuwa anasema kwamba, ikitokea KIRANJA amekupa adhabu, halafu ukaigomea, maana yake ni kwamba umemgomea RECTOR ambaye amemteua huyo kiranja, na kama umemgomea Rector maana yake umemgomea Askofu wa Jimbo ambaye amemteua huyo Rector kuwa hapo, na kwa maana hiyo umemgomea Kadinali na kwa maana hiyo umemgomea Papa(Baba Mtakatifu), na kwa maana hiyo hiyo umemgomea YESU KRISTO ambaye kamteua huyo Papa, na kwa maana hiyo umemgomea MUNGU MWENYEZI aliyemleta mwanaye mpendwa duniani. Hivyo wewe uliyemgomea kiranja adhabu hufai kuendelea kuwepo hapo seminari, zawadi kubwa unayopaswa kuzawadiwa ni kufukuzwa seminarini. Na nikujuze tu kuwa seminarini viranja wana nguvu na wanaogopwa sana.
Sasa katika hili la Maaskofu, je ni nani alipendekeza majina ya hao viongozi wa dini walioyeuliwa kwenye bunge la KATIBA? na walikuwa wanamuwakilisha nani?
Hapo hapo niunganishe na hadithi nyingine.
Kulikuwa na kaka angu, yeye alikuwa kanisa moja la kilokole, sisi wengine tukiwa ni RC. Na yeye kaka yetu alikuwa anatuona sisi kama ni wahuni na tumepoteza mwelekeo, sasa kuna siku akasema ameoteshwa na MUNGU kuwa dada fulani atakuwa ndo mke wake na huyo dada walikuwa wanasali kanisa moja, lakini sisi wahuni tukamwambia kaka huyo dada unayetaka kumuoa hajatulia, na sisi tumekumbana naye sana katika matukio kadhaaa, yeye akawa anabisha, ikawa ni ugomvi mkubwa sana katika familia, yeye akasisitiza ameonyeshwa na ROHO MTAKATIFU, Lakini ukweli ni kwamba alikuwa anashinikizwa na mchungaji wa hili kanisa maana huyo dada alikuwa ni ndugu wa huyo mchungaji, kama mjuavyo siku hizi watu wanamfuata na kumuamini mtu zaidi kuliko neno la MUNGU. basi kama familia tukaridhia, na mahari ikatolewa. Sasa tukiwa tunasubiri kuanza mipango ya lini harusi ifungwe, siku moja kaka kwa macho yake mwenyewe akamfumania huyo mchumba wake anafumuliwa MARINDA. Akajifanya kutuficha lakini siku zilivyokuwa zinakwenda akasema yeye hatamuoa, tukamuuliza kwanini akasema ROHO MTAKATIFU amemtokea kuwa yule sio mke, kumbuka hapo Mahari tayari tumetoa.
Binafsi nikamuuliza hebu tueleze huyo MUNGU wako ambaye leo anakuonyesha kijani halafu kesho anakuonyesha nyekundu.
Sasa hizi habari zinafanana na haya wanayoyafanya maaskofu leo hii.