Dragunov Sniper
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 2,795
- 9
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema amefurahishwa na uamuzi wa Tamko la Maaskofu wa Makanisa yote nchini ya kuikataa Katiba Pendekezwa.
Jaji Warioba amesema ni ukweli ulio wazi kwamba maoni mengi watanzania waliyotoa yamepuuzwa kwenye Bunge la Katiba la Samwel Sitta na badala yake kuingizwa maoni ya watawala.
Jaji huyo mstaafu amesema Tamko la Maaskofu kuomba muda zaidi wa kusoma katiba pendekezwa kabla ya kura ya maoni ni muafaka kabisa hasa ikizingatiwa viongozi wa dini ndiyo wenye waumini.
Tayari leo Jumapili Makanisa yote ya Kikatoliki nchi nzima umesomwa waraka wa kinabii wa kuikataa katiba pendekezwa kwani imebeba maoni ya chama kimoja tu cha CCM.Na waraka umesisitiza katiba hiyo ilipatikana kwa njia ya HILA kubwa.
Mwaka jana Shura ya Maimamu wa dini ya Kiislamu ndiyo ilikuwa taasisi ya kwanza ya dini kuikataa katiba Pendekezwa na kuwataka Waislam wote kupiga kura ya HAPANA
Nadhani viongozi wetu wa kiroho wamejisau kuwa wao sio sehemu ya wanasiasa,ndio maana kanisa lilitenganisha siasa na dini,Sasa nashangaa hawa maaskofu wetu wanapogeuka mawakala wa siasa, sisi waumini tumeshtushwa sanaa na mwenendo wa viongozi wetu.ndio maana hata Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania Kardinali Pengo Katika mahubiri yake wakati wa kufungua mafungo ya Wanawake Wakatoliki Tanzania, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. alisema hatuwezi kufikia hatua ya kusema nenda kapige kura ya hapana, hakuna mtu aliye na uwezo wa kumwambia mwingine akapige kura ya hapana, hakuna mwadadamu aliye na uwezo huo. Kama mungu mwenyewe hafanyi hivyo, mwanadamu anayapata wapi madaraka hayo
sasa nyie Maaskofu mmepata wapi ujasiri wa kuanza kufanya uwakala wa shughuli za siasa ndani ya Kanisa Takatifu la Mungu,Kwani huo ndio wito mlioitiwa?