Ta Muganyizi
R I P
- Oct 19, 2010
- 5,355
- 2,736
Wewe kodoa macho tu kama mjusi aliyebanwa na mlango maana mbivu na mbichi utajajuaga soon!
Sio limesomwa katoliki tu hata huku kwetu KKKT tumesomewa na hatuwezi kwenda kinyume na tamko hlo.
Tamko limetoa ufafanuzi nzuri sana kuhusu katiba inayopendekezwa kwa namna ilivyopindisha uhalisia na kumbeba mtawala...tamko hili limeweka wazi sababu ya msingi ya kuipigia kura ya HAPANA
Ninaunga mkono waraka huu
ni kwel huko nakanisa yote ya roman imesomwa? ngoja niulizie
Naomba niseme mimi ni mkiristo tena Mseminari safi, niliyefunzwa nikafunzika. Ila naomba niseme MAASKOFU ni wanafiki.
Wakati wa bunge la Katiba, hatukuona kiongozi yeyeto wa dini ya Kikristo amabye alitoka nje kuungana na UKAWA, inakuwaje leo wanasema Katiba ni ya chama kimoja? Naomba niseme karibia viongozi wote wa dini ni wanafiki tu. Kitu kimoja amacho naamini kuwa wanaweza kuwadanganya wanadamu lakini sio MUNGU, Sizungumzii tu katika hili la kupinga katiba bali katika mambo mengi. Mimi huwa nawaona ni wa kawaida sana.
Kama kweli wanamaono toka kwa MUNGU kwanini wasingesimama kipindi kile na kukemea kisawasawa? na wangewaamuru wanaowakilisha watoke.
Naomba nisimulie kitu kimoja.
Wakati tukiwa seminarini pale Mbalizi Siminari, tulikuwa na Mkuu wa seminari (RECTOR) kwa sasa ni marehemu alikuwa anasema kwamba, ikitokea KIRANJA amekupa adhabu, halafu ukaigomea, maana yake ni kwamba umemgomea RECTOR ambaye amemteua huyo kiranja, na kama umemgomea Rector maana yake umemgomea Askofu wa Jimbo ambaye amemteua huyo Rector kuwa hapo, na kwa maana hiyo umemgomea Kadinali na kwa maana hiyo umemgomea Papa(Baba Mtakatifu), na kwa maana hiyo hiyo umemgomea YESU KRISTO ambaye kamteua huyo Papa, na kwa maana hiyo umemgomea MUNGU MWENYEZI aliyemleta mwanaye mpendwa duniani. Hivyo wewe uliyemgomea kiranja adhabu hufai kuendelea kuwepo hapo seminari, zawadi kubwa unayopaswa kuzawadiwa ni kufukuzwa seminarini. Na nikujuze tu kuwa seminarini viranja wana nguvu na wanaogopwa sana.
Sasa katika hili la Maaskofu, je ni nani alipendekeza majina ya hao viongozi wa dini walioyeuliwa kwenye bunge la KATIBA? na walikuwa wanamuwakilisha nani?
Hapo hapo niunganishe na hadithi nyingine.
Kulikuwa na kaka angu, yeye alikuwa kanisa moja la kilokole, sisi wengine tukiwa ni RC. Na yeye kaka yetu alikuwa anatuona sisi kama ni wahuni na tumepoteza mwelekeo, sasa kuna siku akasema ameoteshwa na MUNGU kuwa dada fulani atakuwa ndo mke wake na huyo dada walikuwa wanasali kanisa moja, lakini sisi wahuni tukamwambia kaka huyo dada unayetaka kumuoa hajatulia, na sisi tumekumbana naye sana katika matukio kadhaaa, yeye akawa anabisha, ikawa ni ugomvi mkubwa sana katika familia, yeye akasisitiza ameonyeshwa na ROHO MTAKATIFU, Lakini ukweli ni kwamba alikuwa anashinikizwa na mchungaji wa hili kanisa maana huyo dada alikuwa ni ndugu wa huyo mchungaji, kama mjuavyo siku hizi watu wanamfuata na kumuamini mtu zaidi kuliko neno la MUNGU. basi kama familia tukaridhia, na mahari ikatolewa. Sasa tukiwa tunasubiri kuanza mipango ya lini harusi ifungwe, siku moja kaka kwa macho yake mwenyewe akamfumania huyo mchumba wake anafumuliwa MARINDA. Akajifanya kutuficha lakini siku zilivyokuwa zinakwenda akasema yeye hatamuoa, tukamuuliza kwanini akasema ROHO MTAKATIFU amemtokea kuwa yule sio mke, kumbuka hapo Mahari tayari tumetoa.
Binafsi nikamuuliza hebu tueleze huyo MUNGU wako ambaye leo anakuonyesha kijani halafu kesho anakuonyesha nyekundu.
Sasa hizi habari zinafanana na haya wanayoyafanya maaskofu leo hii.
songea pia tumesomewa nawapongeza maaskofu kwenye mambo ya msingi tuache ushabiki. katiba ndo maisha yetu, ambayo yanawahusu watu wa dini zote pamoja na maaskofu wenyewe. naona wamefanya uamuzi wa busara sana. Mimi ni kada wa CCM ila kwa haya siungi mkono maendeleo tunahutaji wote si baadhi ya watu tu.
ni kwel huko nakanisa yote ya roman imesomwa? ngoja niulizie
Waraka umesomwa kwa makanisa yote ya RC Arusha, Dar na kwengineko!
Naomba niseme mimi ni mkiristo tena Mseminari safi, niliyefunzwa nikafunzika. Ila naomba niseme MAASKOFU ni wanafiki.
Wakati wa bunge la Katiba, hatukuona kiongozi yeyeto wa dini ya Kikristo amabye alitoka nje kuungana na UKAWA, inakuwaje leo wanasema Katiba ni ya chama kimoja? Naomba niseme karibia viongozi wote wa dini ni wanafiki tu. Kitu kimoja amacho naamini kuwa wanaweza kuwadanganya wanadamu lakini sio MUNGU, Sizungumzii tu katika hili la kupinga katiba bali katika mambo mengi. Mimi huwa nawaona ni wa kawaida sana.
Kama kweli wanamaono toka kwa MUNGU kwanini wasingesimama kipindi kile na kukemea kisawasawa? na wangewaamuru wanaowakilisha watoke.
Naomba nisimulie kitu kimoja.
Wakati tukiwa seminarini pale Mbalizi Siminari, tulikuwa na Mkuu wa seminari (RECTOR) kwa sasa ni marehemu alikuwa anasema kwamba, ikitokea KIRANJA amekupa adhabu, halafu ukaigomea, maana yake ni kwamba umemgomea RECTOR ambaye amemteua huyo kiranja, na kama umemgomea Rector maana yake umemgomea Askofu wa Jimbo ambaye amemteua huyo Rector kuwa hapo, na kwa maana hiyo umemgomea Kadinali na kwa maana hiyo umemgomea Papa(Baba Mtakatifu), na kwa maana hiyo hiyo umemgomea YESU KRISTO ambaye kamteua huyo Papa, na kwa maana hiyo umemgomea MUNGU MWENYEZI aliyemleta mwanaye mpendwa duniani. Hivyo wewe uliyemgomea kiranja adhabu hufai kuendelea kuwepo hapo seminari, zawadi kubwa unayopaswa kuzawadiwa ni kufukuzwa seminarini. Na nikujuze tu kuwa seminarini viranja wana nguvu na wanaogopwa sana.
Sasa katika hili la Maaskofu, je ni nani alipendekeza majina ya hao viongozi wa dini walioyeuliwa kwenye bunge la KATIBA? na walikuwa wanamuwakilisha nani?
Hapo hapo niunganishe na hadithi nyingine.
Kulikuwa na kaka angu, yeye alikuwa kanisa moja la kilokole, sisi wengine tukiwa ni RC. Na yeye kaka yetu alikuwa anatuona sisi kama ni wahuni na tumepoteza mwelekeo, sasa kuna siku akasema ameoteshwa na MUNGU kuwa dada fulani atakuwa ndo mke wake na huyo dada walikuwa wanasali kanisa moja, lakini sisi wahuni tukamwambia kaka huyo dada unayetaka kumuoa hajatulia, na sisi tumekumbana naye sana katika matukio kadhaaa, yeye akawa anabisha, ikawa ni ugomvi mkubwa sana katika familia, yeye akasisitiza ameonyeshwa na ROHO MTAKATIFU, Lakini ukweli ni kwamba alikuwa anashinikizwa na mchungaji wa hili kanisa maana huyo dada alikuwa ni ndugu wa huyo mchungaji, kama mjuavyo siku hizi watu wanamfuata na kumuamini mtu zaidi kuliko neno la MUNGU. basi kama familia tukaridhia, na mahari ikatolewa. Sasa tukiwa tunasubiri kuanza mipango ya lini harusi ifungwe, siku moja kaka kwa macho yake mwenyewe akamfumania huyo mchumba wake anafumuliwa MARINDA. Akajifanya kutuficha lakini siku zilivyokuwa zinakwenda akasema yeye hatamuoa, tukamuuliza kwanini akasema ROHO MTAKATIFU amemtokea kuwa yule sio mke, kumbuka hapo Mahari tayari tumetoa.
Binafsi nikamuuliza hebu tueleze huyo MUNGU wako ambaye leo anakuonyesha kijani halafu kesho anakuonyesha nyekundu.
Sasa hizi habari zinafanana na haya wanayoyafanya maaskofu leo hii.
Ukawa wazo lenu la kususia kura ya maoni lilikuwa la msingi lkn kutokana na guvu hii ya kanisa shirikini kwenye kura ya hapana
aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba jaji joseph warioba amesema amefurahishwa na uamuzi wa tamko la maaskofu wa makanisa yote nchini ya kuikataa katiba pendekezwa.
Jaji warioba amesema ni ukweli ulio wazi kwamba maoni mengi watanzania waliyotoa yamepuuzwa kwenye bunge la katiba la samwel sitta na badala yake kuingizwa maoni ya watawala.
Jaji huyo mstaafu amesema tamko la maaskofu kuomba muda zaidi wa kusoma katiba pendekezwa kabla ya kura ya maoni ni muafaka kabisa hasa ikizingatiwa viongozi wa dini ndiyo wenye waumini.
Tayari leo jumapili makanisa yote ya kikatoliki nchi nzima umesomwa waraka wa kinabii wa kuikataa katiba pendekezwa kwani imebeba maoni ya chama kimoja tu cha ccm.na waraka umesisitiza katiba hiyo ilipatikana kwa njia ya hila kubwa.
Mwaka jana shura ya maimamu wa dini ya kiislamu ndiyo ilikuwa taasisi ya kwanza ya dini kuikataa katiba pendekezwa na kuwataka waislam wote kupiga kura ya hapana

mapambano kila kona ushindi wanukia
sio limesomwa katoliki tu hata huku kwetu kkkt tumesomewa na hatuwezi kwenda kinyume na tamko hlo.