Maaskofu wamtembelea Freeman Mbowe gerezani, wasema yuko Imara kuendelea kupigania Katiba Mpya

Maaskofu wamtembelea Freeman Mbowe gerezani, wasema yuko Imara kuendelea kupigania Katiba Mpya

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,358
Leo tarehe 8 Agosti 2021, sisi Askofu Emmaus Mwamakula na Askofu William Mwamalanga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe kuhusu Maadili, Amani na Haki, tuliongoza Ujumbe Maalum wa Viongozi wa Dini kutembelea Magereza na Mahabusu Mkoani Dar es Salaam kwa lengo la kuwajulia hali mahabusu wa kisiasa. Katika sehemu zote tulizokwenda, tulipokelewa vizuri na kufanisha lengo lengo kwa kiasi kikubwa kama taarifa fupi hapa chini inavyoeleza:

UKONGA: Tulipata muda wa kuongea na Freeman Mbowe. Tulimpa ujumbe wa viongozi wa dini na baadaye tukapata nafasi ya kumsikiliza. Alitueleza kuwa hali yake ya kiafya ilikuwa nzuri kabisa na kwamba hakuwa na shida ye yote na 'wenyeji wake' ambao ni Askari wa Jeshi la Magereza pale Ukonga. Alieleza kusikitishwa kwake jinsi walinzi wake 3 amabo ni wanajeshi wanaoshitakiwa pamoja naye katika Kesi ya Ugaidi walivyopata mateso kupitia mikono ya Jeshi la Polisi na kuwekwa ndani kwa kipindi cha mwaka mzima. Anasema aliamua kuwa na walinzi waliokuwa ni Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ili kuimarisha ulinzi wake baada ya kushambuliwa na kuvunjwa mguu kule Dodoma. Ameeleza pia kutokuridhishwa na kitendo cha Jeshi la Polisi kuendelea kuwakamata na kuwaweka mahabusu viongozi wa CHADEMA wanaojitokeza kusikiliza Kesi yake Mahakamani. Hata hivyo, amewashukuru Watanzania wote wanaoendelea kumuombea nchi nzima nzima. Amewataka Watanzania wote kuungana katika kuandika Katiba Mpya!

MBURAHATI: Baada ya kutoka Ukonga, tuliwatembelea mahabusu ambao ni viongozi 12 wa CHADEMA wanaoshikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Mburahati ambao walikamatwa Segerea wakiwa wanafanya Kikao cha Ndani. Tulikuta hali isiyo nzuri ya mahusiano kati ya mahabusu wale na Askari waliokuwa zamu wa Kituo cha Mburahati. Tulishughulikia changamoto ile kwa njia ya mazungumzo na sala na hatimaye kurejesha mahusiano na pande zote mbili ziliweza kusameheana. Mazingira hayakuruhusu kuwaona mahabusu wote lakini tulifanikiwa kuonana na viongozi wao 3 ambao ni Gerva Lyenda, Asenga na Mwita. Pia, tuliruhusiwa kuonana na mahabusu 2 wanawake. Mwishoni, tuliwaona mahabusu 2 ambao ni watu wazima akiwemo mzee wa miaka 74 ambao walipelekwa Hospitali kwa matibabu. Leo ilikuwa siku ya 6 tangu wakamatwe pasipo kufikishwa Mahakamani.

CENTRAL POLICE: Tulifika jioni sana kule Posta. Kwa sababu ya muda, tuliruhusiwa kuonana na kiongozi wao ambaye ni Katibu Mkuu wa BAWACHA, Catherine Ruge. Alitueleza changamoto ambayo tuliweza kuifikisha kwa Afisa wa Jeshi la Polisi ambaye alituhakikishia kuwa ataishughulikia. Leo ilikuwa siku ya 4 tangu wakamatwe pasipo kufikishwa Mahakamani. Catherine alitueleza kuwa kulikuwa na mahabusu 30 waliokamatwa walipokwenda kuhudhuria Kesi ya Mbowe katika Mahakama ya Kisutu. Alieleza kuwa baadhi ya waliokamatwa hawakuwa wanachama wa CHADEMA, bali walisombwa tu katika kamatakata. Alieleza zaidi kuwa wengi wa waliokamatwa ndugu zao hawajui kuwa walikuwa wamekamatwa.

Muono wetu kama viongozi wa dini kuhusu ziara hiyo ni kama ifuatavyo: Kitendo cha kuwakamata na kuwaweka ndani viongozi na wanachama wa CHADEMA kwa sababu zilizoelezwa kinalipaka matope Jeshi la Polisi na kinazidi kuinajisi Katiba ya Nchi. Kesi ya Freeman Mbowe inalichafua Taifa letu machoni duniani. Tunafahamu pia kuwa kuna viongozi na wafuasi wengine wa CHADEMA waliokamatwa mikoani kwa sababu za kudai Katiba Mpya. Kudai Katiba Mpya sio jinai.

Ni kwa sababu hiyo, tunatoa wito wa kuachiliwa huru kwa mahabusu wote pasipo masharti ye yote. Kuendelea na Kesi ya Mbowe hakuijengei heshima nchi yetu. Hivyo, tunatoa wito kwa Serikali kuifuta Kesi hiyo kwani kuendelea nayo na kuendelea kukamata watu wanaodai Katiba Mpya ni kujenga mazingira ya kutibua utulivu nchini. Sisi Maaskofu tuliofanya ziara hiyo tumefanya hivyo tukiwawakilisha viongozi wengine wa dini na tumetimiza wajibu wetu (Ezekieli 33:1-20).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kwa niaba ya Viongozi wa Dini waliotembelea Gereza la Ukonga, Mahabusu ya Mburahati na Mahabusu ya Central Police, Dar es Salaam.
 
Asante kwa taarifa.
Kesi ya Mbowe muiachie mahakama kwakuwa tayari imeshafunguliwa.

Ombi langu kwenu viongozi wa dini.
1.Mmuandikie ujumbe/waraka Sirro.
2.Mumuombe Mabeyo mkutane ana kwa ana mtoe hisia zenu.
NB!
Kama ambavyo mumeeleza kuwa tunachafuka kimataifa ni sahihi kabisa.
Kama Mabeyo hatawasikiliza basi nanyi itawapendeza sana mkubaliane viongozi wote wa dini kuanza kutoa elimu ya katiba mpya kwenye nyumba za Ibada kwa dk 5.
Amani kwenu!
 
Hawa maaskofu mbona wanatoa hitimisho la kipuuzi namna hii?

Kesi ya Mbowe imeshafikishwa mahakamani, sasa wanawashwa na nini tena kuanza kusema eti inachafua taswira ya nchi!??

Kwani kuna ambae yupo juu ya sheria, au kuwa Mwenyekiti wa chama cha siasa inakupa kinga ya kutokushitakiwa kwa jambo lolote lihusulo uvunjaji wa sheria?

Pia, tunapohubiri kuheshimu misingi ya demokrasia, utawala bora na haki za binadamu,,, sasa kwann kwa Sabaya iwe ni sawa kwamba Serikali inatenda na kufuata utawala bora ila kwa Mbowe imekuwa sio tena kutenda haki bali uonevu? Double standard

Mbowe huyu huyu alikataza watu wasije msiba wa Kaka yake kisa kuepusha maambukizi kwa Jamii yake, ila baada ya mazishi akakimbilia Mwanza kufanya mkusanyiko bila kujali kuwa huko kutapelekea kueneza maambukizi. Kwahyo akaona Jamii ya wana Mwanza wacha wafe tu ilimradi mrengo wake kisiasa utimie. Ila nyie Maaskofu uchwara mkakaa kimya

Kwa double standard hizi, ni wazi nyie maaskofu uchwara mnatumikia upande mmoja na sio kutumikia wananchi wote

Watanzania wenzangu tuweni makini na hawa kina kibweteres' type waliopo Tanzania.
 
Back
Top Bottom