Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Najilaumu hadi Leo kuacha kusoma cookery halafu kipindi chetu wanaume ilikua mnasoma free kipindi cha mama kilato pale kibasila . Nikajifanya sayansi na French nikaacha kidato cha tatu. Nilikua nafurahia vipindi vya mwalimu wa fizikia RIP Benedict mgini. Kipindi kile kuna monthly test kila mwisho wa mwezi . Kwa mama kilato umenikumbusha
 
Dah, mulemule ase
 
Aisee mm sipendi mno hio biashara ya vyombo na ndio inanifanya nikale mgahawani ilihali kila kitu ninacho ndani
Hili la kuosha vyombo ndo litafanya wengi wetu tuoe mapema, sometimes huwa nabaki tu nacheka, unakuta nimerundika vyombo vya almost week nzima jikoni.
 
Mi naweza kupika misosi ya aina zote.but inshu huwa ipo ktk kuchochea maharagwe mpaka yaive hapo ndo shughuri huwa naishia kuunguza tu kutokana na kupitiwa usingizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana nimetulia zangu getoni, mara nje naskia mboga mboga! Roho ikafurahi nikasema ngoja leo nichemshe mboga mboga. Najikoki kutoka tuu naskia jamaa anakomaa..."Mbogaa mbooooga kina mama humo ndani" mbogaa mbogaa kina dada humo ndani "mbogamboooga mashangazi jamani!!! Kiukweli nilighairi pale pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…