Tetesi: Mabadiliko Baraza la Mawaziri; J. Makamba, Mhagama, Ummy Mwalimu nje; Adadi Rajabu, Bashe watajwa

Tetesi: Mabadiliko Baraza la Mawaziri; J. Makamba, Mhagama, Ummy Mwalimu nje; Adadi Rajabu, Bashe watajwa

Teua baba wana wa Israel kutoka-Kilimanjaro kwenye baraza lako uone mafanikio na baraka kwenye baraza lako.
Kilimanjaro ccm imekataliw, labda unaota mchana
Teua baba wana wa Israel kutoka-Kilimanjaro kwenye baraza lako uone mafanikio na baraka kwenye baraza lako.
Kilimanjaro ccm imekataliwa, labda unaota mchana
 
Muda wowote mabadiliko makubwa yanategemea kutokea katika baraza la mawaziri ambapo mawaziri kadhaa watatemwa kutokana na sababu kadhaa.

1. Jenister Muhagama - Anatuhumiwa kwa kuzunguka mamlaka za teuzi (Rais na Waziri Mkuu) katika sakata la kumteuwa kaimu mkurugenzi wa NSSF... Mhagama alitenda kosa hilo akishirikiana na Balozi Ombeni Sefue ambaye kwa sasa kashatumbuliwa.

2. January Makamba - Maranyingi amesikika na kurekodiwa akimsema vibaya Rais, akimsengenya Rais pamoja na kuratibu mipango mbalimbali ya kumdhoofisha Rais Magufuli. haya anayatenda katika Hotel ya Protea Dar es Salaa., na Dodoma ambapo amekuwa akifanya vikao vya siri usiku wa manane na baadhi ya wabunge wa upinzani, pamoja na wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wa sukari

3. Ummy Mwalimu - Inasemekana kasi na uwezo wake mdogo haumrithishi Rais kwa sasa..

Katika mabadiliko hayo Adadi Rajabu, Mbunge wa Muheza inasemekana anaweza kuingia kuchukua nafasi ya Kitwanga, wengine wanaotajwa ni Bashe, mbunge wa Nzega ambaye anaweza kupewa docket ya Mazingira au Maliasili na pia Serukamba amekuwa akitajwa.

Mytake: wananchi kwa umoja wetu tumuunge mkono Rais Magufuli ana dhamira njema kabisa la kuwatumikia watanzania.

hapo labda Adadi , hao wengine kina bashe timu luwasa hao, alafu bashe ana uwezo gani jamani hebu tuache propaganda
 
Hii thread imenifanya nimkumbuke sana ndugu Filikunjombe. Dah!!!
Apumzike kwa Amani.
 
Bashe ni mvumilivu, ni jasiri haogopi, Nadhani anafaa kuwa Waziri, amenifurahisha sana jinsi alivyokata ishu katika bunge hili.

Huyu dogo Makamba ni strategist mzuri lakini alinikera alivyoanza kumsema vibaya JK mtu aliyemmentor na kumsaidia kufika hapa alipofika. Akiwekwa pembeni siwezi kulia machozi.

Kuhusu Mwigulu, huyu ni mzalendo wa Ukweli na kamanda wa ukweliukweli, alijiuzuru unaibu katibu mkuu wa CCM bila kujali kuwa ana slim chance ya kupitishwa na CCM kugombea uraisi.
 
JPM kama kweli anataka tusonge mbele awateue na baadhi ya wabunge wa upinzani kuwa mawaziri mfano zitto, mdee,Bulaya ama lissu. hapo tutasonga. hawa wa ccm ni walewale tu.....
 
Lowasa kafanya kipi kuhatarisha usalama wa nchi ?? Amekaa zake kimya ,sasa nawashangaa nyie mnaosema sijui January atamwaga ugali kisa anajua yote yaliyofanyika kwenye uchaguzi na Magufuli hana ubavu wa kumgusa ,

Wakiamua ataguswa na hana la kufanya huyo January








Si lazima kila jambo lihatarishe usalama wa nchi,nchi yetu ipo salama si kwa sababu ya uimara wa vyombo vyetu vya kiusalama,bali ni kwa sababu ya uvumilivu na ustahimilivu wetu hata pale dola linaposimamia na kubariki uhalamia wa watu wachache waliojiapiza kubaki madarakani hata kama walikataliwa kwenye sanduku la kura.

Ni Watanzania pekee ambao unaweza kuwapiga kibao shavu la kushoto,kisha kwa unyenyekevu wa kipekee wakakugeuzia na shavu la kulia ukawapiga.Uthibitisho wa haya niyasemayo ni uchaguzi wa Zanzibar,CCM ilishindwa uchaguzi lakini kwa sababu ya nguvu ilizonazo iligoma kuachia madaraka.Ushahidi wa kushindwa kwao upo wazi,kama wazanzibar kwa kauri moja walimchagua Mh.Lowassa kuwa Rais wa JMT,na kumuacha kwa mbali mno Magufuli,unafikiri walifanya nini kwa Kipenzi chao Mh.Maalim Seif?

Credibility ni nyenzo ya msingi katika kutimiza majukumu ya kisiasa,jamii isipokuamini haiwezi kutilia maanani hata yale unayojaribu kuwaaminisha kuwa unayafanya kwa ajili yao,unafikiri washiriki hawa wa ushindi wa ccm hawana mambo wanayoyafahamu yaliyopelekea ushindi wao na ambayo wakiyasema yanaweza kupunguza credibility ya mtu wao?
 
Bashe ana stahili kua waziri

Bashe si alikuwa ana msupport Lowassa leo hii ghafla kagehuka a pro Dk.Magufuli?

Bashe aendelee na Ubunge wake, cabinet ya JPJM a recruit watu wanao msupport by 100% asiweke mawaziri watakao tumiwa na maadui wa Rais kumuhujumu/kumpa ushauri potofu.
 
Naona ishu ya Adadi Rajabu inazidi kuvuma tu maana kulikuwa na tetesi kwamba jamaa alikuwa anajua atapewa hiyo wizara ya Kitwanga
 
Back
Top Bottom