Tetesi: Mabadiliko Baraza la Mawaziri; J. Makamba, Mhagama, Ummy Mwalimu nje; Adadi Rajabu, Bashe watajwa

Tetesi: Mabadiliko Baraza la Mawaziri; J. Makamba, Mhagama, Ummy Mwalimu nje; Adadi Rajabu, Bashe watajwa

Rabda awachague na wabunge wa Ukawa nao waingie kwenye baraza la mawaziri tofauti na hapo atapangua mpaka achoke maana chama kimekuwa chakavu na waliopo kwenye chama nao wamechoka
 
Natumaini makubwa na Dr Magufuli safari hii atanikumbuka.Wakuu wa Mikoa nilisahaulika kiduchu,Makatibu Tawala wa Mikoa nikakoswa koswa sasa ni zamu yangu Wizara ya Mambo ya Ndani nataimudu bila mbwembwe sitakunywa Konyagi wala Safari chonde chonde Dr usinisahau katika ufalme wako.

Mkuu na mimi pia nina matumaini kama yako. Nimekua nikisubiria za ubalozi, naona kimya. sasa hii reshuffle ya cabinet ikifanyika unaweza jikuta nawe uko ndani ya nyumba!
 
Magufuli akimpiga chini January ndiyo nitaamini jamaa ni mtu anayefanya anachoamini. Uthubutu huo hana. Jamaa anamuogopa January kuliko hata panya wanavyoogopa paka.
Hilo haliwezi kutokea Tanzania hii ya Magufuli maana anajua akimwaga ugali January atamwaga mboga, maji ya kunawa, ya kunywa na kutupa sahani jalalani Huku akienda kumshitakia Kwa zile kamati za Ufundi toka Gambia na kwingineko Duniani , ni vigumu kumgusa January Makamba na Kama asingekuwa Mbunge Leo hii angekuwa kampa cheo cha katibu mkuu kiongozi au hata ugavana BOT, chezea January Wewe .....
 
Ummy Mwalimu tumpe muda,...
Hata mimi nadhani, bado anafanya vizuri na sidhani kama katika mawaziri waliokosea unaweza kumuweka humo. Wizara ya afya ni mtambuka, huwezi kuona impact baada ya mda mfupi wa yeye kuwa waziri, lakini nadhani Ummy anajitahidi.

Shida yangu ni Kigwa, simkubali sana na sidhani kama kweli ana uwezo japo anayajua mengi kuhusu afya.
 
Magufuli akimpiga chini January ndiyo nitaamini jamaa ni mtu anayefanya anachoamini. Uthubutu huo hana. Jamaa anamuogopa January kuliko hata panya wanavyoogopa paka.

Endelea kujitekenya na kucheka mwenyewe.... Subiri muda hutaamini macho yako
 
Hakuna mabadiliko makubwa labda za sura ila kiutendaji labda amchague Lema, Zitto na Mbatia ila ndani ya CCM mmmm ila wamo akina Good luck mzee wa sanamu ya Diamond na Agness Marwa ili akazane kulia
 
Hilo haliwezi kutokea Tanzania hii ya Magufuli maana anajua akimwaga ugali January atamwaga mboga, maji ya kunawa, ya kunywa na kutupa sahani jalalani Huku akienda kumshitakia Kwa zile kamati za Ufundi toka Gambia na kwingineko Duniani , ni vigumu kumgusa January Makamba na Kama asingekuwa Mbunge Leo hii angekuwa kampa cheo cha katibu mkuu kiongozi au hata ugavana BOT, chezea January Wewe .....

Yule mganga wa Gambia noma, viongozi wote walikua wanakimbilia kwake
 
Unaweza kumuona ana bahati mbaya,lakini ndiye mwenye siri ya ushindi wa CCM.Yeye ndiye aliyeratibu vitengo vyote vilivyotumika kumpa ushindi mukulu,wasipomuangalia kwa jicho la tatu anaweza kumwaga mboga na ugali wote wakakosa msosi.
Acheni kumvika kilemba cha ukoka January ,Kakatwa Lowasa na nchi imetulia ndio ije kuwa kwa huyu January ?
Watu wakiamua atakatwa na atatulia afungue mdomo tu halafu ataelewa nini maana ya kugusa chochote kinacho hatarisha usalama wa nchi
 
Back
Top Bottom